#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Mnapata taabu Sana kupotosha what is going on in this country at the moment. .the country is more divided now than ever ..mnapotosha kwa kudai kuwa kuwa Kuna genge or gang au to be specific the so called Sukuma gang...wote wenye Shaka na what is going on kwa Sasa mnawabatiza kuwa ni genge la Wasukuma...mmefanya dhambi kubwa mno kuingiza ukabila...itafika wakati hao Wasukuma mnaowadhalilisha wanaweza kujimobilize kwa kuona wanatengwa ndani ya nchi yao ...ni Jambo la hatari Sana kwa kweli...Kuna kabila lilinufaika na mfumo wa ukolonni na serikali zilizofuatia baada ya uhuru...wakapata elimu, wakajazana kwenye taasisi nyeti, TRA, mabenki, bandari, wizara ya fedha...wakapeana kandarasi na kadhalika...lakini hawajawahi kuitwa genge la kabila Fulani...haya tunayashuhudia Sasa dhidi ya wasukuma kwa kosa la kusingizuwa kwamba eti walifaidi enzi za JPM ...it is a dangerous move, a very dangerous move...eti wasukuma walifaidi!! ?! Ni hatari kwa kweli..Mimi siyo msukuma ila naiona hatari iliyopo..watu wengine wore wanaoonesha hofu kwa Sasa nao wanaitwa wasukuma...the so called Sukuma gang...
Ila mnashundwa kuitathimini Hali ya mitaani na hasa kwa watu wa kawaida wanafikiria Nini kuhusu JPM na namna anavyokejeliwa..wengine humu wanafanya hata kufurukusema wataenda kuweka kinyesi kwa kaburi la wanayemsema eti ni mwendazake..just imagine...Yaani humu mitandaoni Baadhi wamerundikana na kusema bad things against JPM na hakuna anayekemewa...mitaani watu in millions mioyo ya watu inavuja damu kwa kupotolewa na mtetezi wao...
Hao wasukuma wanaobaguliwa Sasa kumbukeni wako zaidi ya milioni 10 nchi nzima...mamilioni ya watu wengine pia are watching..
Kuhusu Corona let us wait and see .tuone hiyo taarifa ya kamati ya watu hao itatekelezwa vipi...lakini ni kweli Kuna divided opinion ndani ya nchi kuhusu taarifa hiyo...very divided opinion...Sasa Kama watu wanaoona taarifa ya kamati hiyo Haina Jambo la maana na kubatizwa kuwa ni genge la wasukuma tutaona athari zake...tungojee tuone...
Ndio maana sijaweka hilo neno sukuma gang, najua hiyo ni codeword tu lakini hilo ni genge nufaika na ukoloni uliopita- siyo wasukuma pekee na pengine wasukuma ni wachache sana humo.
Kuhusu corona inanisikitisha na jinsi watu wengi wasivyokuwa na informations sahihi kutoka nchi ambazo corona imezipiga sana kujua sababu yake na jinsi wanavyofight against.- kwenye kipengele hiki wameingia wapotoshaji ambao sijui wana makusudi gani ya kufanya hivyo.
 
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​

---

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA​

KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA​

MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA

WA COVID-19 NCHINI​

DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari,
mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,

2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:

1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.

2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.

4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.

5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:


a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;

b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;

c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:

i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.

e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.

6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.

7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.

8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.

9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.

14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.

15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.

16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.

17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.

18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.

19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
Yaani kwa nchi yetu imebidi iundwe tume ya wataalamu kutushauri jambo hili?
 
Chanjo iletwe kwa anayetaka hatutaki kuchwa kwa kulazimishana hapa. Sisi wengine tumaini na tegemeo letu ni Bwana Yesu wa Nazareti aliye hai, ndiye chanjo yetu na mlinzi wetu wa uhakika hatuhitaji kuhusishwa na kuwa sehemu ya huu upuuzi.

Team ya madaktari inashauri wachanjwe waongoza watalii kwa nini wasianze wenyewe hao madaktari kuchwanjwa? Maana wao pia wako ftont line. Hatutakubali kuwa sehemu ya kumdharaulisha Mungu tuliye mtegemea siku zote katika janga hili. Mungu wa mbinguni hadhihakiwi na wala watutokubali kuwa sehemu ya kumdhihaki Mungu wetu.
Kila mtu abaki na msimamo wake.ndio maana serikali haijalazimisha.
 
Hvi toka lini kutumia chanjo ni kumdhalilisha Mungu? Hvi bila ARVs Tanzania wangekufa watu wangapi? Je kutumia ARVs ni kupinga uweza wa Mungu au ni precaution tu?

Cha kushangaza ukiugua malaria huendagi kuombewa ila unaendaga pharmacy ila linapokuja suala la Corona ndio pharmaceuticals zinageuka dharau kwa Mungu?
weird
Kila mtu ana tafsiri yake kuhusu chanjo japo nina imani watanzania wengi tumepokea chanjo nyingi tuu tangu tukiwa wadogo ila kwa hii ya Corona watu wana wasiwasi.
 
... Rais na Mwenyekti wa Kamati kwenye makabidhiano ya ripoti (just two people) wamevaa barakoa halafu kapuku mwenzangu unajitoa ufahamu eti hakuna korona! Watch out!
Mkuu uraisi ni title tu,kuvaa kwake barakoa hakumfanyi kuwa sahihi kwa kila kitu
 
Mimi naamini Mungu alishatushindia Corona
Sitachanjwa na wala sitaki barakoa wavae wapagani wasio amini Mungu

Kuvaa barakoa kwanza kunaharibu sura MTU USO unaonekana kama wa kinyago cha kimakonde
Endelea kuwa na imani mkuu. Imani huponya.
 

Nawashangaa Baadhi ya watu kuanza mijadala ya kupinga suala la chanjo kama vile serikali imelazimisha kila mtu achanjwe.

Hatuwezi kuwa na mawazo yanayolingana ndani ya nchi hii tupo tunaotaka chanjo na tuna sababu zetu kwa mfano. Biashara za kimataifa, working overseas n.k kwa sasa kama huna kinga huwezi kuingia katika nchi zingine.
Na wanaopinga chanjo nao wana sababu zao kwamfano wengine wanasema chanjo ni mpango wa mabeberu kutuua .sawa zote ni sababu.

Kimsingi naipongeza serikali kuweka Uhuru kwa kila mwananchi kuamua anaetaka sawa na asiyetaka sawa. TUSIPANGIANE.
Iletwe kwa pesa zetu za kodi au kwa pesa zako binafsi? Muda mwingine muache kutumia makalio kufikiri, hata kama sio lazima, kodi yangu si ya kuchezea hivyo, ebo!
 
Hao wanaojiita maproffesor jana hata sura zao zinaonyesha walivyo guilt. Corona watu wanafunga virago nyie ndiyo mnataka kufanya agenda? Hawa wanatakiwa waitwe proffesseur ya kifaransa maana ili ya kiingereza hawana sifa.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Mnapata taabu Sana kupotosha what is going on in this country at the moment. .the country is more divided now than ever ..mnapotosha kwa kudai kuwa kuwa Kuna genge or gang au to be specific the so called Sukuma gang...
Huu ni mwendelezo tu, wakati wa JPM watu waliokuwa wakitoa ushauri tofauti waliitwa wachochezi, hawana uzalendo, wanatumiwa na mabeberu mpaka Kabudi akasema wakae kimya. Sasa kibao kimegeuka, watu wanalalamika.

Kuhusu Usukuma, sio wamebatizwa, ni JPM alienda Mwanza akasema "hawa ni wapiga kura wangu, msiwabomolee" kwani Kimara hakukuwa na wapiga kura wake? Ni Gwajima ndio alitengeneza clip ya kikabila akihimiza wasukuma waunde vikundi vya kumtetea JPM. Gwajima hajawahi kuomba radhi wala JPM hakuwahi kumkemea. Imagine Butiku atengeneze clip ya kuhamasisha watu wa Mara kutengeneza vikundi vya kumtetea Nyerere, je mwalimu angefanya nini?

Hizi negativity ni matokeo ya miaka 5 ya utawala wa kishamba, kimabavu, kionevu na uliojaa upendeleo.
 
Kwakuwa waTz wameishi na kike kinachoitwa Corona kwa miaka miwili sasa na hakuna imoact ueyote tuliyoiona, mi nadhani huo wote ni utopolo tu, hakai mtu lockdown, na hizo pesa za kodi wanazotaka kuchezea kwenye chanjo watazitapika!!
 
Acha u.fala nani kakulazimisha!?
Huna abc yoyote kuhusu elimu ya afya unaropokwa tu.
"+&@$ wahed
Wewe unaonekana ni mtoto wa juzi,na bado haujaijua vizuri dunia.Hao wenye ABC yoyote kuhusu elimu ya afya, wengi tunao huku wamepata matatizo ya kiafya yasiyotatulika kwa hiyo elimu zao.
 
Baada ya mda mrefu naona wataalam Tanzania wanaanza kurudia elimu zao! Sijui mwendazake angetuongoza kwa miaka mingine kumi ingekuwaje...
Tanzania kuna wataalamu? We unaliwa wewe sio bure[emoji28][emoji28].
 
WASTAGE OF MONEY NGOJA IKUPIGE NDIO UTAJUA KAMA NI MATUMIZI MABAYA watu hatuna shukrani at all....
Corona ni no vijimafua tu, na haiwezi kunifanya chochote. Kama ingekuwa na nguvu kiasi hicho, tangu iingie 2020 nisingekuwepo. Ni upumbavu na upetezaji wa hela tu.
 
Huyo ndio kiongozi wa Kweli, maana ya kiongozi ni kujitoa kwa ajili ya watu wako,hata kama itakugalimu maisha yako,sio huyu takataka kazi ni kujipamba na kupaka lipstick tu, unafikiri anatafuta umiss Tanzania
Naona kenyataa kamwambia haya..pengine ..hii covid ni chaos tu ..tumeishi nayo na haya juzi WHO kwenye taarifa yao walisema wanafikiri kuachana na kudeal na sheria kali za ugonjwa huu..hii inamaana wameshajua kuwa huo ugonjwa ni hofu tu ..ambayo watanzania hatykuwa nao..Mimi nitawaelewa Sana Kama hawataanza kuleta sheria lazimishi za kuwataka watu wazingatie hayo masharti ya kuvaa barakoa..sijui n.k
 
Back
Top Bottom