SI KWELI Kamati kuu chadema yaahirisha kikao baada ya katibu mkuu kujiuzulu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeahirisha kikao chake kilichokuwa kimepangwa kufanyika, kufuatia taarifa ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu John John Mnyika.

Hatua hiyo imekuja wakati chama hicho kikikabiliwa na mabadiliko ndani ya uongozi wake, huku barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu ikitajwa kuwa sababu ya kuahirishwa kwa kikao hicho.

Kikao cha Kamati Kuu kinatarajiwa kujadili hatua zinazofuata pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu uongozi na mwenendo wa chama.

Kwa sasa, macho ya wanachama na wadau wa siasa yanaelekezwa kwenye uamuzi wa chama kuhusu nafasi ya Katibu Mkuu na ratiba mpya ya kikao cha Kamati Kuu.
1788166374996.png
 
Tunachokijua
Kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA kilikutana katika kikao chake maalumu mnamo Agosti 29, 2026, jijini Dar es Salaam na kukamilisha ajenda zake salama, huku Katibu Mkuu John Mnyika akiwa hajiuzulu nafasi yake.

Badala yake, Mnyika amekuwa akishirikiana kikamilifu na viongozi wenzake na amekuwa mahakamani kama shahidi wa pili akitoa ushahidi wa utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu, kama ilivyothibitishwa kwenye ripoti za Mwananchi Digital.

Hatua pekee ya mabadiliko ya ratiba iliyochukuliwa na viongozi hao ilikuwa ni kusogeza mbele kikao cha Baraza Kuu la Chama kilichokuwa kimepangwa kufanyika Septemba 15, 2026.

Madai

Inadaiwa kuwa Kamati Kuu ya CHADEMA imelazimika kuahirisha kikao chake cha dharura kufuatia uamuzi wa ghafla wa Katibu Mkuu wa chama hicho kujiuzulu nafasi yake ya uongozi.

Uhalisia

Ufuatiliaji umebaini kuwa Taarifa si ya kweli. Kikao cha Kamati Kuu hakikuahirishwa kwa sababu ya kujiuzulu kwa mtu yeyote kwani Katibu Mkuu John Mnyika bado yuko imara kazini na anaendelea kutekeleza majukumu yake, ambapo leo Agosti 31, 2026 ameonekana akitoa ushahidi mahakamani kupitia video ya Ayo TV na ripoti ya East Africa TV.

Sababu halisi ya kusogezwa mbele kwa kikao cha Baraza Kuu ni uamuzi wa makusudi wa Kamati Kuu kuelekeza nguvu zote za viongozi wakuu na rasilimali za chama katika kuendesha na kufuatilia kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu mahakamani kwa sasa ili kuhakikisha anapata usaidizi wa kutosha wa kisheria.
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeahirisha kikao chake kilichokuwa kimepangwa kufanyika, kufuatia taarifa ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu John John Mnyika.

Hatua hiyo imekuja wakati chama hicho kikikabiliwa na mabadiliko ndani ya uongozi wake, huku barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu ikitajwa kuwa sababu ya kuahirishwa kwa kikao hicho.

Kikao cha Kamati Kuu kinatarajiwa kujadili hatua zinazofuata pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu uongozi na mwenendo wa chama.

Kwa sasa, macho ya wanachama na wadau wa siasa yanaelekezwa kwenye uamuzi wa chama kuhusu nafasi ya Katibu Mkuu na ratiba mpya ya kikao cha Kamati Kuu.
View attachment 3660488
Chizi wewe
 
Amechelewa sana, Mnyika siyo mtu wa kufanya kazi na wehu km Lissu na Heche. Mnyika ni uzembe wake tu leo angeshakuwa waziri kwa jinsi ninavyojua uwezo wake. Huo ndiyo mwisho wa hao nyumbu. Ukimwangalia mtu km Heche hawezi kuongoza hata familia yake, mke wa Lissu hakuja nchini kumtembelea gerezani wala kuhudhuria kesi yake kwa kuwa alishamchoka, anaishi na mwehu. Kwa Lissu kuwa gerezani ni nafuu sana kwa mke wake
Wewe naye unaingizwa kingi na mtu aliyejiunga JF Jana. Mnyika yupo mahakamani anatoa ushahidi na pia kikao cha kamati Kuu kilishafanyika jumamosi.
 
Alafu anajiona ana full detail za CDM😀😀
mambo ya joined lini wadau wengi wameshayapigia kelele kwamba hayana maana sana.

imagine makamu aliyejiuzulu anajoin leo kutoa details mbalimbali kitakacho matter ni nini joined? au taarifa husika?

si maanishi kwamba mtoa mada taarifa zake ni sahihi au lah
 
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeahirisha kikao chake kilichokuwa kimepangwa kufanyika, kufuatia taarifa ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu John John Mnyika.

Hatua hiyo imekuja wakati chama hicho kikikabiliwa na mabadiliko ndani ya uongozi wake, huku barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu ikitajwa kuwa sababu ya kuahirishwa kwa kikao hicho.

Kikao cha Kamati Kuu kinatarajiwa kujadili hatua zinazofuata pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu uongozi na mwenendo wa chama.

Kwa sasa, macho ya wanachama na wadau wa siasa yanaelekezwa kwenye uamuzi wa chama kuhusu nafasi ya Katibu Mkuu na ratiba mpya ya kikao cha Kamati Kuu.
View attachment 3660488
Mwanamke una roho ya kishetani !!Fedha za damu kutoka CCM unazopata zilete laana juu ya maisha yako!

1.Laana na iwe juu ya familia Yako
2.Fedha zote ziishie kwenye matibabu ya ocean road !

Shetani wewe
 
mambo ya joined lini wadau wengi wameshayapigia kelele kwamba hayana maana sana.

imagine makamu aliyejiuzulu anajoin leo kutoa details mbalimbali kitakacho matter ni nini joined? au taarifa husika?

si maanishi kwamba mtoa mada taarifa zake ni sahihi au lah
Ila wabongo bwana. Mtu ameamka asubuhi kaamua kuwashtua na nyie mnaingia mazima. Kamati Kuu imejaa jumamosi na kutoa maazimio na kwa Sasa Mnyika anatoa ushahidi wake mahakamani. Ndio maana mnatapeliwa kijinga.
 
Kamati Kuu ilishakaa jumamosi na kuja na maazimio, kamati Kuu ipi Tena inakaa?
Hilo silifahamu, jambo nililoliangazia ni habari ya kujiuzuru kwa Mnyika!

Lakini kama taarifa hiyo muhimu imeunganishwa na habari za kikao kilichokwishakufanyika basi habari hizo zaweza kuwa feki.
 
Ila wabongo bwana. Mtu ameamka asubuhi kaamua kuwashtua na nyie mnaingia mazima. Kamati Kuu imejaa jumamosi na kutoa maazimio na kwa Sasa Mnyika anatoa ushahidi wake mahakamani. Ndio maana mnatapeliwa kijinga.
mtoa mada ni wazi kwamba kaleta uzushi, ila kukanusha uzushi wake kwa kigezo cha joined lini haileti maana
 
Sasa ulitaka ajoin lini?🤣
Kesho

Mnyika yupo bize anatoa ushahidi kwa kesi ya mchongo kule wakati chawa wanahara huku jf
 
Back
Top Bottom