Kamata kamata tinted taa za Magari

KWANI TBS HAIKUHUSISHWA?
 
Bora langu halina hata hizo plate namba
 
Wazee wa 3D nao wanasakwa.. hii ndo bongo ipo siku watakamata wanaojaza mafuta full tank tupo hapa si mtaonaaa[emoji16]
Tatizo wanaiga chuga.
Si unaona hata pikipiki zinavyokatwa hadi inakywa inapakia dereva tuu nabtena dwreva mwenyewe bado anakaa kwa shida
 
we huoni kama wameingilia tenda za watu? Japo namba za 3D zinaonekana ni bora na za kisasa lakini hazijaidhinishwa na tbs na pia hao jamaa wanaofoji namba hizo hawakupewa tenda hiyo
Ni kweli
 
😅🤣 ONA WAPUMBAVU WALIOWEKA 3D NA TINTED wanavyo jitetea ushenz mtupu... Huna akili kama hujui madhara ya 3d na Taa za tinted... Huna akili kabisa
Umeshaambiwa ni 'unyama' Shida za kukulia kijijini zinakusumbua.
 
Mfahamu pia number plates zimetengenezwa in such a way that haziungui kirahisi. Yaani gari yaweza Waka moto lakini yale maandishi yaliyotuna yakawa yanasomeka vizuri tu. Kitu ambacho kwa hizi 3d sidhani kama zina ubora huo.
3D haifuti namba ya awali, wala haibadili kibati cha awali. Zile block zinagandishwa tu juu ya herufi/namba zilizopo. Hata ukiamua kuzitoa unabandua tu 3D inabaki namba ya awali. Kwa hiyo swala la plate number kutoungua liko pale pale.
 
Changamoto za 3D ni poor visibility at certain angles pia nyakati za usiku tatizo linaongezeka zaidi.

Hii ni simple model nimefanya kwenye program kuangazia uonekanaji wa 3D vs non 3D plate number kwa nagle tofauti tofauti.

NON 3D



3D



NON 3D



3D




NON 3D



3D



Kama zinavyoonekana hapo nimejaribu kuweka angle tofauti tofauti, kwa plate number zenye raised 3D letters na zile za kawaida.

Hitimisho
3D letters zina mwonekano mzuri na wakuvutia ila zina changamoto ya kushindwa kusomeka kwenye angle fulani, na pia wakati wa usiku.

Solution
3D letters zinatengenezwa na aina ya vioo vya plastic vinavyojulikana kwa jina la acrylic panels zipo rangi kadhaa na pia zina thickness tofauti.
ili kutatua changamoto ya kutoonekana vizuri inabidi zitumike panel zenye thickness ndogo.

Mamlaka husika sioni haja ya kuzuia utumikaji wa hizi 3D raised letters endapo zitarekebishwa changamoto za uhafifu wa kuonekana kwake.

Nawasilisha.
 
You are great thinker.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…