Mwanzoni mwa mwezi huu wa January wizara ya michezo na ilitangaza kamati ya hamasa Kwa ajili ya kuhamasisha mashabiki kuishangilia taifa stars.
Watu mbalimbali akiwemo Joti, Mwijaku, Baba levo, Eng Hersi n.k waliteuliwa lakini Cha kushangaza haieleweki hii kamati hizo hamasa inafanyia wapi!
Hivi Sasa taifa stars ipo Ivory coast inashiriki mashindano ya kumtafuta bingwa wa Africa ila haieleweki Hersi na wenzake akina Mwijaku hamasa wanafanyia wapi, maana hata kusikia wakizungumzia timu ya taifa hicho kitu hakionekana wala kusikika!
Hii nchi ukiwa mwepesi wa Kucheka unaweza kupasuka Mbavu , Yaani Wahuni ndio wanaoteuliwa eti kwenye kuhamasisha timu ya Taifa . Kwenye kikosi hicho yumo Mwijaku aliyeshindwa kutimiza ahadi yake ya kutembea uchi ikiwa timu yake ingefungwa. --- Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas...
www.jamiiforums.com
Hebu wizara na wadau wengine wanajua hii kamati ilipo watuambie!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.