Kamata kamata tinted taa za Magari

Kamata kamata tinted taa za Magari

1690901223661~2.jpg

Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani limesema litaendelea kuwakamata madereva wa magari wanaoweka ‘tinted’ kwenye taa za mbele na nyuma pamoja na wote wanaoweka namba aina ya 3D kwenye magari.

Mkuu wa Elimu ya Usalama Barabarani, Kamishina Msaidizi wa Polisi Michael Deleli amesema ni kosa kisheria kufanya mabadiliko na kubadilisha uhalisia kwenye gari kwani huongeza hatari hususan nyakati za usiku.

“Plate number mtu anachukua dukani vizuri kabisa anaiwekea namba zingine, badala ya ile ambayo imechapichwa dukani, lakini ananunua zipo saizi zinachongwa za vioo na herufi zile zinakuwa na ujazo, zote hizo tunafanya oparesheni kuziondoa,” amesema Kamishna

Ameongeza, “Herufi tu ile inatengenezwa kwa viwango, lakini mtu ameingia tu kati na yeye anaanza kufanya biashara [..] watu waheshimu sheria na kanuni zetu, wasijifanyie kama jinsi wanavyotaka.”
 
Attachments

  • 1690901223661.jpg
    1690901223661.jpg
    61.7 KB · Views: 21
Wahuni tu.
Kituo kinachofuata ni walioweka tints kwenye windscreens 😎😎
 
Attachments

  • FB_IMG_1690821017872.jpg
    FB_IMG_1690821017872.jpg
    86.9 KB · Views: 14
  • FB_IMG_1690821020758.jpg
    FB_IMG_1690821020758.jpg
    110 KB · Views: 18
  • FB_IMG_1690821026799.jpg
    FB_IMG_1690821026799.jpg
    45.6 KB · Views: 10
  • FB_IMG_1690821023528.jpg
    FB_IMG_1690821023528.jpg
    98 KB · Views: 10
WOTE WANAUWEKA 3D NI WAPUMBAVU WASHAMBA NA MATAIRA MALIMBUKENI... KUNA UPUMBAV NI MTOTO MDOGO WA DARASA LA 4 NDIO ANAWEZA KUFANYA...
Mtu una miliki ki crown IST passo rush au xtrail unaweka mbwembwe, what if ukija kumiliki brand kubwa??
 
Punguza jazba. Point yako ipo wapi? We sema tu 3D inahatarisha maisha ya watumia barabara hivi na vile. Basi.
 
1690902257318.png

3D Plate number
1690902382715.png

Taa zilizoTinted
Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani limesema litaendelea kuwakamata madereva wa magari wanaoweka ‘tinted’ kwenye taa za mbele na nyuma pamoja na wote wanaoweka namba aina ya 3D kwenye magari.

Mkuu wa Elimu ya Usalama Barabarani, Kamishina Msaidizi wa Polisi Michael Deleli amesema ni kosa kisheria kufanya mabadiliko na kubadilisha uhalisia kwenye gari kwani huongeza hatari hususan nyakati za usiku.

“Plate number mtu anachukua dukani vizuri kabisa anaiwekea namba zingine, badala ya ile ambayo imechapichwa dukani, lakini ananunua zipo saizi zinachongwa za vioo na herufi zile zinakuwa na ujazo, zote hizo tunafanya oparesheni kuziondoa,” amesema Kamishna.

Ameongeza, “Herufi tu ile inatengenezwa kwa viwango, lakini mtu ameingia tu kati na yeye anaanza kufanya biashara [..] watu waheshimu sheria na kanuni zetu, wasijifanyie kama jinsi wanavyotaka.”
 
Madhara ya tinted za taa ni yap? Mda mwingine maelezo ya kutosha husaidia utii bila shurut...
 
Back
Top Bottom