Niliwahi kuwa mraibu wa makamari haya ya karata,makamari makubwa ambayo yalinirudisha nyuma kimaendeleo pamoja na kuondoa uaminifu kwa watu ambao ni muhimu sana,majuto ya hali ya juu na maumivu ya hali ya juu zaidi,nilikuwa na marafiki ambao nikiwa na hela na nikiwa nashinda mara kwa mara kwenye hayo makamari huwa wana ni heshimu,kunisifia juu ya uwezo wangu pia na kunikubali kuwa me ni wina,nishavunja{kushinda} sana kwenye makamari makubwa makubwa,ila sijawahi kuingia CASINO na kucheza kamari,ila nikianza kupunwa na kuishiwa kabisa nilikuwa nanyanyasika,kutengwa na mifano mengine ifananayo na hayo,nilitamani saana niache huo mchezo wa haramu,nilisha acha na kurudi mara kwa mara.Niwahi kuyaona hayo MADUBWI na hata kukaa nayo karibu ila hayo MADUBWI {MABONANZA} sikumbuki kama nishawahi kucheza kwa kuwa siwezi kusubiri mia mbili {200} ambazo zinazotoka mule hata kama zikiwa na uwezo wa kufika Million,napambana na nafsi yangu kule nisirudi,maisha ya mateso na manyanyaso,watu washaliwa hela muhimu.Mtu unaweza kufanya tukio la kuogopeka,kukutana na watu ambao wanafanya shughuri mbali mbali ambazo si za halali.
Naona watu wanasifia tu sijui CHAFU TATU {3}
Nikisema imenirudisha nyuma basi muelewe,na ukipata hela yake sidhani kama unafanyia kitu cha maana.
Piga vita kamari.