Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,258
Nimekuwa nafuatilia sana vipindi mbalimbali hasa vya mahojiano katika TBC ONE/TAIFA, kwa mijadala mbalimbali ya siha, kwa kufanya hivi nimebahatika pia kufanya uchambuzi wa watangazaji mbalimbali na wengi kuvutiwa nao na wengine kuona kuna maeneo wanayohitaji maboresho kidogo. Wenzetu huwa wanaangalia sana hasa vipindi vya mahojiano kumpeleka mtu mwenye taaluma husika kufanya mahojiano na mlengwa wake
Hata hivyo bado sijavutiwa sana na kamaradi Gabriel Zacharia, ninaona muda mwingi akiwa kama muoga hivi anapowahoji walengwa mbalimbali na hujikita sana kwenye maswali aliyoandaa, aidha mara nyingi simuoni akiwa na umakini kwenye swali alilouliza yaani akishauliza anasubiri mjibu swali amalize ili amuulize swali linalofuata bila kufanya analysis ya majibu (kuuliza alimradi maswali yaishe) sidhani kama ni nidhamu ya woga iliyojengeka kwa TBC sasa au la....
Nadhani Kamaradi Gabriel bado anayo nafasi ya kuonyesha zaidi ya taaluma akiwa kwenye anga zake (kipaji)........moja ya sifa kuu zinazowabeba watangazaji wengi kama Larry King etc ni kuonesha vipaji vyao halisi wanapopewa rungu (smartness upstairs)
Nakutakia kila la heri unapotafakari haya....