Kamari za Radio One, Clouds FM na EFM

Kamari za Radio One, Clouds FM na EFM

DINHO

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
880
Reaction score
1,750
Habari zenu wadau,

Pamoja na habari hii mimi nimekuwa mtu wa kufuatalia sana masuala ya uchumi ambapo ndio kada yangu niliyobobea ingawa si kwa kiwango kikubwa saaaana.

Mwaka jana, kuliibuka kamari/bahati nasibu ambazo binafsi sikuelewa msingi wake hasa ni nini.

Bahati nasibu hizi zinaendeshwa na Radio za hapa nchini hasa Clouds Fm (MCHONGO PESA) EFM (PESA MSHINDO), RADIO ONE nk.

Nyongeza ya Hapo tuna bahati nasibu ambazo ni TATU MZUKA nk

Hoja yangu ni kwamba kwa sheria zetu za Kampuni ni lazima kampuni iweke wazi shughuli zao rasmi zinazoiingizia kipato, sasa basi hizi kamari ambazo zinaendeshwa na hizi Redio zimesajiliwa kwa mtindo upi?
Na je kodi yake inalipwaje? Kwanini mshindi halipi kodi kutokana na kipato chake kama sheria inavyotaka.

Lakini kubwa zaidi kwanini iwe kila redio wawe na huu ujinga, ambao wanainchi makumi kwa maelfu wanaibiwa pesa zao kwa mgongo wa kudanganywa kuwa pesa za mchongo ni za bure?

Serikali kupitia wizara ya Fedha kwanini wasitoe tamko rasmi juu ya hizi kamari ambazo sasa tunaweza ziita kama MUSHROOMING WAMBLING? TRA watoe ufafanuzi on how they collect taxes as kodi ni suala la wazi bila kificho. Kampuni ipi hasa imesajiliwa kwa biashara hizi as all we know kazi za hizo Redio ni kurusha matangazo ya habari nk.

Je, hizi redio sio kwamba wanatumia mgongo wa hizi kamari kujipatia fedha kwa ajili ya kulipia mishahara ya watumishi wao au kutakatisha fedha haramu?

Wadau wa maendeleo ningeomba tuchangie hoja hii kwa utulivu huku tukitafuta suluhisho la huu wizi wa wazi kwa Watanzania.

Hii nchi haiwezi endeshwa kienyeji kiasi kwamba mtu anaamua kujitafutia pesa kwa nyia za hovyo na ambazo hazina well verifacation ya ushindi kama ilivyo kwa football/basketball betting, ambazo mshindi anaona kwa uwazi ameshindwa au ameshinda.

Sambamba na hilo kwanini sasa hiyo michezo isiendeshwe na bodi ya bahati nasibu ili kuweka uwazi, na badala yake iendeshwe na wapumbavu kama MWIJAKU, DA HUU, MAESTRO, KISHAMBA, OSCAR OSCAR, KITENGE na wajinga wengine.

BODI YA BAHATI NASIBU IKO WAPI KUWEZA KURATIBU HIZI BAHATI NASIBU.

Nawasilisha.
 
kamari zina regulator wake (Gaming Board) na kuna sheria inayosimia hiyo michezo, na jinsi ya kutoza kodi kuafatana na aina ya kamari unayofanya (slots. table, online n.k)
Sasa hivi radio/TV zimegundua kwamba kamari ndio trusted source ya income, Mteja (msikilizaji) unaambiwa lipa buku just to chase the shadow, hoping to pocket 500,000/=
Unapocheza kamari, nafasi ya muendesha kamari kushinda ni kama 97 % na wewe mtoa buku ni kama 2- 3%. Piga hesabu hapo. uone watu wanavyopumbazwa kupoteza hela
 
kamari zina regulator wake (Gaming Board) na kuna sheria inayosimia hiyo michezo, na jinsi ya kutoza kodi kuafatana na aina ya kamari unayofanya (slots. table, online n.k)
Sasa hivi radio/TV zimegundua kwamba kamari ndio trusted source ya income, Mteja (msikilizaji) unaambiwa lipa buku just to chase the shadow, hoping to pocket 500,000/=
Unapocheza kamari, nafasi ya muendesha kamari kushinda ni kama 97 % na wewe mtoa buku ni kama 2- 3%. Piga hesabu hapo. uone watu wanavyopumbazwa kupoteza hela
Na ndio maana nimetaka waweke wazi utaratibu nzima wa kusajili hizo Radio kuwa wachezesha kamari.
 
Kama sio mvivu wa kusoma, Tafuta Gaming Act Chapter 41 Revised edition 2019 yote hayo yamo humo.
Nilijaribu kupitia kwakweli, na nikiri wazi hizo sheria inapaswa kurekebishwa kwa kuangalia hali ya uchumu wa wananchi na sio tu kukusanya kodi bila kuzingatia usawa wa kiuchumi na madhara yake.
Hata madawa ya kulevya ya mkwanja mrefu mno ila yanazuiliwa kutokana na athari zake kwa jamii.

Hii inaitwa SMS lotteries, changamoto iliyopo kwanini hatuna standards za nani afanye hii biashara na kwa mtaji gani nk.
Ikumbukwe biashara ya mikopo hii chap chap au mikopo umiza hizi ndogo tu, zina utaratibu wake ambapo kuna kiwango cha mtaji mtu au kampuni anapaswa kuwa nayo kabla ya kuanza hiyo biashara, hali kama hiyo haina tofauti na Sports betting.

Hapa kwenye SMS LOTTERIES kuna kiwango ambacho wamewekewa kwamba kabla ya kufanya biashara hii lazima uwe na kiwango fulani cha mtaji?? Na je Sheria inatambua wazi makampuni tofauti na ya kamari hulipa kodi zao kila mwaka na kwa awamu nne mara baada ya kuproject au kupata faida. Hali hii ni tofauti na Kamari ambapo hulipa kila mwezi au wiki.
Je hawa Claudz, EFM wamesajili hizi kamari as separate entity au ipo ndani ya hizo Radio zao?
Utaratibu wao wa kusajiliwa ulizingatia vigezo muhimu. Pamoja na hilo, SMS LOTTERIES zinapaswa kuchezwa kila mtu aone ni kwa usahihi gani hakuna upangaji wa matokeo.
 
mtoa hoja ni muathirika namba moja
Binafsi hata siamini kwenye hizi kamari za kuamuliwa na utashi wa mtu, na hapa ndipo hoja yangu ilipo. Binafsi nimefuatilia sana namna gani hizi kamari zinaendeshwa na nimegundua huu ni utapeli wa kiwango cha juu mno.
 
Sasa kwa nini uwaite hao watangazaji wajinga? nani alikuambia wao ndio wanaendesha hiyo Michezo? kwanini hukuamua kufuatilia kabla ya kuliltea hapa?
 
Sasa kwa nini uwaite hao watangazaji wajinga? nani alikuambia wao ndio wanaendesha hiyo Michezo? kwanini hukuamua kufuatilia kabla ya kuliltea hapa?
Wao ndio wanaendesha. Mi pia nachukizwa na hizo kamari za kijinga.
 
bora leo umeliweka hapa

radio zimegeuka kuwa magenge ya wachezesha kamari
 
Ujinga wa Wasikilizaji na kupenda Vitonga, mitelezo a.k.a Ganda la ndizi ndio Mtaji pekee wa hizo Biashara..

Na Wajinga ni wengi sanaaa na kila siku wanakuja wapya...

Ukifanya investment kwa wajinga lazima ikulipe tu siku zote,, kwasababu huwa ni wengi na kila siku ongezeko lao ni kubwa....
 
Binafsi hata siamini kwenye hizi kamari za kuamuliwa na utashi wa mtu, na hapa ndipo hoja yangu ilipo. Binafsi nimefuatilia sana namna gani hizi kamari zinaendeshwa na nimegundua huu ni utapeli wa kiwango cha juu mno.
mkuu kama huna imani achana nazo, hata mimi sina imani nazo, sichezi kabisa
 
Back
Top Bottom