Uchaguzi 2020 Kamati kuu ya CHADEMA, tunaomba mtuletee maazimio yafuatayo

Dalili zote zinaonyesha movement ya Lissu ni zaidi ya Kimbunga kumbakumba, huwezi kukizuia kwa mwavuli
Umetoa pondekezo zuri mkuu. Hata mimi nadhani Lissu na Chadema waitumie ''adhabu'' hii ya kishetani kuwafanya NEC-CCM wajute kumfungia. Zitafutwe mbinu za kumfanya ku-engage na wananchi na kijitangaza kulika hata angepiga kampeni.
 
Wakati gani Mkuu kwa hivi vimkwara vya lissu jukwaani [emoji3][emoji3]
Lb7 Kwamba Lissu yu hai nyongo zenu milini ni kutenda sumu tu.

Mna wakati mgumu kuliko maelezo.
 
Wakati gani Mkuu kwa hivi vimkwara vya lissu jukwaani [emoji3][emoji3]

Hamuwezi kuwa wakati mwepesi. Inawezekana je kutusemea na wengine hali hatujakutuma kama si kuweweseka vilivyo?

 
Nashauri TL na kamati yake watumie muda huu wa kusimamishwa kwa kampeni zao kuandaa mikakati ya kupata mawakala wasomi, wenye nguvu, waaminifu,na wahakikishe kila kituo kinakuwa na mawakala zaidi ya mmoja kwa kutumia uwakilishi wa vyama rafiki hasa ACT wazalendo.

Kumbuka kivumbi, patashika nguo kuchanika, figisu, vitimbwi, mazingaombwe, vituko na kila aina ya mihemko, kura kupotea, mabox kunyakuliwa, mawakala kushambuliwa na kunyimwa nakala za matokeo, kunyimwa fomu za malalamiko, kukataa kusaini matokeo, kubadili matokeo kwa maana ya kura za A kumpa B na za B kumpa A, yote hayo muda wake ni kuanzia saa1 jioni ya tarehe 28/10/2020.

Uzoefu wangu unanionyesha kuwa hicho ndio kitakachokuwa kipindi kigumu na cha kutisha sana huenda kuliko nyakati nyingine zote katika historia ya uchaguzi wa nchi hii.

Ndio kipindi pekee cha kuhakikisha chungwa linabaki kuwa chungwa, au kwa nguvu ya ajabu, chungwa litabadilishwa kuwa limau.

Ndio kipindi cha kuamua hatima ya amani ya nchi hii.
 
Mkuu umewaza vema, hapo wanapima upepo
 

Heshima kwako mleta mada.

Bila kukomaa na kukataa yasiyo haki kufuata sheria na kanuni zao ni kuelekezwa rasmi machinjoni.

Kukubali liwalo na jiwe ni option ya maana pia.

Yalikuwa maamuzi bora kabisa - kuunganisha nguvu zote na kukataa rasmi katazo lao. Ikiendana rasmi na kutangaza rasmi mashirikiano na vyama vingine.

Muda mzuri wa ku declare mbwai!

Mamboleo na hata wale wa kisutu walitambua mbwai hiyo wakachomoa betri!

Nguvu yetu inatosha sana kuendelea na kampeni dhidi vya makatazo uchwara kama haya.
 
Polisi ipo kulinda sheria, sisi Watanzania tutabaki nyumbani kutii sheria hatuwezi kwenda kumskililiza muhubiri chuki
Muhubiri chuki ni yule aliyesema Tunduma wasipomchagua Silinde hawezi kuwapelekea Maji
 
Badala ya kuhimiza atulie na kuomba msamaha wewe unahimiza aendelee kufanya ujuaji na kiburi....wahenga walishasema mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi

Aombe msamaha kwa kosa gani? Au unataka kumvalisha Lisu lile pepo la nidhamu za woga la kina Nape, Makamba, Kinana nk? Lisu hana nidhamu ya woga wala unafiki, na akitaka tumdharau, basi afuate huu upuuzi wako ulioshauri hapa.
 
Safi sana uko vizuri
 
Napendekeza kwankipindi hiki avuruge jiji la Dar es salaam kuwapigia debe wabunge wa jiji Hilo.
 
Umeona mbali na mawazo yako yanafungamana na yangu. Aendelee kuchanja mbuga tu.
 
Kama vile ulikuwa kwenye akili yangu, kampeni sawa Ila Kuna mambo nje ya kampeni Ni muhimu zaidi,

Niliona mh Membe kwenye interview pale airport akionya juu ya Jambo hili

Kuna Haja ya kupanga team ya mawakala waaminifu, wasio na njaa na wenye misimamo nchi nzima,

Kuna Haja ya kuwawekea ulinzi wagombea ambao watashinda lakini watatafutwa ili wahongwe na kukubali kushindwa,

Kunahitajika watu ambao siyo lazima wagombea watakao hamasisha watu kuingia barabarani haki ikionenaka kutokutendeka
 
Ccm wamepanga kuapishwa mawakala feki ili wawahi vituoni kuchakachua kabla mawakala original hawajafika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…