Kamata kamata tinted taa za Magari

Kamata kamata tinted taa za Magari

Siafu na Manga

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
2,884
Reaction score
8,956
Kwa wale waliobahatika kuwa na usafiri kama umebandika tinted kwenye taa za mbele na nyuma kuna msako wakukamata unafanywa na polisi
6269c6fd-a39e-455c-aa5e-941e61752769.jpg

c63ddae1-be2f-4519-8235-8dc99c6381e7.jpg

787ea8de-33a3-4358-a2ae-199b95ad60a3.jpg

---

Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani limesema litaendelea kuwakamata madereva wa magari wanaoweka ‘tinted’ kwenye taa za mbele na nyuma pamoja na wote wanaoweka namba aina ya 3D kwenye magari.

Mkuu wa Elimu ya Usalama Barabarani, Kamishina Msaidizi wa Polisi Michael Deleli amesema ni kosa kisheria kufanya mabadiliko na kubadilisha uhalisia kwenye gari kwani huongeza hatari hususan nyakati za usiku.

“Plate number mtu anachukua dukani vizuri kabisa anaiwekea namba zingine, badala ya ile ambayo imechapichwa dukani, lakini ananunua zipo saizi zinachongwa za vioo na herufi zile zinakuwa na ujazo, zote hizo tunafanya oparesheni kuziondoa,” amesema Kamishna.

Ameongeza, “Herufi tu ile inatengenezwa kwa viwango, lakini mtu ameingia tu kati na yeye anaanza kufanya biashara [..] watu waheshimu sheria na kanuni zetu, wasijifanyie kama jinsi wanavyotaka.”
 
Safi kabisa, huwa napata wakati mgumu barabarani haswa wakati wa mchana unakuta mtu kaonesha anakata upande fulani ila kwa sababu ya sticker alizoweka huoni vizuri na inaweza kusababisha ajali.
 
Back
Top Bottom