Kamati ya Bunge yatoa sababu ya kucheleweshwa kwa mradi wa Dege ECo Village wa Kigamboni

Kamati ya Bunge yatoa sababu ya kucheleweshwa kwa mradi wa Dege ECo Village wa Kigamboni

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Godius Kahyayara amesema mradi huo umeshatekelezwa katika awamu mbili

Dar es salaam. Mvutano wa hisa kati ya Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Azimio, umeelezwa kuwa chanzo cha kuchelewa kwa mradi wa nyumba zaidi 7,000 zilizopo eneo la Dege Beach Kigamboni jijini Dar es salaam.

Hayo yalibainika leo Januari 20, 2018 katika ziara iliyofanywa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) katika eneo la mradi.

Awali Mkurugenzi mkuu wa NSSF, Godius Kahyayara amesema mradi huo umeshatekelezwa katika awamu mbili ambapo nyumba 3,750 zimeshakamilika kati ya nyumba 7,160 za mradi mzima.

Amesema kwa mujibu wa mkataba huo, kampuni ya Azimio iliyotoa ardhi ya hekta 300 inamiliki hisa 55% huku NSSF iliyowekeza zaidi ya Dola 500 ikimiliki hisa asilimia 45.

Amesema mradi huo utakaogharimu dola za 544 za Marekani ulitarajiwa kukamilika mwisho wa mwaka huu lakini haitawezekana kutokana na dosari za mkataba.

Baadhi ya wajumbe wa PAC wamehoji sababu ya Mkurugenzi wa kampuni ya Azimio kutoonekana kila anapotafutwa.

Mbunge wa viti maalum (CCM), Shaly Raymond amesema kuchelewa kwa mradi huo kutapandisha gharama kutoka Dola 544 milioni hadi zaidi ya 700 na kuhoji nani atakayelipa.

"Angalia hiyo meza kuu, mwekezaji hayupo wewe Mkurugenzi umekuja peke yako, wenzako wako wapi?" alihoji Shaly.

Naye mbunge wa viti maalum (CCM), Felister Bura amesema kama Azimio hataki kuonyesha ushirikiano, atafutwe mwekezaji mwingine."Tulipozungumza na mwekezaji huyu alikubali kupunguza hisa zake kwa sababu amewekeza kidogo. Kama anasumbua NSSF waangalie namna ya kupata mwekezaji mwingine,” amesema.

Akijibu hoja za wabunge hao, Profesa Kahyarara amekiri i kucheleweshwa kwa mradi, kwamba bado wanajadiliana na kampuni ya Azimio.

Alimtetea mwekezaji huyo akisema amekuwa na safari nyingi nje ya nchi na kwamba atakuwepo kwenye kikao cha January 26 ambapo mambo yote yatajadiliwa na kutolewa uamuzi.
 
Blah blah blah yale magholofa yatachakaa kabla kuanza kutumika.. tumesitisha ujenzi halafu hatujui tufanyeje kuendelea na ujenzi!!.. its amazing!!
 
Amesema kwa mujibu wa mkataba huo, kampuni ya Azimio iliyotoa ardhi ya hekta 300 inamiliki hisa 55% huku NSSF iliyowekeza zaidi ya Dola 500 ikimiliki hisa asilimia 45.

Mbunge wa viti maalum (CCM), Shaly Raymond amesema kuchelewa kwa mradi huo kutapandisha gharama kutoka Dola 544 milioni hadi zaidi ya 700 na kuhoji nani atakayelipa.

Duuuu

Eti NSSF imetoa dola 500!

Nchi hii ina waandishi sijui walifeli darasa la nne?
 
Ameshindwa kutafsiri english version ya taarifa..

Hata huyo mwandishi mwinginine naye kaandika ovyo ovyo tu.

Anasema mradi ulichelewa kwa sababu ya dispute ya mgawanyo wa hisa. Halafu anasema NSSF wanamiliki 45%, Azimio 55%. Kwa hiyo huo ndio muafaka wa sasa au bado wamekwama na kwamba haieleweki mustakabali hapa ni nini?

Haya ndio mambo ya ovyo yaliyofanywa siku za nyuma ambayo Rais anayaongelea kila siku lakini cha ajabu amemzawadia ubalozi Ramadhani Dau, anachagua nani wa kum punish nani wa kumuonea aibu, hana principles.

Huu mradi sio umechelewa, umekwama!
 
Zikikosa wanunuzi wazipangishe tu hakuna hasara kwenye nyumba wala kwenye ardhi wacheni uoga ni masuala ya muda tu
 
Zikikosa wanunuzi wazipangishe tu hakuna hasara kwenye nyumba wala kwenye ardhi wacheni uoga ni masuala ya muda tu

Wazipangishe kina nani? Nani mwenye majengo?

Kuna mgogoro wa mkataba, utawala mpya umekuja ukakuta mambo ya hovyo yaliyofanywa na genge la Mkurugenzi Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi Abubakar Rajabu. Hawakuwa na chembe ya uzalendo, walijali familia zao na matumbo yao.

Mradi sio umechelewa, umekwama!

w6.jpg
 
Wanaruka na kukanyagana......

Ni muhimu kujali tonge langu,maana hamna anayesikia ati.....haya mengine namwachia UBONGO, moyo kashapewa majukumu ya msingi na Ditto alimsisitizia.
 
Mradi umesimama au hakuna hela za kuuendeleza Dr Dau na genge lake walisha piga zao % kadhaa wanakula upepo mwanana nje.....
 
Mradi umesimama au hakuna hela za kuuendeleza Dr Dau na genge lake walisha piga zao % kadhaa wanakula upepo mwanana nje.....

Genge la Ramadhani Dau walikuwa wana mazoea ya kupongezana kwa vyeti na ubwabwa na Bodi ya Wakurugenzi pamoja na machafu chafu yote ya NSSF

IMG_4490.JPG

IMG_4420.JPG

Mwenye tai na miwani kweye foleni ya ubwabwa ni mjumbe wa bodi Mussa Assadi ambae JK alimzawadia kuwa Mkaguzi Mkuu wa Serikali. Amekua akikataa kuji recuse kutoka kwenye kila ukaguzi wa NSSF na matokeo yake amekuwa akiwapa hati safi pamoja na madudu yote yaliyobainishwa na uongozi mpya. Alitakiwa aseme mimi nimefanya kazi NSSF siwezi kujikagua mwenyewe!
 
Huu mradi Mh. Rais wetu JPM ebu ingilia kati haraka.. Huu ufisadi mkubwa mno mno .. Aaaarrghhrrw
 
Wazipangishe kina nani? Nani mwenye majengo?

Kuna mgogoro wa mkataba, utawala mpya umekuja ukakuta mambo ya hovyo yaliyofanywa na genge la Mkurugenzi Ramadhani Dau na Mwenyekiti wa Bodi Abubakar Rajabu. Hawakuwa na chembe ya uzalendo, walijali familia zao na matumbo yao.

Mradi sio umechelewa, umekwama!

w6.jpg
Ndugu huo mradi jamn ni bonge la project hivi mpaka sasa hao wakubwa washamaliza hio sitofahamu na project linaendelea au ndo vipi tena nipatieni info kidogo kwa anayejua kwasababu hizi taarifa zimenisikitisha sana.
 
Mradi umesimama kabisaaa mpaka sasa na watu wameiba kila kitu hasaaa Nondo na vitu vingine vimeibiwa msa mrefu tu now hamna walinzi tena......
 
dah huo ni utapeli. hekari mia tatu zinakupa 55% na dola 544mln zinakupa 45%. Kwa hesabu maana yake hekari mia tatu zina thamani ya dola milioni 664. hii ni karibu Tsh trilioni 1.5!!!. yaani Hekari moja ni dola milioni 2.2 sawa na zaidi ya Tsh bilioni 5!!. kwa bei hiyo ekari moja wameuziwa Tsh bilioni 2. Huu ni ufisadi wa waziwazi. Kwani Hawa NSSF hawakuweza kupata viwanja vya kununua wenyewe? hata ukihamisha watu wenye nyumba zao huwezi lipa bilioni 2 kwa ekari.
 
Mradi umesimama kabisaaa mpaka sasa na watu wameiba kila kitu hasaaa Nondo na vitu vingine vimeibiwa msa mrefu tu now hamna walinzi tena......

Aisee!!.. kwa hiyo project haina mwenyewe sasa!!.. daah nyumba kali sana zile zinaharibika bure
 
dah huo ni utapeli. hekari mia tatu zinakupa 55% na dola 544mln zinakupa 45%. Kwa hesabu maana yake hekari mia tatu zina thamani ya dola milioni 664. hii ni karibu Tsh trilioni 1.5!!!. yaani Hekari moja ni dola milioni 2.2 sawa na zaidi ya Tsh bilioni 5!!. kwa bei hiyo ekari moja wameuziwa Tsh bilioni 2. Huu ni ufisadi wa waziwazi. Kwani Hawa NSSF hawakuweza kupata viwanja vya kununua wenyewe? hata ukihamisha watu wenye nyumba zao huwezi lipa bilioni 2 kwa ekari.
Na ugomvi ndio ulianzia hapa.
Hawa Azimio waliambiwa wazithaminishe upya heka zao wakagoma. Yaani Sqm1 kwa Tshs 1.22mil, duh

NSSF walijitetea kua eti unapoingia mkataba wa kuwekeza kwenye ardhi wa muda mrefu, lazima upige bei ya wakati ujao, sio ya sasa.
 
Aisee!!.. kwa hiyo project haina mwenyewe sasa!!.. daah nyumba kali sana zile zinaharibika bure

Mkuu nimesikitika sanaa maana nina eneo karibu na pale na target yangu ilikuwa kuweka nyumba za kupangaaa pale palikuwa hot cake sanaa sijui mambo yameishia wapi mpaka sasaa hata sielewi aiseeee....
 
Na ugomvi ndio ulianzia hapa.
Hawa Azimio waliambiwa wazithaminishe upya heka zao wakagoma. Yaani Sqm1 kwa Tshs 1.22mil, duh

NSSF walijitetea kua eti unapoingia mkataba wa kuwekeza kwenye ardhi wa muda mrefu, lazima upige bei ya wakati ujao, sio ya sasa.

Daaa inahuzunisha sanaaa aisewe ule mradi ulikuwa ndio kila kitu pale.....
 
Mkuu nimesikitika sanaa maana nina eneo karibu na pale na target yangu ilikuwa kuweka nyumba za kupangaaa pale palikuwa hot cake sanaa sijui mambo yameishia wapi mpaka sasaa hata sielewi aiseeee....

Pole sana mkuu na hivi tunahamia Dodoma, things will never be the same again!! Biashara gani itafanyika pale tena? Nani atapanga pale na nchi ishahama? Sad!
 
Back
Top Bottom