Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Rais Samia Suluhu Hassan atapokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai.
======
Kamati ya kuandaa mkakati wa kutekeleza Tume ya Haki Jinai, imekabidhi mkakati wa kutekeleza mapendekezo ya tume huku ikibainisha mafanikio kadhaa yaliyopatikana.
Akiwasilisha taarifa mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan jana Ikulu ya Chamwino, Makamu Mwenyekiti wa kamati, Balozi Ombeni Sefue alisema mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi kutoa waraka namba 1 wa mwaka 2023 unaowaelekeza wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuzingatia ipasavyo matumizi sahihi ya sheria inayowapa mamalaka ya ukamataji.
Alisema waraka huo unalenga kutafuta dawa ya malalamiko ya wananchi kuwa wakati mwingine mamlaka haya yanatumika vibaya kinyume na lengo na kinyume na sheria.
“Waraka huo pia umebainisha kuwa iwapo mwathirika wa maamuzi ya kukamatwa atafungua shauri mahakamani na ikibainika kiongozi alikiuka sheria wakati wa kukamata, kiongozi huyo atawajibika yeye mwenyewe na serikali haitakuwa sehemu ya shauri litakalotokana na ukiukwaji huo wa sheria,” alisema.
Balozi Sefue alisema mifumo ya Tehama imeunganishwa katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mahakama na Jeshi la Polisi hatua ambayo imeongeza ufanisi na uwazi katika kushughulikia makosa ya jinai.