DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ado Shaibu Ado, alipozungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge, Dodoma, tarehe 4 Agosti 2026. Amesema kuwa mahojiano hayo yalianza tarehe 3 Agosti 2026 na yataendelea kwa muda wa wiki tatu, huku awamu ya pili ikitarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2026.
- Kushughulikia maoni yote ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu matumizi ya fedha za Serikali za Mitaa yaliyowasilishwa katika taarifa zake;
- Kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ili kuondoa matatizo yaliyojitokeza;
- Kutoa mapendekezo na ushauri kwa Serikali kuhusu hatua za kuboresha usimamizi na matumizi ya fedha za umma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Aidha, Ado amesema kuwa kupitia mahojiano hayo, Kamati itatoa maelekezo ya papo kwa papo kwa Maafisa Masuuli kuhusu utekelezaji wa hoja za ukaguzi na hatua za kuzirekebisha. Vilevile, baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa taarifa zote, Kamati itawasilisha mapendekezo yake kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili hatua stahiki zichukuliwe.
Akizitaja Halmashauri zitakazohojiwa katika awamu hii, Ado amesema kuwa ni:
- Mkoa wa Singida: Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
- Mkoa wa Kigoma: Halmashauri ya Mji Kasulu, Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza.
- Mkoa wa Tabora: Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua.
- Mkoa wa Pwani: Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.
- Mkoa wa Dar es Salaam: Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
- Mkoa wa Lindi: Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na Halmashauri ya Wilaya ya Liwale.
- Mkoa wa Shinyanga: Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu na Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
- Mkoa wa Geita: Halmashauri ya Manispaa ya Geita, Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe na Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
- Mkoa wa Mara: Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
- Mkoa wa Songwe: Halmashauri ya Mji Tunduma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.
- Mkoa wa Rukwa: Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.
- Mkoa wa Ruvuma: Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
- Mkoa wa Tanga: Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
- Mkoa wa Kilimanjaro: Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, Halmashauri ya Wilaya ya Same na Halmashauri ya Wilaya ya Moshi.
- Mkoa wa Manyara: Halmashauri ya Mji Babati na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’.
Ado amesisitiza kuwa lengo la zoezi hilo si kutafuta makosa pekee, bali kuhakikisha hoja za ukaguzi zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu, kuimarisha uwajibikaji, kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha za umma na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.