#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Mkuu umeeleza vyema kunawatu wanataka kutufanya Kama viziwi yaan wao ndo wanasikia tuuuuuu... Anyway tunakwenda kuangamizwa bure kwa kutiwa hofu ili watu wafe kwa hofu... Sa iv wanafunzi wanasoma kwa aman kabisa, watu wanasafri bila kuogopana, wanasafrisha bidhaa na kuuza bila shida kabisa... Kunastarehe za kila aina na n.k

Sasa njoo uone kitakachotokea pind takwimu zikianza kutolewa yaan wagonjwa watazid mpka hospital zitalemewa na kunaweng tu hawataugua ila hofu itawauguza na wengi Zaid kufa
Ngoja tuone mkuu
 
Kwakuwa waTz wameishi na kike kinachoitwa Corona kwa miaka miwili sasa na hakuna imoact ueyote tuliyoiona, mi nadhani huo wote ni utopolo tu, hakai mtu lockdown, na hizo pesa za kodi wanazotaka kuchezea kwenye chanjo watazitapika!!
Cool bana, hakuna aliyetangaza lockdown. Wananchi walikaririshwa kipindi kile kuwa mabeberu wanataka muweke lockdown- ulikuwa uongo mtupu.
Na chanjo itakuwa hiari,, so endelea kurelax.
 
Mkuu umeeleza vyema kunawatu wanataka kutufanya Kama viziwi yaan wao ndo wanasikia tuuuuuu... Anyway tunakwenda kuangamizwa bure kwa kutiwa hofu ili watu wafe kwa hofu... Sa iv wanafunzi wanasoma kwa aman kabisa, watu wanasafri bila kuogopana, wanasafrisha bidhaa na kuuza bila shida kabisa... Kunastarehe za kila aina na n.k

Sasa njoo uone kitakachotokea pind takwimu zikianza kutolewa yaan wagonjwa watazid mpka hospital zitalemewa na kunaweng tu hawataugua ila hofu itawauguza na wengi Zaid kufa
Hofu inalazimishwa ili tu kuonyesha kuwa hatua zinazochukuliwa sasa si sahihi kwasababu za ajabuajabu sana.
Mbona kikitokea kipindupindu tunaelezana njia za kukiepuka na wala hatuonyani kuhusu hofu?? Wala hatusemi haya masharti ya kipindupindu yataleta hofu hivyo watu watakufa sana.
Watanzania mlikuwa brainwashed na wansiasa wachumia tumbo hakika.
Lakini cha kujiuliza ,,tumeishi kwa kutegemea hii sayansi kwa muda mrefu sana, kwanini sasa??
Lakini pamoja na hayo ,magonjwa yote yakitokea tunaikimbilia sayansi,,, kwanini corona pekee??

Je ni kweli mzungu anashindwa kukuua wewe mbongo ikiwa kweli anataka kukuua mpaka aisubiri corona??

Hebu fikiria wakiamua kuwaua kwa kupitia AC za magari mnayonunua kwao watashindwa??

Amka mbongo ,,fikiria logically.
 
Kamati ya Corona imeishauri Serikali ya Tanzania;

1) Itangaze uwepo wa Corona
2) Iruhusu matumizi huru ya Chanjo sahihi za Corona
3) Ikubali maadhimio ya Kikanda na Kimataifa
4) Ipanue maktaba za kupima
5) Itoe takwimu sahihi za Corona
6) Tiba asili zitathiminiwe Kisayansi

View attachment 1788449
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kufanya tathmini ya Ugonjwa wa Corona -COVID -19 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Said Aboud​

---

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU YATOKANAYO NA RIPOTI YA​

KAMATI MAALUMU YA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA​

MUUNGANO WA TANZANIA YA KUFANYA TATHMINI YA UGONJWA

WA COVID-19 NCHINI​

DAR ES SALAAM 17 MEI, 2021

Ndugu wanahabari,
mtakumbuka kwamba kupitia hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
aliyoitoa tarehe 6 Aprili, 2021 wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu kuunda Kamati ya kitaalamu ya kufanya tathimini ya ugonjwa wa COVID-19 na baadaye msisitizo alioutoa tarehe 22 Aprili,

2021 wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma, naomba kuwajulisha kuwa Kamati hiyo imewasilisha rasmi ripoti yake kwa Mheshimiwa Rais leo tarehe 17 Mei, 2021.

Ndugu Wanahabari, Kamati ilifanyia kazi hadidu za rejea 12 zilizohusu maeneo mbalimbali ya tathmini ya mwenendo wa ugonjwa pamoja na afua za udhibiti wa COVID-19 ikiwemo chanjo hapa nchini, kikanda na kimataifa.

Ndugu Wanahabari, Tangu kuingia kwa ugonjwa wa COVID-19 nchini mwezi Machi 2020, Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani na kuna tishio la kutokea kwa wimbi la tatu hapa nchini.

Ndugu Wanahabari, Baada ya uchambuzi wa kina Kamati imependekeza yafuatayo:

1. Serikali ihuishe mipango ya dharura (Contigency and Response Plans) katika ngazi zote kwa ajili ya kukabiliana na majanga likiwemo janga la ugonjwa wa COVID-19.

2. Serikali itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga
(interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa huo.

3. Wataalamu wa afya watimize wajibu wao kitaalamu, kwa kuzingatia weledi, miiko na maadili katika kuelimisha, kukinga na kutibu ugonjwa wa COVID-19 nchini.

4. Tanzania ishiriki ipasavyo katika maamuzi na itekeleze maazimio ya kikanda na kimataifa iliyoridhia katika jumuiya za EAC, SADC, AU na WHO.

5. Kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19:

a. Kamati inashauri Serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 kwa kutumia chanjo zilizoorodheshwa na Shirika la Afya Duniani ili kuwapa fursa ya kinga wananchi wake kwa kuwa kupitia uchambuzi wa Kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi;

b. Pamoja na mapendekezo haya, Kamati Huru ya Kitaifa ya Ushauri wa Chanjo (NITAG) na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ziendelee kushirikishwa katika kutoa ushauri na kudhibiti chanjo hizo;

c. Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi yafuatayo kwa umuhimu:

i. Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wa huduma (frontline workers) mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji;
ii. Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50;
iii. Watu wazima wenye maradhi sugu mengine (comorbidities) mathalani kisukari, shinikizo la damu, maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k.;
iv. Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama; na
v. Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi.
d. Kufanya uhamasishaji na maandalizi ya upokeaji, utunzaji, usafirishaji na utoaji wa chanjo na wananchi wawe huru kuamua kuchanja au la.

e. Serikali iratibu upatikanaji wa chanjo kwa watumishi wa taasisi za kimataifa walioko nchini.

6. Serikali ya Tanzania ijiunge na COVAX Facility kwa kuwasilisha andiko la kupatiwa chanjo, kwa kutumia fursa inayotolewa na GAVI.

7. Serikali itumie fursa zilizopo wakati huu wa janga la COVID-19 kuanza mchakato wa uanzishaji wa viwanda vya kutengeneza chanjo.

8. Serikali iimarishe huduma za uchunguzi kwa kuijengea uwezo Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na maabara nyingine nchini ili kupanua wigo wa upimaji wa ugonjwa wa COVID-19.

9. Serikali ijenge uwezo wa ndani wa utambuzi wa virusi anuai vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.

10. Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa wa COVID-19 kwa umma na Shirika la Afya Duniani ili wananchi wapate taarifa sahihi toka Mamlaka za Serikali na kuheshimu makubaliano na kanuni ambazo nchi iliridhia.

11. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikamilishe mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa wa COVID-19.

12. Serikali iendelee kuhakikisha kuwa matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi.

13. Serikali iendelee kutoa fursa na kuwawezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa kufuata miiko, maadili na taratibu zilizowekwa ili kuimarisha kinga, tiba, uchunguzi wa ugonjwa wa COVID-19 na athari zake katika jamii nchini.

14. Serikali iendelee kuzingatia mazingira ya kitanzania katika udhibiti wa ugonjwa wa COVID-19 katika kuamua kuweka au kutokuweka shuruti ya kujifungia (lockdown) na kuwa na ubunifu ili kuruhusu ukuaji wa uchumi na kuimarisha sekta zinazochangia katika uchumi.

15. Wizara yenye dhamana ya fedha na uchumi ifanye tathmini ya kina ya athari za janga la COVID-19 na kuweka mpango madhubuti wa haraka wa sasa, wa muda wa kati na wa muda mrefu unaotekelezeka ili kukuza uchumi wa nchi.

16. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ziendelee kushirikiana ipasavyo katika hatua zote za kukabiliana na janga la COVID-19 pamoja na majanga mengineyo ikiwemo utoaji wa nyaraka za kimataifa kama vile Travel Advisory Note.

17. Idara ya Maafa katika Ofisi ya Waziri Mkuu iendelee kutekeleza ipasavyo jukumu la uratibu na kutoa rasilimali husika wakati wa majanga ya kitaifa na kimataifa kama ugonjwa wa COVID-19 kwa kushirikisha ngazi na sekta zote.

18. Serikali ikamilishe malipo ya madeni ya watoa huduma na watumishi waliokuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19 ili kuongeza ari na tija ya udhibiti wa ugonjwa huo.

19. Serikali iendelee kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wadau wa maendeleo, sekta binafsi na vyombo vya habari katika mapambano dhidi ya janga la ugonjwa wa COVID-19.

Ndugu Wanahabari, Asanteni kwa kunisikiliza.
1621372967922.png
1621373313260.png

Niombe serikali kutoa agizo la ABIRIA wote kukaa viti kwenye daladala au magari ya biashara ya usafiri wa abiria; kwa kuzingatia idadi ya viti vya abiria katika gari husika, kama kweli imeanza kupambana na covid-19 kama tulivyojitahidi mwaka uliopita !
1621373438524.png
1621373513232.png
1621373556379.png
 
Korona ipo haipo? Watu wanakufa hawafi? Mnaogopa kuambiwa ukweli au? Ina maana timu ya wataalamu imetudanganya?

Lini watu waliacha kufa? Chanjo ya Malaria iko ima haiko?. Kwa nini maendeleo ya sayansi na technologia yaliyo wezesha upatikanaji wa chanjo ya corona kwa kasi ya voda fasta yasiwezeshe na chanjo ya malaria? Maana wako wataalamu wanasema upatikanaji wa chanjo ya corona ndani ya kipindi kifupi umesababishwa na maendeleo ya technologia.

Unaposema unachanja watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama kuna uhiari tena hapo au ni mwendo wa amri na ndio afande, timamu. Tusidanganyane wako watu wamedhamiria kuwa madalali wa chanjo na vifaa tiba.

Wengine hatuko tayari kuwa nguruwe guinea/panya weupe wa majaribio kwa hii chanjo ya korona.

'Nguto' kwa kikojani ni 'tiger.'
 
Cool bana, hakuna aliyetangaza lockdown. Wananchi walikaririshwa kipindi kile kuwa mabeberu wanataka muweke lockdown- ulikuwa uongo mtupu.
Na chanjo itakuwa hiari,, so endelea kurelax.
Hiari hilo liko wazi, suala ni pesa zitakazotumika kuagiza, ni kodi zetu au ni zao binafsi?
 
View attachment 1790203 View attachment 1790208
Niombe serikali kutoa agizo la ABIRIA wote kukaa viti kwenye daladala au magari ya biashara ya usafiri wa abiria; kwa kuzingatia idadi ya viti vya abiria katika gari husika, kama kweli imeanza kupambana na covid-19 kama tulivyojitahidi mwaka uliopita !
View attachment 1790213 View attachment 1790214View attachment 1790215
Tangu Corona imeanza na watu wamekaa kwa kubanana hivyo, kuna chochote kimetokea?
 
Hiari hilo liko wazi, suala ni pesa zitakazotumika kuagiza, ni kodi zetu au ni zao binafsi?
Hayo ndiyo matumizi sahihi ya kodi za wananchi.
Watu walitaka kulazimishia kijiji kiwe jiji tuliona poa tukasema ni sehem ya Tanzania, halafu eti tuone ni dhambi serikali kulinda wananchi wake dhidi ya magonjwa.
 
Finaly we are here, wanaotaka chanjo wasinyimwe haki yao, na wasiotaka pia waheshimiwe, sijui mwendazake angekua macho angesemaje
Mimi sina imani nao hao watu wa Laboratory tangu Hayati Dr Magufuli kuwapa Vipimo vya Mbuzi ,Damu ya kwale,mafuta ya dizeli na mafenisi yote hayo walipima hao Wana-Sayansi wa Laboratory. Na Wakakuta Vipo Positive Covid19?
Leo Mheshimiwa Rais Mama Suluhu amewapa hao hao Wana -Sayansi wa Laboratory kupima Chanjo ya Corona Virus? Unafikiri watasema haifai kuchanjwa? Au si Salama? Sisi Waafrika Akili zetu kitu kikitoka kwa Mzungu tuna imani kipo salama. Kumbe kina madhara makubwa sana.

RAIS MAGUFULI.jpg
 
Halafu ili kutudanganya wamecopy na kupaste mavolume ya vitabu sijui nani atayasoma hayo mavitabu, kwanza siamini kuwa kwa muda mfupi kiasi hiki wameweza kuandika mihutasari/ripoti na taarifa za kitibabu kwa hayo mavitabu na mwisho hakuna tafiti ya kitibabu inakuwa tayari kwa muda mfupi namna hiyo pia ripoti inatakiwa ituambie na madhara ya hizo chanjo, muda wa kutumia au kutokutumia, hayo yote hayajazungumziwa hadharani wakati yalitakiwa yaongelewe hadharani ili kutoa wasiwasi kwa wananchi,haitoshi tu kusema chanjo hii ni salama ,tusisahau hawa hawa watalaamu wetu ndio walisema GMO inatufaa, ni hawa hawa watalaamu wetu wameruhusu wakulima watumie dawa ya uuawa magugu ya Roundup itumike wakati huko huko Marekani inakotengenezwa imepigwa marufuku na hadi vibao vya matangazo vimewekwa jwenye highway zao kupiga marufuku dawa hiyo lakini huku kwetu hadi sasa imejaa maduka ya dawa na bado inatumiwa na wakulima . Mwendazake hakuwa mjinga alipokuwa na wasiwasi na hata aliposema mashine za kupima virusi vya corona vina matatizo wengi walimkebehi lakini mwisho wake ikawa aibu kwao baada ya kugundulika hizo mashine kuwa zina matatizo na nchi kadhaa kuacha kuzitumia.
Tanzania Hakuna Wataalam Wazuri ni watu kuiga atakacho kisema mtu Mweupe M-Taaalam wa Tanzania hawezi kukipinga. tuna Wana-Sayansi feki Tanzania.
 
Hofu inalazimishwa ili tu kuonyesha kuwa hatua zinazochukuliwa sasa si sahihi kwasababu za ajabuajabu sana.
Mbona kikitokea kipindupindu tunaelezana njia za kukiepuka na wala hatuonyani kuhusu hofu?? Wala hatusemi haya masharti ya kipindupindu yataleta hofu hivyo watu watakufa sana.
Watanzania mlikuwa brainwashed na wansiasa wachumia tumbo hakika.
Lakini cha kujiuliza ,,tumeishi kwa kutegemea hii sayansi kwa muda mrefu sana, kwanini sasa??
Lakini pamoja na hayo ,magonjwa yote yakitokea tunaikimbilia sayansi,,, kwanini corona pekee??

Je ni kweli mzungu anashindwa kukuua wewe mbongo ikiwa kweli anataka kukuua mpaka aisubiri corona??

Hebu fikiria wakiamua kuwaua kwa kupitia AC za magari mnayonunua kwao watashindwa??

Amka mbongo ,,fikiria logically.
Mkuu sio kwamba watu wanapingana na sayansi ila uhalisia ndio unaopingana na hiyo mnayoita sayansi, kwa jinsi ambavyo bongo tulivyojiachia kwa kutozingatia taratibu za kujikinga na corona basi ilitakiwa tuone athari zake kwa kiwango kikubwa kabisa na hali hiyo ingeelezeka kisayansi kama inavyoelezeka huko India, lakini uhalisia unaeleza tofauti na hiyo sayansi mnayoizungumzia. Bongo tumekuwa ndio kwanza tunaogopa kuletewa corona kutoka nchi za nje kama huko India au Afrika kusini.
 
Kwanza hatuweki record yoyote hivyo situation chini kwetu ni ya kuhisia tu.
Kwanini India iko vile: Ni vizuri pia kutafiti hizo sababu,, mpaka sasa zipo ambazo hazijathibitika.

Mfano mzuri kwako ni Rwanda.
 
Record zingetueleza tumeathirika kwa kiasi gani lakini wakati huo athari tunaziona, yani ilitakiwa tuone hospitali kuzidiwa kuelemewa kwa wagonjwa wenye kuhitaji mashine za kusaidia kupumua na hali ya mazishi kuongezeka kama ambavyo tumesikia wenzetu sehemu za kuhifadhi maiti zilijaa na huko India tunasikia hadi kuni za kuchomana zimeisha. Sasa hizo ni athari ambazo tungeziona na hapo ndio record zingetuambia kiwango cha maambukizi,wagongwa waliyopo na vifo. Sasa huwezi kusema hatuoni hayo kwa sababu hatuweki record.
 
Sasa tumeamua tutafute data ili tujue nguvu ya adui wetu na kisha tujue tunamtokomeza kiasi gani,- lina ubaya hilo?
Dunia inairate kila nchi kulingana na situation yake, Tanzania imekuwa siku zote ni unknown , hata tu jinsi ya kujieleza ni aibu tupu.
 
Mwendazake alitupoteza sana, kusema chanjo ya Corona ina matatizo wakati chanjo nyingine za wazungu tunazitumia miaka mingi hakuwa sawa, hasa alipodai wazungu hawatupendi it was such a very primitive mentality.
Alichokisahau yeye na waliomuunga mkono ni kuwa vingi vya mabeberu tunavyovitumia kv: "mionzi ya simu, magari, ndege zifushazo moshi angani zinapokatiza anga letu... vifaa tiba toka hukohuko kwa wazungu" walijiridhisha kuwa havina athari???
 
umieni Chanjo kutoka China ambayo hadi sasa haijapatikana na kasoro za kuhatarisha maisha kama chanjo zinazoka kwa wazungu .
 
Back
Top Bottom