Hilo la kesi kuendelea mahakamani ni jambo la kawaida hata huku tuna zaidi ya kesi 400 mahakamani kwa ajili ya watuhumiwa wa ufisadi, mimi nilitaka unionyeshe kipi mumefaulu cha zaidi, kama vile kutaifisha mali, unaishia kuniambia watu walipewa kifungo cha kufanya kazi za jamii, community service, like seriously mtu ameiba mabilioni unampa adhabu ya kufagia, a slap on the wrist, halafu unakuja kujisifia hapa eti mnapigana na mafisadi.
Hii awamu mlianza kwa mbwembwe nyingi sana, nimejaribu kutafuta nini mlifanikisha tofauti na ilivyokua hapo awali sijakiona, zaidi ya PR za kuzunguka na wana habari mkishtukiza. Juzi hapa tuliona ukuaji wa uchumi wenu umeshuka zaidi ya hatamu na awamu zote, ukaishia kubwabwaja eti ni kwa sababu mumewaondoa wawekezaji hewa.