Kamati ya hadhi ya wachezaji imeshindwa kuamua kesi ya Fei Toto

Kamati ya hadhi ya wachezaji imeshindwa kuamua kesi ya Fei Toto

Ngoja niwe mkweli, kamati ya hadhi ya wachezaji haiwezi kuamua kesi ya Fei Toto, nimesikiliza interviews za Mwenyekiti Mzee Said Sudy namna anavyoongea unajua kabisa hakuna wanachoweza kuamua.

Kamati inataka kusawazisha ubao, inataka kuibeba Yanga, inataka kujisafisha mbele ya Yanga kutokana na mahusiano yao kuanzia kesi ya Morrison na sakata la “Bingwa la Kufeli”.

Hakuna mkataba wa kazi duniani hauvunjiki na hakuna namna ya mkataba wa Feisal umeelekeza kwamba hawezi kuuvunja akaondoka. Wanaoimba Busara wanataka Fei aingie upepo na arudi Yanga kutumikia mkataba asoupenda.

Waandishi na watu wenye nguvu mitandaoni wanatumika kupotosha hili sakata makusudi ili kutisha wachezaji wazawa waendelee kucheza kwa huruma. Lakini ukweli ni kwamba FEISAL keshaondoka Yanga na sasa au mwisho wa msimu atacheza sehemu nyingine.

GENDAEKA wengi wanapiga kelele ili kuifunika Kamati ya hadhi ya wachezaji ambayo kimsingi ni kamati dhaifu. Kwangu mimi hii kesi Feisal anakwenda kushinda CAS au mamlaka za kinchi lakini hawezi kucheza Yanga. Yanga wakubali tu kwamba Feisal ana uwezo wa kununua mkataba wake na akaendelea na maisha mengine.

Hili litakua funzo kwa idara za Sheria pamoja na wanaosajili wachezaji na wanaosimamia wachezaji. Niwakumbushe tu, hakuna mkataba usofunjika Duniani kote. Kama Simba walivyovunja mkataba kwa Akpan na Okwa na kama Yanga kwa Kambole.

Che Guevara🫡

NB:
Vicent Aboubakary baada ya kutakiwa na Man United ameamua kuvunja mkataba na Al Nasry.
ni kweli hakuna mkataba usiovunjika duniani lkn haijawai kutokea mtu akavunja mkataba kwa namna feisal alivyovunja,dogo ataondoka yanga kwa signing fee yeye na vilaza wenzie waliomrubuni wajiandae kwa hilo ila sio kwa kuvunja mkataba...
 
Mtu ameshaonesha jeuri alafu bado mnamng'ang'ania wa nini?
Mwacheni aende atakako!
 
Hakuna mahali popote kwenye mkataba wa Feisal panapotamka suala la kukaa mezani kuzungumza kwanza ikiwa Feisal atataka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama za mkataba wake.

TFF ni wajinga na wapuuzi.
Nilikuwa nashangaa watetezi wa100 kumbe ni vilaza hivi!
 
Mmejaa ujinga mwingi sana, kama mambo yangekuwa mepesi kama mnavyojaribu kujidanganya, hao TFF na Kamati yake wasingepoteza muda ili kuwabeba, utetezi wenu kwenye hii issue ni ujinga mtupu.
Kwenye hii case nyinyi mnahusika kama nani?
 
Umeandika kwa hisia tu , hujaweka Facts Matters wala Legal matters.

Umeandika Upumbavu, Sheria hizi zinalinda wachezaji lakini pia zinapaswa zilinde VILABU .
 
Yanga acheni kulazimisha dogo hawataki tena,kitendo alichokifanya kinajieleza kabisa hautaki mshahara wenu,anachozaka ni kuondoka tu.

Hata mkikaa mezani swala litabaki pale pale....vipengele vya mikataba ni vibovu sana...pia ujanja ujanja wa kuwanyonya wachezaji wazawa ufike mwisho...unaweza kuta hiyo M4 fei anakula m2 zingine zinaenda juu KWA juu.
ALIUSAINI AMA LAH...

Kkabu inafanya biashara pia, siyo kituo cha kulelea Yatima mzee
 
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
Vipi kama wachezaji wote kwa timu wakifanya hivyo katikati ya msimu.Kila siku anaamka mmoja anaweka hela kwa account anasepa(bila majadiliano yoyote na timu).Mwisho wa mwezi timu inabaki na kocha pekee...vipi hapo watakuww wamevunja mkataba kwa halali?
 
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
Wewe ni kiazi asee!!, Hata mikataba ya kawaida tu mfanyakazi lazima umuarifu Boss wako kabla ya miezi mitatu... Tz tunawajuaji wahovyo sana..
 
Vipi kama wachezaji wote kwa timu wakifanya hivyo katikati ya msimu.Kila siku anaamka mmoja anaweka hela kwa account anasepa(bila majadiliano yoyote na timu).Mwisho wa mwezi timu inabaki na kocha pekee...vipi hapo watakuww wamevunja mkataba kwa halali?
Unayemweleza hajui hata maana ya mkataba. Kajaa ushabiki na bendera fuata upepo. Mwenye akili timamu hawezi kusema mtumishi anaweza kuacha kazi bila kumjulisha mwajiri.
 
Mleta bandiko ni mmoja wa ma Mbumbumbu walio bobea, Ata uyo Mzee Sudy ambaye ume mnukuu akitoa ufafanuzi hakusema kwamba Feisal hawezi Kuvunja mkataba.

Alicho Sema alichotakiwa Feisal ni kukaa na Yanga na kuwaeleza haridhiki na mkataba alionao na kutokana na wao kushindwa ku uboresha angeomba kuondoka.

Inamaana Yanga wange mjibu Kwa maandishi, Sababu za wao kutoweza kuboresha mkataba wake na kupitia andiko ilo la klabu, Feisal angekua amepata kielelezo Cha kuonyesha walisha Kaa na Yanga kujadili swala lake na hawakufikia muafaka.

Kinacho mkwamisha Feisal ni kuonekana amevunja mkataba wa pande mbili bila kuwashirikisha waajiri wake.

Wapuuzi wengine wanadai Feisal hata akirudi hatocheza Kwa Moyo Wala furaha!

Yanga hai itaji Moyo wa Feisal, Moyo ubakie kusukuma damu anachotakiwa ni kuwajibika kwenye mkataba wake.

Feisal analipwa na klabu hachezi Bure, angekua anacheza bila kulipwa, hoja ya kucheza Kwa Moyo ingekua na mashiko.

Huu mkataba Feisal angefanikiwa ku
uvunja Kwa namna alivyo fanya, kwanza Dunia ingetuona watu wa ajabusana na ingeanzisha migogoro mingi baina ya wachezaji na klabu na wachezaji wangekua wakitumia reference ya mgogoro huu.

Kwa namna alivyo fanya Feisal ata aende CAS hatoboi, sanasana utakua ni mwendelezo wa Wanasheria wake kujitafunia pesa za Yusufu Bakresa.

Yusufu ambaye ndie yuko nyuma ya sakata hili, na Mimi nawashauri Wanasheria endeleeni kuzitafuna izo fedha msiwe na huruma hata kidogo, izo ni fedha zetu za matokeo ya kukwepa Kodi Serikalini Sasa zinampa jeuri.

Mwambie kule CAS mtafanya namna mtashinda iyo kesi Ili kuendelea ku utafuna uo mgodi wa fedha.
Kwani lazima tujadiline na Hali Mimi sitaki kuchezea Timu yako?? Mimi sitaki nachofanya ni kukupa taarifa tu
 
Kwani lazima tujadiline na Hali Mimi sitaki kuchezea Timu yako?? Mimi sitaki nachofanya ni kukupa taarifa tu
Wajinga wengi nchi hii, una sign mkataba, unachukua mshahara harafu unasema hautaki ? umeishia darasa la ngapi wewe?
 
N
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
Kuna mdau aliweka JF mkataba wa Feikubwa alieota mapembe kipengele Cha kulipa tozo ya usajili na mishahara Mitatu kimesema kukiwa na "sababu ya maana" ndo afanye hivyo

1. Sababu za maana za kuvunja mkataba hazikuanishwa Katika huo mkataba hiyo inawapa Yanga na TFF loophole ya Kisheria ya kukataa sababu yoyote ya Feikubwa kwa kusema si ya maana kwa kutaja sababu za maana kama kuwekwa benchi, kutolipwa mishahara au kutotibiwa akiumia!

Pia

2. Feikubwa hakutaja sababu ya maana ya kuvunja mkataba ye kapiga shisha kisha kaweka mzigo mezani na kutimka Dubai mara ndondo kapu JKu!

Feitoto Yuko kifungoni Utopolo hadi akae mezani tutoe dau lake ambalo ni 1 billion!

Yanga si kama Makolo fc. Yanga Ina mawakili wasomi wa kubana wachezaji wanaorubuniwa na Simba wanaokufa kwa kihoro na wivu kwakuwa tu Sasa Yanga ni unbeaten team, tunaongoza ligi , tunacheza makundi shirikisho, tuna mchezaji hatari Mayele , tuna kipa Diarra anadaka mishale, mabomu, makombora, mawe, kombeo , manati na tuna makombe yote kasoro mapinduzi tu ambalo tumewaachia mikia Simba na wameshindwa kulibeba!

Kesi imefungwa!
 
Mpira wa Kiswahili,mwacheni Feisal akacheze popote msimbanie wait.
 
Back
Top Bottom