BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,767
- 23,198
Maoni ya wananchi kwenye ushauri wa kitaalam?????
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
This was a rubbish kamati! Yaani mapendekezo ya kuvaa barakoa tulihitaji kamati? Hawakufanyakazi yao na yaonekana hawana uzoefu wa kuandika ripoti.View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud
----
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;
1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA
KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA
DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021
WA COVID-19 NCHINI
Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,
2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.
Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.
Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.
Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:
1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.
2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.
3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.
4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.
5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:
a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;
b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;
c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:
i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; nav. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.
e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.
6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.
7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.
8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.
9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.
10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.
11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.
12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.
13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.
14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.
15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.
16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.
17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.
18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.
19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.
Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
Zama za mwenda zakeNchi imeshkiliwa na vipuppet
Kwa kadiri ya uelewa wangu ni kuwa hakuna nchi iliyofanya chanjo iwe lazima. Kila sehemu wamesema ni hiari. Kuhusu kuvaa barakoa wanaweza kusema zivaliwe iwapo wave nyingine itakuja.Daah aisee ila mi kuvaa hayo mabarakoa sipendi kwakweli. Ni bora iwe hiyari na sio lazima. Wakiweka maisha yawe kama mwaka jana, hali itakua ngumu sana.
Mambo yawe hivi hivi, iyo chanjo nayo iwe hiyari ya mtu kuchanjwa.
WaoUkisoma ripoti nzima hakuna jipya na ni yale yale tunayoyasikia mataifa ya nje.Inaonekana hawakutumia ujuzi na akili zao wala kusikiliza maoni ya wananchi bali wamekopi na kubandika.
Hivi kamati haijasikia kwamba chanjo nyingi zina madhara na mataifa kadha wa kadha wanazirejesha kwao.
Na hawajasikia kuwa taifa lillochanjwa kwa zaidi ya asilimia 60 corona ndio kwanza inaongezeka.
Na kwamba sasa corona huko ilipo haichagui tena umri,mbona wao bado wanagwa makundi ya watoto na wazee.
Kaka ukiwa umevuta bangi jitahidi kuwa mbali na kifaa chako cha mawasiliano.Mwendazake alikuwa anatisha kwelikweli, halafu sijui akili zake alikuwa amepewa na nani maana hata mama janeth & jokate walikuwa hawamuelewi wao walikuwa ni kuvua na kutegesha basi mambo mengine walikuwa wanamuachia mwenyewe
Kiduchu tu na sio maktaba kubwaa ya nini...View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud
----
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;
1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA
KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA
DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021
WA COVID-19 NCHINI
Ndugu wanahabari, mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,
2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.
Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.
Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.
Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:
1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.
2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.
3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.
4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.
5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:
a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;
b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;
c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:
i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; nav. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.
e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.
6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.
7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.
8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.
9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.
10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.
11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.
12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.
13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.
14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.
15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.
16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.
17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.
18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.
19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.
Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
🤣 🤣 🤣Of course huna haja ya kusafiri. 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Mimi sitachanjwa hata iweje,waache wachanjwe wenyewe, kama ni kusafiri sio lazima nisafiri kila kitu kipo hapa hapa Bongo. Bongo ni paradiso nisafiri niende wapi na nikafanye nini?
Kwa hiyo unataka chanjo kama wazungu. Tatizo lako unakopi na kutuletea unayaona mitandaoni na kuyasikia kupitia king'amuzi. Unavyoona kwa miaka miwili na zaidi ya kuishi na COVID-19 hali ni ngumua kiasi cha kuhitaji na kukubali madhara hayo ya chanjo? Madhara ya chanjo baada ya miaka 3, 5, 10 n.k. umeshayaelewa? Ni kweli hutambui chanjo zote zimepitishwa kwa mpango dharula kuokoa wanavyoteketea? Je sisi tunateketea? Kenya waliteketea? Burundi Uganda, Rwanda, majirani ...... wanateketea.
Tumieni akili bhana!
Nimesoma mstari wako wa mwisho. Kwa hiyo haya yote yamefanyika na tuyafanye kwa sababu ya maingiliano na wengine? Uingilie wapi? China? Maisha yetu siku hizi ni attachment na china, FINITO! Hiyo ndo iwe sababu ya kujiandikia mavitabu kama haya na baadaye tuanze show za kuvaa barakoa?Kwa kuangalia hii picha, unaweza kuja na dhana Mbili za muhimu;
(1)Ukweli (Truth) (T)
na
(2) Uhalisia (Reality) (R)
Truth is Objective but
Reality is subjective.
Regardless of outcome, the Truth is determinant-- It has finality. It is what it is; unlike Reality which can be interpreted in different ways by the various people it affects".
Kwenye probability; occurrence of Event is always less or equal to 1:Ukweli +Uhalisia =? Dunia tunayoishi ni moja na muingiliano baina ya raia wa Nchi mbali mbali ni lazima
Kama ni hiari, nini sababu ya kulifanya ni jambo la kitaifa? Tutachezeshwa taarabu hadi lini?
Shule yako ni ya chini ya mti kama mwendazake.Uko lndia ambao ni watengenezaji wakubwa wa chanjo, unaona wamepotea wangapi kwa siku? Wewe ni njinga kama wajinga wengine haujui dunia inavyoenda.Ngoja takwimu kuhusu corona zianze kutoka,ili mfungiwe ndani kama kuku ndio utajua, maana Samia ndicho anachokitafuta
Unataka waje na mapya kutoka wapi mbinguni?kamati imekuja na yale yale ya nchi za nje kwa sababu ndio facts, hamna namna nyingune
Shule yako ni ya chini ya mti kama mwendazake Sibishani na wajinga