Kamati Kuu ya CHADEMA haina meno. Mbona Tundu Lissu alijiamulia tu kumuunga mkono Maalim Seif na haikumfanya chochote?

Kamati Kuu ya CHADEMA haina meno. Mbona Tundu Lissu alijiamulia tu kumuunga mkono Maalim Seif na haikumfanya chochote?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kamati kuu ya CHADEMA na Tundu Lissu akiwemo iliteua jina la mgombea Urais wa Zanzibar na baadaye likapitishwa na Kikao cha Baraza Kuu Tundu Lissu akiwemo pia.

Wakati wa kampeni Tundu Lissu akabadili gia angani na kulitangazia taifa kuwa yeye anamuunga mkono mgombea urais kupitia ACT Wazalendo na kuwataka wafuasi wake kumpigia kura Maalim Seif na Zitto Kabwe kwa nafasi ya Ubunge Kigoma Mjini.

Mbona kamati kuu ya CHADEMA haikumuhoji Tundu Lissu wala kumchukulia hatua yoyote kama ilivyofanya kwa wale wabunge 19?

Ama ni mfumo dume umetamalaki au kamati kuu haina meno.

Maendeleo hayana vyama!
 
hakujiamulia ulikua ni msimamo wa chama.

Comrade una swali lingine?
Uongo

Mgombea uraisi wa Chadema ZANZIBAR alipitishwa na kamati kuu ya CHADEMA na mkutano mkuu wa CHADEMA

Lisu akajibwatukia tu kuwa anamuunga mkono maalim seif bila kikao cha kamati kuu wala mkutano mkuu wowote!

Chadema mnadai katiba mpya wakati hata hiyo ya kwenu yenyewe hamuwezi kuisimamia!!! mkamwacha solemba mgombea uraisi wenu wa Zanzibar hewani

Vivyo hivyo kwa ACT wazalendo walitangaza kumuunga mkono Tundu LISU na kumtelekeza mgombea wao Membe ambaye aliteuliwa na kamati kuu na mkutano mkuu.iLIPOFIKA KUMTELEKEZA HAKUNA KIKAO CHA KAMATI KUU WALA MKUTANO MKUU kilikaa !!!

Upinzani Tanzania ni hopeless kabisa.Hawajali katiba zao halafu utasikia ohhhh tunataka katiba mpya!!!

Laana ya yule mgombea uraisi wa CHADEMA Zanzibar na Ya MEMBE ndiyo ilimfanya Lisu ashindwe uraisi
 
Swali halina misingi ya kisheria. Una swali lingine?
 
Swali halina misingi ya kisheria. Una swali lingine?
Lina msingi wa kisheria Lisu alivunja katiba ya CHADEMA kujitamkia kuwa anaunga mkono mgombea urais wa chama kingine bila kupata ridhaa ya kamati kuu na mkutano mkuu wa CHADEMA
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema baada ya Kamati kuu kukaa kikao,kimeona ni sahihi kwa chama hicho kumuunga mkono Mgombea Urais kupitia Act Wazalendo kwa upande wa Zanzibar Maalim Seif Sharif.

''Sisi kama Kamati kuu tumeridhika na kauli mbalimbali zilitolewa na viongozi wa vyama vyetu hususani CHADEMA na ACT-Wazalendo na baada ya kushauriana na mgombea wetu wa zanzibar Mhe.Said Issa Mohammed tumeona ni sahihi kwa Chama chetu kumuunga mkono Seif Sharif Hamad''amesema Freeman Mbowe

Source: EATV:

Una jingine?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Source: EATV:

Una lingine?
Ni mkutano mkuu ndio ulitakiwa uamue mgombea urais Zanzibar kupitia CHADEMA ajitoe sababu ndio waliomchagua na kumwidhinisha kamati kuu ilipeleka pendekezo tu la majina .

Mkutano mkuu ndio ulitakiwa kutoa tamko sio kamati kuu.
 
Ni mkutano mkuu ndio ulitakiwa uamue mgombea uraisi Zanzibar kupitia CHadema AJITOE SABABU NDIO ULIOMCHAGUA na kumwidhinisha kamatti kuu ilipeleka pendekezo tu la majina .

Mkutano mkuu ndio ulitakiwa kutoa tamko sio kamati kuu
Unaweza kuweka kifungu cha katiba ya CHADEMA kinachosema ni Mkutano Mkuu ndio ulitakiwa kuamua kufanya hivyo?
 
Unaweza kuweka kifungu cha katiba ya CHADEMA kinachosema ni Mkutano Mkuu ndio ulitakiwa kuamia kufanya hivyo?!
Mkutano mkuu ndio huteua mgombea uraisi hivyo ni automatic ndio wenye uwezo wa kutengua ugombea sio LISU na mdomo wake
 
Back
Top Bottom