Kamati ya hadhi ya wachezaji imeshindwa kuamua kesi ya Fei Toto

Kamati ya hadhi ya wachezaji imeshindwa kuamua kesi ya Fei Toto

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Ngoja niwe mkweli, kamati ya hadhi ya wachezaji haiwezi kuamua kesi ya Fei Toto, nimesikiliza interviews za Mwenyekiti Mzee Said Sudy namna anavyoongea unajua kabisa hakuna wanachoweza kuamua.

Kamati inataka kusawazisha ubao, inataka kuibeba Yanga, inataka kujisafisha mbele ya Yanga kutokana na mahusiano yao kuanzia kesi ya Morrison na sakata la “Bingwa la Kufeli”.

Hakuna mkataba wa kazi duniani hauvunjiki na hakuna namna ya mkataba wa Feisal umeelekeza kwamba hawezi kuuvunja akaondoka. Wanaoimba Busara wanataka Fei aingie upepo na arudi Yanga kutumikia mkataba asoupenda.

Waandishi na watu wenye nguvu mitandaoni wanatumika kupotosha hili sakata makusudi ili kutisha wachezaji wazawa waendelee kucheza kwa huruma. Lakini ukweli ni kwamba FEISAL keshaondoka Yanga na sasa au mwisho wa msimu atacheza sehemu nyingine.

GENDAEKA wengi wanapiga kelele ili kuifunika Kamati ya hadhi ya wachezaji ambayo kimsingi ni kamati dhaifu. Kwangu mimi hii kesi Feisal anakwenda kushinda CAS au mamlaka za kinchi lakini hawezi kucheza Yanga. Yanga wakubali tu kwamba Feisal ana uwezo wa kununua mkataba wake na akaendelea na maisha mengine.

Hili litakua funzo kwa idara za Sheria pamoja na wanaosajili wachezaji na wanaosimamia wachezaji. Niwakumbushe tu, hakuna mkataba usofunjika Duniani kote. Kama Simba walivyovunja mkataba kwa Akpan na Okwa na kama Yanga kwa Kambole.

Che Guevara🫡

NB:
Vicent Aboubakary baada ya kutakiwa na Man United ameamua kuvunja mkataba na Al Nasry.
 
Mpole vs Geita

Yeah mikataba inavunjika vizuri tu, tena mchana kweupe. Na niwachache sana wanao shindwa kuvunja mikataba yao

Al nasr wangeweza kugoma ili waweze kupata pesa ya kumuuza huyu mkameruni kwa nanchester utd

Pia sina kumbukumbu nzuri, hivi yule cheupe wa angola alivunja mkataba au walimuuza kwenda kwao?
 
Mleta bandiko ni mmoja wa ma Mbumbumbu walio bobea, Ata uyo Mzee Sudy ambaye ume mnukuu akitoa ufafanuzi hakusema kwamba Feisal hawezi Kuvunja mkataba.

Alicho Sema alichotakiwa Feisal ni kukaa na Yanga na kuwaeleza haridhiki na mkataba alionao na kutokana na wao kushindwa ku uboresha angeomba kuondoka.

Inamaana Yanga wange mjibu Kwa maandishi, Sababu za wao kutoweza kuboresha mkataba wake na kupitia andiko ilo la klabu, Feisal angekua amepata kielelezo Cha kuonyesha walisha Kaa na Yanga kujadili swala lake na hawakufikia muafaka.

Kinacho mkwamisha Feisal ni kuonekana amevunja mkataba wa pande mbili bila kuwashirikisha waajiri wake.

Wapuuzi wengine wanadai Feisal hata akirudi hatocheza Kwa Moyo Wala furaha!

Yanga hai itaji Moyo wa Feisal, Moyo ubakie kusukuma damu anachotakiwa ni kuwajibika kwenye mkataba wake.

Feisal analipwa na klabu hachezi Bure, angekua anacheza bila kulipwa, hoja ya kucheza Kwa Moyo ingekua na mashiko.

Huu mkataba Feisal angefanikiwa ku
uvunja Kwa namna alivyo fanya, kwanza Dunia ingetuona watu wa ajabusana na ingeanzisha migogoro mingi baina ya wachezaji na klabu na wachezaji wangekua wakitumia reference ya mgogoro huu.

Kwa namna alivyo fanya Feisal ata aende CAS hatoboi, sanasana utakua ni mwendelezo wa Wanasheria wake kujitafunia pesa za Yusufu Bakresa.

Yusufu ambaye ndie yuko nyuma ya sakata hili, na Mimi nawashauri Wanasheria endeleeni kuzitafuna izo fedha msiwe na huruma hata kidogo, izo ni fedha zetu za matokeo ya kukwepa Kodi Serikalini Sasa zinampa jeuri.

Mwambie kule CAS mtafanya namna mtashinda iyo kesi Ili kuendelea ku utafuna uo mgodi wa fedha.
 
Umepuyanga tu bila hata kuweka vifungu vya sheria unavyotaka watu wajue kuwa Feisal ameonewa na kamati.
Ukiwa na akili timamu utagundua hakuna sehemu Yanga au kamati au mtu yoyote mwenye akili timamu amesema Feisal hawezi kuvunja mkataba na Yanga, ila kilichopo ni utaratibu na hajalazimishwa kubaki Yanga ila akafate utaratibu.

Sasa ukitaka kueleweshwa uliza ni utaratibu gani unatakiwa Feisal aufate ili kuvunja mkataba wake lakini ukija na haya matakataka yako ya sijui mbona Akpan na Okwa wamevunjiwa utaulizwa kuwa kwani unadhani mikataba ya wachezaji inafanana masharti yake?

Huyo Vincent Abubakar hujui hata kilichofanyika baina yake na Al Nasr ila unajaribu tu kufananisha vitu usivyovijua.
 
Ngoja niwe mkweli, kamati ya hadhi ya wachezaji haiwezi kuamua kesi ya Fei Toto, nimesikiliza interviews za Mwenyekiti Mzee Said Sudy namna anavyoongea unajua kabisa hakuna wanachoweza kuamua...
Inategemea na aina ya mkataba wenyewe; usifunike mikataba ya wachezaji wote kwa blanket moja.

Mikataba ya mpira inatakiwa kuwa na release clause ambayo inaruhusu mchezaji kuvunja mkataba na kuwa free agent au kununuliwa/kukodiwa na timu nyingine. Release clause kati ya mambo mengine huweka wazi kuwa hataruhusiwa kabla ya kuitumikia timu kwa kipindi fulani, na atakapotaka kuondoka atailipa timu pesa kiasi gani kulingana na timu itakavyoamua kuwa thamani yake itakuwa kiasi gani wakati huo. Thamani ya mchezaji haipimiwi kwa mashahara wake, ila thamani hiyo husaidia mchezaji kubargain mshahara mnono zaidi.

Hata hivyo kuna mikataba ya "gentleman's agreement" ambayo inaonekana kushamiri kwenye mpira wetu bila kuwa na release clause bali ni makubaliano tu baina ya mchezaji na timu. Kuvunja mkataba huu ni lazima upitie njia ya gentleman's agreement pia, yaani pande zote mbili husika zikubaliane.

Mikataba hii ni ngumu kuvunjwa kirahisi, na FIFA imetaja vigezo ambavyo vinaweza kutumiwa na mchezaji au timu kuvunja mkataba wa aina hiyo na lazima pia bado pande zote mbili zijadiliane kwanza, siyo kuamka tu na kusema leo sichezi mpira nimevunja mkataba.

Mkataba baina ya Mpole na Geita ulifuata vigezo hivyo vya FIFA. Mpole alisema aliumia akiwa mpirani halafu Geita haikumhudumia na akatoa ushahidi wa kuwa alikuwa anatibiwa Dar ambapo Geita haikulipia gharama hizo za matibabu.

Inawezekana ilikuwa ni janja yake tu lakini inaonekana alikuwa na msimamizi mzuri anayejua njia za kutengua mikataba ya gentleman's agreement kwa vigezo vya FIFA. Hata hivyo, bado Mpole na Geita walifikia makubaliano ya kvunja mktaba wake, siy tu kuwa George Mpole aliamka na kuvunja peke yake.
 
Ngoja niwe mkweli, kamati ya hadhi ya wachezaji haiwezi kuamua kesi ya Fei Toto, nimesikiliza interviews za Mwenyekiti Mzee Said Sudy namna anavyoongea unajua kabisa hakuna wanachoweza kuamua...
Wewe ndiyo mpotoshaji na kwa kuwa umejizima data kutokana na uchawa wako kwa Makolowzard SC maelezo aliyotoa mwenyekiti haiwezi yaekewa.

Ni sawa na mwanafunzi kuingia na majibu kwenye mtihani finally akakutana na maswali mengine kabisa ambapo majibu yake aliyobeba hayana nafasi, lazima ujikojolee tu.
 
Ngoja niwe mkweli, kamati ya hadhi ya wachezaji haiwezi kuamua kesi ya Fei Toto, nimesikiliza interviews za Mwenyekiti Mzee Said Sudy namna anavyoongea unajua kabisa hakuna wanachoweza kuamua...

Bila vifungu vya sheria umeandika upupu, kweli wa Tanzania tu mazuzu, hivi chombo kinachotumika kuamua si sheria?
 
Inategemea na aina ya mkataba wenyewe; usifunike mikataba ya wachezaji wote kwa blanket moja.

Mikataba ya mpira inatakiwa kuwa na release clause ambayo inaruhusu mchezaji kuvunja mkataba na kuwa free agent au kununuliwa/ kukodiwa na timu nyingine...
Mkuu, Mtoa Mada kama hatakuelewa basi atakuwa ni Mbumbumbu namba 1. Kingine nilichoelewa kuhusu sakata la Feisal na Yanga ni kuwa tuna Wanasheria wengi vilaza ambao wanaziaminisha hata kampuni na watu mashuhuri uongo wa kiwango cha juu. Vilevile, huenda wale 26 (kati ya wengi) waliofaulu mitihani wa Shule ya Sheria kuna uhalisia kuhusu matokeo yale.
 
Ngoja niwe mkweli, kamati ya hadhi ya wachezaji haiwezi kuamua kesi ya Fei Toto, nimesikiliza interviews za Mwenyekiti Mzee Said Sudy namna anavyoongea unajua kabisa hakuna wanachoweza kuamua...

NB:
Vicent Aboubakary baada ya kutakiwa na Man United ameamua kuvunja mkataba na Al Nasry.
uelewa wako mdogo sana
 
Mleta bandiko ni mmoja wa ma Mbumbumbu walio bobea, Ata uyo Mzee Sudy ambaye ume mnukuu akitoa ufafanuzi hakusema kwamba Feisal hawezi Kuvunja mkataba...
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
 
Yanga acheni kulazimisha dogo hawataki tena,kitendo alichokifanya kinajieleza kabisa hautaki mshahara wenu,anachozaka ni kuondoka tu.

Hata mkikaa mezani swala litabaki pale pale....vipengele vya mikataba ni vibovu sana...pia ujanja ujanja wa kuwanyonya wachezaji wazawa ufike mwisho...unaweza kuta hiyo M4 fei anakula m2 zingine zinaenda juu KWA juu.
 
Yusuph Kagoma kanunua mkataba wake kwenda SBS mbona hakuna kesi......soka la Bongo la hovyo sana....akili zote zimeishia Simba na Yanga tu.
 
Ngoja niwe mkweli, kamati ya hadhi ya wachezaji haiwezi kuamua kesi ya Fei Toto, nimesikiliza interviews za Mwenyekiti Mzee Said Sudy namna anavyoongea unajua kabisa hakuna wanachoweza kuamua.

Kamati inataka kusawazisha ubao, inataka kuibeba Yanga, inataka kujisafisha mbele ya Yanga kutokana na mahusiano yao kuanzia kesi ya Morrison na sakata la “Bingwa la Kufeli”.

Hakuna mkataba wa kazi duniani hauvunjiki na hakuna namna ya mkataba wa Feisal umeelekeza kwamba hawezi kuuvunja akaondoka. Wanaoimba Busara wanataka Fei aingie upepo na arudi Yanga kutumikia mkataba asoupenda.

Waandishi na watu wenye nguvu mitandaoni wanatumika kupotosha hili sakata makusudi ili kutisha wachezaji wazawa waendelee kucheza kwa huruma. Lakini ukweli ni kwamba FEISAL keshaondoka Yanga na sasa au mwisho wa msimu atacheza sehemu nyingine.

GENDAEKA wengi wanapiga kelele ili kuifunika Kamati ya hadhi ya wachezaji ambayo kimsingi ni kamati dhaifu. Kwangu mimi hii kesi Feisal anakwenda kushinda CAS au mamlaka za kinchi lakini hawezi kucheza Yanga. Yanga wakubali tu kwamba Feisal ana uwezo wa kununua mkataba wake na akaendelea na maisha mengine.

Hili litakua funzo kwa idara za Sheria pamoja na wanaosajili wachezaji na wanaosimamia wachezaji. Niwakumbushe tu, hakuna mkataba usofunjika Duniani kote. Kama Simba walivyovunja mkataba kwa Akpan na Okwa na kama Yanga kwa Kambole.

Che Guevara🫡

NB:
Vicent Aboubakary baada ya kutakiwa na Man United ameamua kuvunja mkataba na Al Nasry.
Nyie simba mmejizoesha kuiba iba vya wenzenu,hii figisu yote ni nyie,mbona hili swala mnalishupalia sana,
 
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
Kwani anaogopa nin kukaa mezani na waajiri wake?
 
Hakuna mkataba wa kazi duniani hauvunjiki na hakuna namna ya mkataba wa Feisal umeelekeza kwamba hawezi kuuvunja akaondoka. Wanaoimba Busara wanataka Fei aingie upepo na arudi Yanga kutumikia mkataba asoupenda.
Fei..akamatie hapo hapo, akirudi tu huko Utopoloni amejimaliza.
 
Back
Top Bottom