Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Tamaduni na Michezo, yasema kufika mwezi April ukarabati uwanja wa Mkapa uwe umekamilika

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Tamaduni na Michezo, yasema kufika mwezi April ukarabati uwanja wa Mkapa uwe umekamilika

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
"Bunge linaazimia kwamba Serikali ihakikishe inakarabati uwanja wa Benjamin Mkapa ifikapo April 2025, Serikali iandae mikakati ya kuanzisha chombo maaulumu cha kusimamia uwanja wa Benjamin Mkapa na viwanja vingine vinavyojengwa na Serikali ili kuhakikisha kuwa vinatunzwa na vinakuwa katika ubora wa Kimataifa"

"Serikali iweke utaratibu wa sehemu ya makusanyo ya uwanja kubaki kwa matumizi ya uwanja ili kurahisisha matengenezo ya dharula zinazoweza kujitokeza, na serikali iandae mkakati wa kuboresha viwanja vingine vya michezo ili kupunguza mzigo wa matumizi makubwa kwa uwanja wa Benjamin Mkapa"

Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Elimu, Tamaduni na Michezo, Husna Sekiboko akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kwa mwaka 2024/2025 leo Bungeni.
Screenshot 2025-02-11 142355.png
 
"Bunge linaazimia kwamba Serikali ihakikishe inakarabati uwanja wa Benjamin Mkapa ifikapo April 2025,
Nadhani mleta mada umenukuhu vibaya. Taarifa inasema "Serikali ihakikishe inakarabati uwanja ifikapo April 2025". Haisemi wala sidhani kama inamaanisha hiyo kamati imeamuru ukarabati uwe umekamilika ifikapo April 2025.

Kwa nini hiyo kamati isihoji ni lini viwanja vya umma vilivyochukuliwa na CCM vitarudishwa serikalini? Sasa hivi pesa za serikali zimepelekwa kukarabati viwanja vilivyo chini ya CCM bila ya utaratibu ulio wao.

Kuhusu hilo wazo la chombo maalumu kusimamia viwanja vyote, hilo wazo niliwahi kulitoa zamani sana.
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imetoa agizo kwa serikali kuhakikisha ukarabati wa uwanja wa Benjamin Mkapa unakamilika ifikapo Aprili 2025, ili uweze kukidhi viwango vya kimataifa kwa ajili ya mashindano ya Chan 2024 na Afcon 2027.

Azimio hili limetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Husna Sekiboko, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati hiyo kwa mwaka wa fedha 2024 hadi 2025, katika kikao cha Bunge kilichofanyika leo Februari 11, 2025 jijini Dodoma.

Katika hatua nyingine, Sekiboko ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongezea bajeti wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Habari, Utamaduni na Michezo, jambo lililosaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi mingi kwa ufanisi.

Hata hivyo Sekiboko, ameiomba serikali kuhakikisha inatekeleza miradi inayoendelea kwa wakati ili kuleta maendeleo ya haraka kwa Taifa na Jamii kwa ujumla.

Fainali za Chan 2024 zilikuwa zifanyike kuanzia Februari Mosi hadi Februari 28 mwaka huu lakini kamati ya utendaji ya Caf iliamua kuzisogeza mbele hadi Agosti mwaka huu.

Taarifa ambayo ilitolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) ilisema kuwa fainali hizo zilisogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa maandalizi yake.
 
Back
Top Bottom