Uchaguzi 2020 Kamati kuu ya CHADEMA, tunaomba mtuletee maazimio yafuatayo

Badala ya kuhimiza atulie na kuomba msamaha wewe unahimiza aendelee kufanya ujuaji na kiburi....wahenga walishasema mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi
We pimbi, aombe msamaha kwa lipi?
 
Mimi kama mwananchi wa kawaida namshauri mheshimiwa mgombea angetumia muda huu kutengeneza video zinazolenga kuongea na ma group mbalimbali.

1. Kwa mfano video ya kwanza kuongea na watumishi wa umma kuwaelezea kwanini wamchague.

2. Kuongea na vijana na kuwapa sababu za kumchagua.

3. Kuongea na kina mama kuwanadia sera zake na kuwapa sababu.

4. Kuongea na walimu nk

5. Kuongea na wanafunzi wa vyuo vya elimu za juu nk

Yaani siku 7 zikiisha anatakiwa kila siku 2 au 3 anarusha video moja mtandaoni ambayo sio ndefu ila ilaelezea sera zake kwa makundi mbalimbali. Na huku anaanza tena kampeni nadhani itamuongezea mileage. Na kinaweza kuwa kimbunga kikubwa ambacho kinatapakaa kwa whatssap na social media zingine kwa muda mfupi. Ningekuwa mimi ndio meneja wa kempeni zake ningefanya hivyo.
 

Hii ni good idea, lakini je akifanya hivyo hawatamhesabia kuwa kafanya kampeni?
 
Nakuelewa sana ndugu.
 
Bonge la idea mkuu. I wish wazo hili lingechukuliwa.
 
Nimeipenda ile namba 4. Mh Mbowe achukue nafasi ya Lissu kwa hizo siku 7, kwa ratiba ile ile ya tume Mbowe apite. Ninafahamu kuwa Mh Mbowe ana uwezo mkubwa sana wa kuwakilisha hoja na wananchi watamuelewa. Na baada ya hapo Lissu aendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…