Kamati ya Bunge ya Miundombinu yataka kuwepo kwa haki ya kusahaulika

Kamati ya Bunge ya Miundombinu yataka kuwepo kwa haki ya kusahaulika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Akiwasilisha mapendekezo Juu ya Muswada wa Ulinzi wa Taarifa Binafsi, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso amesema baada ya kufanya mapitia ya muswada huo na kusikiliza maoni ya wadau mbalimbali wakiwemo JamiiForums amesema ni muhimu kwa sehria hiyo kutambua haki ya kusahaulika.

Haki ya wahusika wa taarifa izingatiwe (data subjects) walioachana na taarifa zilizokusanywa kuendelea kuhusishwa na taarifa hizo tofauti na utashi wao izingatiwe katika utekelezaji wa sheria inayopendekezwa. Aidha stahili ya marehemu kuhusu ulinzi wa taarifa zao iwekwe na utaratibu uzingatiwe.

Akitoa mapendekezo yake amesema, ni muhimu sheria kuweka uhuru wa mtu kuweka ukomo wa matumizi ya taarifa zake ili ziendelee kutumika ikiwa hataki ziendelee kutumika hivyo. Pia ametaka kuwepo muswada uainishe haki za marehemu ambao taarifa zao huendelea kutumika visivyo.

Haki ya kusahaulika ni moja kati ya haki muhimu, ikiwa mtu hataki kujulikana tena kama mtu wa namna fulani. Mfano mtu aliyekuwa mwanachama wa chama A, amebadili chama. Inabidi asahaulike na chama A ili kuepuka kuwa na idadi za uongo au idadi hewa.
 
Back
Top Bottom