Kamati kuu CHADEMA wataka wote walioingiza nchi katika mkataba huu mbovu kuchukuliwa hatua

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648


akisoma maazimio hayo leo 14/7/2023 katika mkutano wa CHADEMA na Waandishi wa Habari juu ya maamuzi yaliyofikiwa na Kamati Kuu kuhusu Mkataba wa Bandari amesema, Kamati Kuu ya CHADEMA imeazimia serikali kuwachukulia hatua wote walioigiza nchi hii kwenye mkataba mbovu ambao haurekebishiki, mkataba ambao ni mbovu mpaka unafanya watu milioni 60 kuonekana watu wa ajabu.

Akiongeza kuwa haiwezekani watu hao wameingiza nchi katika mkataba huu mbovu na bado wameachwa tu mpaka sasa.
 
Kumekucha
 
Akiongeza kuwa haiwezekani watu hao wameingiza nchi katika mkataba huu mbovu na bado wameachwa tu mpaka sasa.[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watawajibika hayo mafisadi yanaolenga kuuza nchi kwa waarabu
 
Samia aendelee kuziba masikio, ajue na kelele ndio zinazidi toka kila upande.

Wakati wakiwatisha wengine kwa kupekua nyumba zao, huku wengine ndio wanaamka, huwezi kuwageuza watanganyika watumwa ndani ya nchi yao kisha wakutazame tu kama mazezeta, haiwezekani.

Samia kwa ule mkataba wa hovyo ametukosea na ni lazima auvunje, amegeuka kuwa msaliti asiye hata na neno moja la kujitetea kwa zaidi ya wiki tatu sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…