Nilishasema Mama anahujumiwa. Ninarudia tena MAMA ANAHUJUMIWA. Kuna cartel inasukuma kete zake kwa ustadi mkubwa sana kumharibia mama kipenzi cha watanzania. Hii ishu ya kuzuia waumini wa kanisa la Gwajima kuabudu inaichafua zaidi serikali ya mama. Kama Gwajima ndo mwenye kosa basi akamatwe yeye ila kanisa lake liendelee kuhudumia waumini kama kawaida.
Kufungia makanisa hadi huko mikoani ni sawa na kuwaamsha hata ambao walikuwa hawana haja ya kufuatilia mambo yanayoendelea. Kuna waumini wengi tu wa haya makanisa ni kama kondoo ambao hawataki kabisa mambo ya vurugu wala siasa. Wao ni kufanya shughuli zao binafsi, kusali na kutoa sadaka kwa Gwajima. Watu kama wanahatarisha vipi amani?
Ninatumaini jumapili ijayo hakutakuwa na aibu iliyojitokeza jana.