Kamati ya Bunge Maalum la Katiba hatimae imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000!

Kamati ya Bunge Maalum la Katiba hatimae imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000!

Kupinga 500,000/- ni jambo jema, pia kupinga 300,000/- ni jambo jema vilevile, ila wakati wajumbe wa bara wanapokea 300,000/- kwa siku wale wa Znz wanapokea 420,000/- huu utata ndio uliopelekea wajumbe wa bara kudai posho iongezwe na iwe sawa kwa wajumbe wote bara na Znz.

Wenyewe wana mahesabu yao (kikokotoo) ila hawajapenda kuweka hadharani ili ku-justify ongezeko la posho, hivyo kufanya umma uje juu!
 
Wewe Zitto kama Yesu kabsaaaa!!!!,kama alivyo kufa msalabani,nawewe sasa upo msalabani kwa kuwakomboa WATANZANIA.
 
Mfanyakazi wa serikali kwa mwezi mshahara 360000: mjumbe wa katiba kwa siku 500000. Kweli haya ni majanga! Mjumbe anayependa posho iongezwe aondoke mara moja dodoma!
 
jaman yani kuna watu hawajui maana ya mitandao ya kijamii
.
.yani kwa kuwa ww unatumia FB kuchat na wajinga wenzio hujui kuwa huo mtandao ni njia moja ya msingi sana katika kufanikisha mawasiliano....ndo mana unaitwa mtandao wa kijamii.....maana yake njia ya kuwasiliana kwa wanajamii....zzk hata kama ni mnafiki anapofanya vzr ni haki tuseme na kutumia fb kama njia ys mawasiliano siyo kosa ni njia nzuri kwani inawafikia watu wengi zaidi.
mapambano ni ya posho katiba ni njia tu ya kuifikia posho.


MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hawa wanasiasa wetu bwana kwa kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii...sasa kama ni msimamo wake, si asubiri kesho ndiyo aweke hiyo saini?

Acha FITNA. Yeye ni mbunge, yaaani mwakilishi wa wananchi. Kwa kuandika maneno hayo:
1. Katoa mrejesho wa kinachojiri katika CA kuhusianana sakata la Posho kwa wananchi anaowawakilisha na umma wa watanzania wote ili wafahamu. Na zaidi, wakishafahamu
2. Washirikiane kumshinikiza raisi asiidhinishe posho hiyo ya laki 5 kwa siku.
SIMPLE!! Hajajipendekeza, ni wajibu wake. Truth be told.
 
Baada ya wabunge kutaka ongezeko la posho kutoka 300,000 hadi 500,000/= kwa siku. Serikali imewaonea huruma watumishi wake ambao nao husafiri kwenda Dodoma na kulipwa posho ya malazi ya chini kabisa huwafanya kuishi maisha ya kubangaiza kwa kulala Guest za vichochoroni. Kutokana na Wabunge kuutangazia umma kuwa posho ya laki 3 haitoshelezi kwa siku kwa waheshimiwa Serikali pia imeamua kubalisha waraka wake wa posho ambao utaanza kutumika Machi 2014. Ambapo Mtumishi aliyekuwa akipata posho ya 45,000/= mfano Dereva na Mhudumu wa Ofisi sasa atakuwa anapata 80,000/= na wale Maafisa waliokuwa wanapata 65,000 na 80,000 watakuwa wanapata posho ya Tsh 120,000/= kwa siku hii ni kuwafanya waweze kumudu gharama za maisha wanapokuwa wamesafiri kikazi.

Source of this information please.
 
Gesti za vichochoroni wanataka nani akalale kama hawataki wafanyakazi walale uko,
 
Kumekucha!!!

BUNGE la KATIBA ZITTO KABWE na JULIUS MTATIRO waungana KUPINGA ongezeko la POSHO.

HAYA NI MANENO YA MZALENDO ZITTO LEO:-

"Posho Bunge Maalumu la Katiba kuwa 500,000 kwa siku.

Habari zilizoandikwa na gazeti la mtanzania la Leo kwamba Kamati ya kufuatilia posho za wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000 kwa siku imethibitishwa ni kweli.

Natoa wito kwa Wananchi wote kushinikiza kwa Rais pendekezo hili asilikubali. Naunga mkono wazo la mjumbe wa Bunge Maalum ndg Julius S. Mtatiro la kuorodhesha majina ya wote wanaopinga nyongeza ya posho. Nitaweka sahihi kwenye petition yake hiyo mapema kesho asubuhi.

Wagombea uenyekiti nao wanaahidi kupandisha posho. Nawaonya wasithubutu kutoa ahadi hiyo kwani sio mamlaka yao. Mgombea mwenye sera ya posho hatapata kura yangu na nitashawishi wajumbe wengine wasimpe kura".
‪#‎NatakaKatibaSitakiPosho‬
 
Wewe Zitto kama Yesu kabsaaaa!!!!,kama alivyo kufa msalabani,nawewe sasa upo msalabani kwa kuwakomboa WATANZANIA.

zito ni shujaa wa taifa, uzalendo wake kwa taifa ni zaidi ya nyerere
 
Hawana sumu wenyewe posho ndio imewapeleka.Sijawahi kuona au kusikia duniani msaliti akitetea wanyonge😛hoto:
 
zito ni shujaa wa taifa, uzalendo wake kwa taifa ni zaidi ya nyerere.
 
Wacha wale hiyo pesa, they deserve. hahahaa
 
sijui tutahitaji viongozi wa aina gani,labda tungekuwa na viongozi aina yadialo au lowasa au ndesapesa/ mbunge wa moshi mjini na wajumbe wengine wa aina hii sijui kama wangelilia posho.sina hakika.
 
Kuomba waongezewe posho maana yake wanajua pesa ipo. Serikali inapesa tena ya kutosha ndio maana wakaomba, kama isingekuwepo wasinge omba. Ya kulipa walimu na wafanya kazi wengine madai yao haipo, ya kuajiri walimu wapya haipo! Mimi nadhani machafuko kwenye nchi hii hayako mbali, viongozi wamezidisha dharau kwa wananchi.
 
Njaa mbaya, hawa wanadamu wakishategeshewa microphone na spika wanabadilika sana akili. Hurukwa akili kbs
 
Back
Top Bottom