KERO Kamata-kamata ya Bodaboda Kariakoo kuna upendeleo, wanaotoa kitu kidogo wanaachwa zingine zinabebwa

KERO Kamata-kamata ya Bodaboda Kariakoo kuna upendeleo, wanaotoa kitu kidogo wanaachwa zingine zinabebwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

mirindimo

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2009
Posts
1,155
Reaction score
2,704
Kamata-kamata ya Bodaboda na Bajaj mitaa ya Kariakoo kuna double standards, zipo zinazoachwa kwa wanaotoa kitu kidogo lakini zingine zinabebwa.

Meza bado zimepangwa njiani



 
"Nimesimama dukani nichukue mzigo, Jiji wamebeba Pikipiki yangu, wanasema nilipe Sh 50,000

Mimi ni dereva wa Taksi Mtandao, leo (Oktoba 7, 2026) nilienda Kariakoo, kuchukua mzigo wa mteja karibu na Msimbazi pembeni kabisa mwa Barabara, sio kwenye barabara kuu wala katikati ya njia, nikaingia dukani nifunge mzigo kisha niondoke.

Cha kusikitisha na kushangaza, nilipotoka dukani nikakuta Maafisa wa Jiji wameibeba na kuipakia kwenye gari lao, nilipouliza kulikoni wakawa wananijibu kwa ukali kuwa "Tukutane ofisini".

Wakati huo kuna pikipiki na bajaji nyingi zimepaki n ahata magari tena mengine yameegeshwa vibaya lakini inakuwaje wanachagua pikipiki za baadhi ya watu na kuzichukua huku zingine wakiziacha?

Sisi Taksi Mtandao ukifika sehemu ukasimama hata kuzungumza na mtu kwenye simu kama ni Mteja wako umuulize alipo hapohapo wanakukamata.

Hali hii inatukatisha tamaa sana sisi vijana tunaojitafutia riziki kwa halali, ajira hakuna, tunapambana kujiajiri kwenye usafiri wa mtandao, lakini badala ya kututengenezea mazingira mazuri na rafiki ya kufanya kazi, Serikali hiyohiyo inatunyanyasa.

Mamlaka zinazohusika ziangalie kero hii ya Kariakoo na kutupatia mazingira stahiki ya kufanyia kazi."
 
Pole sana mkuu, ila pikipiki kariakoo zinakera sana, hazina tofauti na wamachinga wanavyokera na meza zao.
 
Hamuaminiki nyie.. Mkiwekewa mafuta ya Buku5 tuu mnakua machawa...
 
Back
Top Bottom