Kamata kamata za watuhumiwa wa ufisadi NYS zaanza

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Yaani kama kuna kitu kilikua kimenichosha kwenye huu utawala ni hili la mafisadi kupeta tu ilhali wamekwapua mfuko wa taifa. Binafsi naomba kuona watu wakinyea debe jela, wasiishie mahakamani tu, na mali zao zitaifishwe, yaani hela ya serikali iwe chungu, iwe na ukakasi, we need to see blood.

Wakenya tuunge mkono hizi jitihadaa bila kujali kama watuhumiwa ni ndugu zetu wala nini, kamata na kuwasomba wote ndani, ikiwezekana wapokee vibao na viboko pia, hata wenye madaraka yashushwe tu.
Hizi kamata kamata zisiishie NYS, naomba kimbuga kipitie kila wizara na idara, kije hadi mitaani nipo radhi kulipa gharama kama hata na mimi kitanikuta.

  • Ms Lillian Mbogo Omollo, Katibu mkuu
  • Mr Richard Dubai, NYS Director-General
  • Mr Sam Muchuki
  • Mr Peter Muchui
  • Mr Matano Odoyo, NYS
  • Mr James Thuita Nderitu, businessman
  • Ms Yvonne Wanjiku Ngugi, businesswoman
  • Mr Sammy Mbugua
  • Mr Timothy Kiplangat Rotich
  • Mr Wellanalo Mulupi, NYS
  • Mr David Kirui
  • Mr Ferdinard Matavo
  • Ms Keziah Mwangi, NYS
  • Mr Duba Galgalo
  • Mr Isaiah Adalo Chopia
---------------------------------

Police on Monday pounced on suspects named in the ongoing National Youth Service probe after the DPP ordered their immediate prosecution.

Thirteen of the suspects were arrested in Nairobi while four were nabbed in Naivasha.

The NYS Director-General Richard Ndubai is among those who have been arrested.

The suspects have been taken to DCI headquarters on Kiambu Road, Nairobi.

Names of those arrested in NYS probe
 
Tell the guy to come to borrow a leaf or two from a bulldozer.
 
Tell the guy to come to borrow a leaf or two from a bulldozer.

Huko kwenu kuna nini cha kuiga zaidi ya show za media za PR, maana kuna kipindi niliskia mtaanzisha mahakama ya mafisadi, leo hii hiyo mahakama imewahukumu mafisadi wangapi, maana ilianza kwa mihemko na kukamata kalasinga halafu baada ya hapo ikafa kifo cha mende.
 

Mafisadi wanahaha huku, siyo kama huko hot bed for looters. Huku sisi kula PESA ya umma ni sawa na kula sumu ya panya.
 
Kuna watu wanayea debe hivi sasa na sio watu wadogo. Mna chakujifunza Tanzania, hakuna huonea aibu rushwa.
 

Wewe kama hujaiba uraia Kenya utakua umeiba uraia Tanzania, Juzi JPM amesema kuna watu wamepewa mali za ccm na hajui kama wana hata kadi za ccm maana hata sio raia nahisi alikua nakulenga wewe.

yaani uraia wako una mashaka, hakuna mkenya mwenye mwandiko kama huo labda angeandika kingereza. una muandiko wa kitanzania lakini unajiita Mkenya
 
Kuna watu wanayea debe hivi sasa na sio watu wadogo. Mna chakujifunza Tanzania, hakuna huonea aibu rushwa.

Nimeomba mnipe mfano wa watu mliokamata na kutaifisha mali yao na kuwafunga gerezani kwa kutumia hiyo mahakama ya mafisadi.
Usinipe zile PR show zenu za kalasinga na Ruge.

Sasa utawala wa awamu ya tano unakaribia kumaliza hatamu ya kwanza, naomba facts za akina nani mumetaifisha mali yao kabisa.
 

Unapindisha mandhari ya mada, Kiswahili ni lugha ya taifa Kenya na pia ni lugha ya asili ya baadhi ya jamii zetu za Pwani, walihusika kwenye kukibuni.
Turudi kwenye mada....
 
Wenye walichagua Jubilee ndio wametuletea hiii shida yote Kenya...very stupid
.. Nablame waliowapigia kura... Kufungwa macho ati kumira kumira. Ona shida sasa.. Hizi za kushikwa tumezoea. Inaeza kua ameshikwa lakini anaenjoy life hapo ndani.. The president should act... Hawa watu wanatumaliza. Wakenya wangekua wajanja tungepigia watu kama miguna kuwa president
 
It's their last term. Hao wanashikwa ni small fish.. There are bigger fish out there. Utasikia story imepotelea hivyo tu... Ama wameachiliwa ati hakuna evidence
 
MK254 huyu Ndio Mkenya Hali’s I

Freddie998 kuchagua Huyo Miguna ningekua mnalia kama one of your neighbors sitaki kuwataja
 
Mbona wengi tu, kuna mawaziri Yona na Mramba walifu nyingi mpaka walipo badilishiwa kufanya kazi za kijamii community service. Mwaka huu tu, Kuna mtu wa CRDB amehukumiwa 93 years. Kesi za TRA, BOT, TBC, IPTL na zingine nyingi bado zinaendelea mahakamani hivi sasa, wengine mnawaficha huko Kenya. Ufisadi Tanzania kwa sasa unapumulia mashine, Kenya bado mnasafari ndefu kuonyesha dunia kama kweli mmepania kumaliza ufisadi.
 
Hilo la kesi kuendelea mahakamani ni jambo la kawaida hata huku tuna zaidi ya kesi 400 mahakamani kwa ajili ya watuhumiwa wa ufisadi, mimi nilitaka unionyeshe kipi mumefaulu cha zaidi, kama vile kutaifisha mali, unaishia kuniambia watu walipewa kifungo cha kufanya kazi za jamii, community service, like seriously mtu ameiba mabilioni unampa adhabu ya kufagia, a slap on the wrist, halafu unakuja kujisifia hapa eti mnapigana na mafisadi.

Hii awamu mlianza kwa mbwembwe nyingi sana, nimejaribu kutafuta nini mlifanikisha tofauti na ilivyokua hapo awali sijakiona, zaidi ya PR za kuzunguka na wana habari mkishtukiza. Juzi hapa tuliona ukuaji wa uchumi wenu umeshuka zaidi ya hatamu na awamu zote, ukaishia kubwabwaja eti ni kwa sababu mumewaondoa wawekezaji hewa.
 
MK254 huyu Ndio Mkenya Hali’s I

Freddie998 kuchagua Huyo Miguna ningekua mnalia kama one of your neighbors sitaki kuwataja
Haha. Inafaa watu waangalie siku zijazo. Hawafai kupiga kura kwa misingi ya kikabila. Hivi vitu ati stronghold ya mtu ni tribe yake inaudhi. Tukipigia viongozi wa kweli tutaenda mbali
 
Tell the guy to come to borrow a leaf or two from a bulldozer.
Sizonje is the gratest thief of all. Since 1995 he steal public money and misuse public funds unashsmedly with impunity.

And just recently he has broken record by stealing 1.5 Trillion + for a very short period in his tenure.

Katia fora katika tasnia ya wizi
 
pumbaff!!! hivi hujawahi kuona hata watz wanaoandika kiingereza kizuri sana hapa JF...kisha utambandikaje uraia wa tanzania mtu usiomjua kwa sababu ya mwandiko wake?...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…