Kamasi la kijani puani; je ni uchafu au ugonjwa?

Kamasi la kijani puani; je ni uchafu au ugonjwa?

G.Jacob

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2013
Posts
3,618
Reaction score
3,478
Nakumbuka nilipokuwa nasoma somo la lugha ya Kiswahili kulikuwa na misemo (hapa namaanisha nahau, methali, vitendawili na misemo yenyewe) mingi sana inayoambatana kwenye ufundisha wa lugha hii. Sio mzuri sana kwenye kutunza kumbukumbu kwa sababu misemo mingine inakuwa kama swali unalotakiwa kulijibu (mfano kitendawili lazima ukitegue, na fumbo lazima ufumbue), hapo kwenye majibu ndipo kwenye mgogoro kwangu.


Unaweza usiamini lakini ukweli ndio huu, huu msemo niliukumbuka kana kwamba nimetoka darasani jana tu, pale nilipokutana na jamaa mmoja pale kidongo chekundu kata ya Gerezani. Nilipomuona tu nikakumbuka kitendawili fulani hivi i.e “mzungua anachungulia dirishani = kamasiii”,,,,,tatizo likaja kwenye rangi ya hilo kamasi lenyewe bwana dooooooh! la kijaniii.


Unaweza usile kwa wale wenye kinyaa kilichopitiliza, lakini pia unaweza ukatapika hapohapo kama ukiliona linachungulia puani, halafu cha kushangaza muhusika yuko poa tu daaaaah! Hata tukisema ndo uchafu wandugu huu umepitiliza kusema kweli, labda kama ni ugonjwa wahusika wa tiba mtatudadafulia hapa lakini usiombe ukutane na mtu wa aina hii halafu ukirudi nyumbani unakuta mkeo kapika ugali na mboga ya mrenda wa bamia, hahahaha ! sidhani kama utalika.
 
Kamasi lile tulilokuwa tukiita la kizungu ni NJANO! Inzi wa KIJANI ndiyo alijulikana kama INZI WA KIZUNGU......
 
ni ugonjwa na ni njia ya mwili kutengeza nasal mucosa nyingi ili kuondoa maambukizi ya vijidudu!
 
dah haya magonjwa mengine sasa, mtu unaweza kutapika hadi nyongo
 
Itakuwa madhara ya bangi hayo! Make mmea siku zote ni kijani ule!
Ukikutana nae tena komba ukalie ugali! Sijui umefikiria nini kufananisha kamasi na mboga ya mlenda.
Unautani na wazigua wewe make wana mlenda wao huo unaitwa hombo mmmh aiseee simaliziii, ngoja waje wenyewe!!
 
Back
Top Bottom