Nimepata taarifa za kuhuzunisha kupitia vyombo mbali mbali vya habari eti wabunge wateule wa raisi na wale tuliowachagua watuwakilishe kwenye bunge la katiba wamegeuza pale bungeni kuwa mahali pa kudai returns.... divindeds,miposho kama kiinua mgongo..... watu tunaumiza vichwa ni namna gani katiba mpya itakavyo tuathiri sisi na vizazi vyetu miaka nenda miaka rudi... siku ya kwanza wanaenda kudai posho..... what a bunch of useless representatives?
Eti maisha ya Dodoma magumu, ni wapi maisha ni rahisi?hapo dodoma mwalimu analipwa bei gani?
Mh. Raisi uliwaokoteza wapi hawa wahuni wanaodhani Bunge la katiba ni sehemu ya kwenda kutanua?
Ingekuwa busara Raisi Kikwete akalivunja hili genge la wabinafsi na wenye uchu wa hela za bure tukaanze upya....
mlijua hapo ni mahali pa kwenda kutafuta hela za kujenga nyumba? kazi ziko nyingi! si mkalime?
OMBI MAALUMU KWA MH. MBOWE.
Move yeyote itakayopelekea posho kuongezwa hata kwa senti moja... utakuwa umearibu image ya chama ambacho wewe ni mwenyekiti wake..., Chama kilichojitoa kwa hali na mali kumtetea mtanazia kwa hali zote na kwa haki....!embu fikiria 300,000*20*3=18,000,000 huo ni mshahara wa mwalimu wa digrii kwa takribani miaka 4.....!
Mh. Mbowe umepewa mtego wa kifo..... akili za kuambiwa changanya na zako.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.