Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Jackson Kiswaga (Mb) imebainisha hayo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wa mkakati wa Bwawa la Kidunda.
Mheshimiwa Kiswaga amesema Kamati ya Bunge Maji na Mazingira itahakikisha inaishauri Serikali vizuri ili fedha za utekelezaji wa mradi huu zisikwame na mradi ukamilike kwa wakati na manufaa yake yaonekane.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Ndugu Rose Ambrose amesema Wizara ya Maji itaendelea kusimamia vyema utekelezaji wa mradi huu na kuhakikisha inatatua vikwazo vyote ili mradi ukamilike kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire amesema mradi wa Bwawa la Kidunda umefikia asilimia 47 ya utekelezaji wake huku mategemeo yakiwa kukamilisha mradi ifikapo Disemba 2026.
Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda utahusisha Bwawa lenye uwezo wa kuhifadhi maji Lita bilioni 19 0, uzalishaji umeme megawati 20, ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe kilomita 75 toka Ngerengere hadi Kijiji Cha Kidunda.