Pre GE2025 Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii yaridhishwa na ujenzi wa mradi wa maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) uliofikia asilimia 99

Pre GE2025 Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii yaridhishwa na ujenzi wa mradi wa maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) uliofikia asilimia 99

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeridhishwa na ujenzi wa mradi wa maktaba ya Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) ambao umefikia asilimia 99 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari 2025.

Akizungumza wakati wa majumuisho mara baada ya ziara ya kukagua ujenzi wa maktaba hiyo mjini Tabora, Mwanyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Timotheo Mzava alisema kamati yake imejionea na kuridhishwa kwa hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa maktaba hiyo pamoja na maendeleo ya chuo hicho.

Soma pia: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Kwa ujumla Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii baada kupitia, kukagua, kupata taarifa na kujionea kwa macho, imeridhishwa na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na uongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja Chuo cha Ardhi Tabora katika kukamilisha jengo hili la maktaba” alisema

Naye, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda aliishukuru kamati hiyo ambayo ndiyo yenye dhana ya kuisimamia, kushauri, kutoa maelekezo mbalimbali na kufuatilia kazi zinazotekelezwa na wizara hiyo.

 
Wamejipiga picha wenyewe badala ya kupiga picha Maktaba
 
Back
Top Bottom