#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Alafu haya mambo ya tume za ujinga yalikua ya enzi za mkwere, kama ndo anaemshauri huyu mama tumekwisha!
 
Wenzetu mnaowaita mabeberu wameshachanja sasa wanaendelea na maisha kama kawaida.sie huku tunajifanya eti tunamjua Mwenyezi Mungu kuliko binadamu yoyote.Ni wapuuzi tu ndio watakaoingiza mambo ya sukuma gang kwenye hili suala.kwa taarifa mpigania uhuru/ubaguzi mkubwa Afrika ya Kusini tena kiongozi wa dini mashuhuri ARCHBISHOP DESMOND TUTU LEO AMEPATA CHANJO YA CORONA.
 
Kabla ya mapendekezo yao watuambie madhara ya muda mrefu ya kutumia hizo chanjo,ya muda mfupi tunajua watu wanakufa ,wengine kuganda damu.
japo hii kamati haijali watakaokufa na chanjo watajujua wenyewe.
 
I can't endorse that, the open truth hakuna chanjo ya korona ambayo imekuwa approved for general use. Hizo chanjo bado zipo kwenye hatua za mwanzo za majaribio, na makampuni wanachofanya ni kufanya janja janja kuwatumia watu kwenye majaribio bila ridhaa na bila fidia yoyote na bila ku-document methodology yoyote hasa sampling, sample size na findings kwenye kila hatua ya utafiti. Kama chanjo imetengenezwa na kuanza kutumika ndani ya mwaka mmoja, hiyo kamati inaweza kutupa long-term effects tuseme za miaka mitano au kumi za watu watakaokuwa wanachomwa hiyo dawa, wanayoita chanjo.....hili halitakiwi kufanyika hivyo na ufafanuzi kuhusu hizo chanjo ulishatolewa na mkurugenzi wa NIMR Dr. Mgaya kwamba bado hakuna conclusive data kuhusu hizo chanjo kuruhusiwa kutumika kwenye general population...
 
Hii chanjo iliyo chini ya mpango wa covax ni ile iliyopigiwa makelele kila kona na wakaamua kuibadilisha hata jina! Nchi nyingi zimeipiga marufuku, halafu mtu anasema chanjo hiyo ni salama (huku akijua kuwa tunafahamu siyo kweli - sijui amewezaje kuikandamiza dhamiri yake!). Wakati baadhi ya watu wamekufa kwa damu kuganda muda mfupi baada ya chanjo hiyo. Pili hizo chanjo zote hakuna ajuaye madhara yàke ya muda mrefu!! Ninaamini hata huko ulaya sehemu kubwa watakuwa wamechanjwa placebo (maji) na wachache ndo wametolewa mhanga wafanyiwe majaribio!!
Niwapongeze kamati kwa kusema hiyo chanjo itakuwa ya hiari, kama majaribio ya chanjo yanavyokuwa.
 
nyererere aliacha nchi ikiwa na maadui watatu ila adui ujinga bado hatujamshinda
 
Maajabu hayaishi duniani mkuu, utafiti wa wiki mbili umekuja na matokeo kwamba chanjo ya covid-19 ni salama na imeonyesha ufanisi, sisi yetu macho na masikio kadri Mwenyezi Mungu anavyotupa uhai....
 
Finaly we are here, wanaotaka chanjo wasinyimwe haki yao, na wasiotaka pia waheshimiwe, sijui mwendazake angekua macho angesemaje
 
Ujerumani kutoa CHANJO YA CORONA kwa wote kuanzia Julai 7,2021

Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema nchi yake itaanza kutoa chanjo za corona kwa kila mtu kuanzia Juni 7.

Germany drops COVID vaccination priority
 
Naona ripoti nene kweli kweli. Sijaona ripoti nene kama hii katika maisha yangu. Kweli SASH ataisoma yote hii?
Halafu wamefikiaje uamuzi wa kuwa chanjo ni salama? Nadhani wame google na kukusanya ripoti tu. Hakuna kitu maalum kilicofanyika Tanzania kilichothibitisha hilo. Ama sivyo watuambie methodology waliyoifuata. Hawa Maprofesa wa Bongo bwana!
Najua kuna shinikizo, na Tanzania pekee haiwezi kukataa, hasa ukiangalia kuwa wangeweza kuifungia watu wake wote wasisafiri.
 
Mimi namkubali sana billy gates na covax yake kupitia chanjo ya astra zeneca.
Jamaa ana uzoefu mkubwa wa kupambana na virusi toka mwaka 1995 alipoanza kupambana na virusi vya windows nikamkubali.
Hesabu rahisi
Kupitia covax mtapewa chanjo za bure 600,000.
Baada ya hapo mtanunua chanjo kwa ajili ya kuwachanja wananchi wenu chanjo tatu kwa kila mtu.
Kwa tz watu 60mill = chanjo 180 millioni
Chanjo moja 40usd-300usd (sababu gharama kubwa inakuja katika kusafirisha na kudistribute katika temperature inayitakiwa= 8trillioni approx ama zaidi ukitaka chanja wqnanchi wako wote.

Billy gates oyeeeed
Pesa oyeeee
Chanjo ni sawa tu na antivirus na billy anao ujuzi
 
Maajabu hayaishi duniani mkuu, utafiti wa wiki mbili umekuja na matokeo kwamba chanjo ya covid-19 ni salama na imeonyesha ufanisi, sisi yetu macho na masikio kadri Mwenyezi Mungu anavyotupa uhai....
Halafu ili kutudanganya wamecopy na kupaste mavolume ya vitabu sijui nani atayasoma hayo mavitabu, kwanza siamini kuwa kwa muda mfupi kiasi hiki wameweza kuandika mihutasari/ripoti na taarifa za kitibabu kwa hayo mavitabu na mwisho hakuna tafiti ya kitibabu inakuwa tayari kwa muda mfupi namna hiyo pia ripoti inatakiwa ituambie na madhara ya hizo chanjo, muda wa kutumia au kutokutumia, hayo yote hayajazungumziwa hadharani wakati yalitakiwa yaongelewe hadharani ili kutoa wasiwasi kwa wananchi,haitoshi tu kusema chanjo hii ni salama ,tusisahau hawa hawa watalaamu wetu ndio walisema GMO inatufaa, ni hawa hawa watalaamu wetu wameruhusu wakulima watumie dawa ya uuawa magugu ya Roundup itumike wakati huko huko Marekani inakotengenezwa imepigwa marufuku na hadi vibao vya matangazo vimewekwa jwenye highway zao kupiga marufuku dawa hiyo lakini huku kwetu hadi sasa imejaa maduka ya dawa na bado inatumiwa na wakulima . Mwendazake hakuwa mjinga alipokuwa na wasiwasi na hata aliposema mashine za kupima virusi vya corona vina matatizo wengi walimkebehi lakini mwisho wake ikawa aibu kwao baada ya kugundulika hizo mashine kuwa zina matatizo na nchi kadhaa kuacha kuzitumia.
 
Mkuu umeeleza vyema kunawatu wanataka kutufanya Kama viziwi yaan wao ndo wanasikia tuuuuuu... Anyway tunakwenda kuangamizwa bure kwa kutiwa hofu ili watu wafe kwa hofu... Sa iv wanafunzi wanasoma kwa aman kabisa, watu wanasafri bila kuogopana, wanasafrisha bidhaa na kuuza bila shida kabisa... Kunastarehe za kila aina na n.k

Sasa njoo uone kitakachotokea pind takwimu zikianza kutolewa yaan wagonjwa watazid mpka hospital zitalemewa na kunaweng tu hawataugua ila hofu itawauguza na wengi Zaid kufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…