Zikiwa zimesalia takribani siku nne tu kuelekea siku ya kupiga kwa ajili ya kumpata kiranja Mkuu wa taifa letu pamoja na wawakilishi wetu katika mjengo wa kutunga sheria, kuna viashiria kadhaa vinavyojionesha kutaka kupoka amani na utulivu ambao watanzania tumekuwa nao kwa miaka mingi sana.
Sasa naomba nitoe rai kwa kikundi chetu kinachojulikana kama "Kamati ya kusimamia amani hapa nchini, kisimamie misingi ya kuundwa kwake na kumkea kila anayekwenda kinyume na misimgi ya uwepo wa kamati hiyo bila kupepesa macho wala kumfumbia macho yeyote yule!
Kwani kinyume na hapo, hayo majoho yenu yasije kuwa chukizo mbele za macho ya Mungu, Watanzania na hata ulimwengu mzima.
Mimi nimetimiza wajibu wangu!
Mungu atusimamie, tuvuke salama!