Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeeleza kuwa kuna shule kadhaa zinazofundisha masomo ya sayansi bila kuwa na maabara, hali inayotia wasiwasi hasa ikizingatiwa kuwa baadhi ya wanafunzi hao wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya mwisho mwezi Mei 2025.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Justin Nyamoga, alibainisha hali hiyo alipokuwa akiwasilisha maoni ya Kamati kuhusu bajeti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Kwa mujibu wa Nyamoga, mafanikio katika ufundishaji wa masomo ya sayansi yanahitaji kuwepo kwa maabara zilizowekwa vifaa muhimu vya kufundishia. Hata hivyo, katika ukaguzi wa miradi ya shule mbalimbali za sekondari, Kamati imegundua kuwa baadhi ya shule hazina vifaa hivyo kabisa.
Ripoti ya Kamati inaonyesha kuwa shule nyingi tayari zimepokea wanafunzi wa masomo ya sayansi, ingawa miundombinu ya maabara haipo. Hali hii inahatarisha uwezo wa wanafunzi kufanya mazoezi ya vitendo kabla ya mitihani yao ya kitaifa.
“Kama Serikali haitachukua hatua za haraka, wanafunzi hawa wanaweza kujikuta wakifanya mitihani ya vitendo bila maandalizi stahiki kwa sababu ya ukosefu wa maabara,” alisema Nyamoga.
Kutokana na changamoto hiyo, Kamati imependekeza Serikali iandae mpango wa dharura wa kusambaza vifaa vya maabara katika shule zote 26 za wasichana za mikoa, bila kuathiri mipango iliyopo ya kusambaza vifaa hivyo kwenye shule nyingine za sekondari.
Aidha, Kamati imeshauri Serikali kutenga bajeti maalumu ya kudumu kutoka kwenye chanzo mahsusi, ili kuhakikisha vifaa vya maabara vinapatikana kila vinapohitajika katika shule zote za sekondari nchini.