Kamati ya hadhi ya wachezaji imeshindwa kuamua kesi ya Fei Toto

ni kweli hakuna mkataba usiovunjika duniani lkn haijawai kutokea mtu akavunja mkataba kwa namna feisal alivyovunja,dogo ataondoka yanga kwa signing fee yeye na vilaza wenzie waliomrubuni wajiandae kwa hilo ila sio kwa kuvunja mkataba...
 
Mtu ameshaonesha jeuri alafu bado mnamng'ang'ania wa nini?
Mwacheni aende atakako!
 
Hakuna mahali popote kwenye mkataba wa Feisal panapotamka suala la kukaa mezani kuzungumza kwanza ikiwa Feisal atataka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama za mkataba wake.

TFF ni wajinga na wapuuzi.
Nilikuwa nashangaa watetezi wa100 kumbe ni vilaza hivi!
 
Mmejaa ujinga mwingi sana, kama mambo yangekuwa mepesi kama mnavyojaribu kujidanganya, hao TFF na Kamati yake wasingepoteza muda ili kuwabeba, utetezi wenu kwenye hii issue ni ujinga mtupu.
Kwenye hii case nyinyi mnahusika kama nani?
 
Umeandika kwa hisia tu , hujaweka Facts Matters wala Legal matters.

Umeandika Upumbavu, Sheria hizi zinalinda wachezaji lakini pia zinapaswa zilinde VILABU .
 
ALIUSAINI AMA LAH...

Kkabu inafanya biashara pia, siyo kituo cha kulelea Yatima mzee
 
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
Vipi kama wachezaji wote kwa timu wakifanya hivyo katikati ya msimu.Kila siku anaamka mmoja anaweka hela kwa account anasepa(bila majadiliano yoyote na timu).Mwisho wa mwezi timu inabaki na kocha pekee...vipi hapo watakuww wamevunja mkataba kwa halali?
 
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
Wewe ni kiazi asee!!, Hata mikataba ya kawaida tu mfanyakazi lazima umuarifu Boss wako kabla ya miezi mitatu... Tz tunawajuaji wahovyo sana..
 
Unayemweleza hajui hata maana ya mkataba. Kajaa ushabiki na bendera fuata upepo. Mwenye akili timamu hawezi kusema mtumishi anaweza kuacha kazi bila kumjulisha mwajiri.
 
Kwani lazima tujadiline na Hali Mimi sitaki kuchezea Timu yako?? Mimi sitaki nachofanya ni kukupa taarifa tu
 
Kwani lazima tujadiline na Hali Mimi sitaki kuchezea Timu yako?? Mimi sitaki nachofanya ni kukupa taarifa tu
Wajinga wengi nchi hii, una sign mkataba, unachukua mshahara harafu unasema hautaki ? umeishia darasa la ngapi wewe?
 
N
Umeandika upuuzi mtupu.

Mtu anapotaka kuvunja mkataba kwa kulipa gharama ya uamuzi wake huo kunakuwa hakuna sababu tena ya kukaa mezani, mkataba wenyewe unajieleza.
Kuna mdau aliweka JF mkataba wa Feikubwa alieota mapembe kipengele Cha kulipa tozo ya usajili na mishahara Mitatu kimesema kukiwa na "sababu ya maana" ndo afanye hivyo

1. Sababu za maana za kuvunja mkataba hazikuanishwa Katika huo mkataba hiyo inawapa Yanga na TFF loophole ya Kisheria ya kukataa sababu yoyote ya Feikubwa kwa kusema si ya maana kwa kutaja sababu za maana kama kuwekwa benchi, kutolipwa mishahara au kutotibiwa akiumia!

Pia

2. Feikubwa hakutaja sababu ya maana ya kuvunja mkataba ye kapiga shisha kisha kaweka mzigo mezani na kutimka Dubai mara ndondo kapu JKu!

Feitoto Yuko kifungoni Utopolo hadi akae mezani tutoe dau lake ambalo ni 1 billion!

Yanga si kama Makolo fc. Yanga Ina mawakili wasomi wa kubana wachezaji wanaorubuniwa na Simba wanaokufa kwa kihoro na wivu kwakuwa tu Sasa Yanga ni unbeaten team, tunaongoza ligi , tunacheza makundi shirikisho, tuna mchezaji hatari Mayele , tuna kipa Diarra anadaka mishale, mabomu, makombora, mawe, kombeo , manati na tuna makombe yote kasoro mapinduzi tu ambalo tumewaachia mikia Simba na wameshindwa kulibeba!

Kesi imefungwa!
 
Mpira wa Kiswahili,mwacheni Feisal akacheze popote msimbanie wait.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…