Kamati ya Maadili piga spana, kanuni hazina jicho la msamaha

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Mhamasishaji wa Yanga SC amekubali makosa aliyofanya kwa Rais wa TFF Ndugu WALLACE KARIA na kusema alienda kumuomba msamaha nyumbani kwake huku wakinywa juice.

Baada ya kukana hadharani kwamba hakukuwa na ugomvi kati yao, hatimaye amekubali kwamba kulikuwa na ugomvi na kwamba alimtafuta kumuomba radhi kwa kumkosea adabu mbele ya halaiki.

Nimetamani hii ndiyo ingekuwa mwisho wa hata kesi ya maadili inayomkabili mhamasishaji.

Lakini sasa utaratibu ndo unazuia hili jambo kuwa limemalizika kwa kuomba msamaha. Kanuni za maadili haziombwi msamaha na ukizingatia maadili yamevunjwa kumuendea Rais TFF na sio Wallace Karia. Rais wa TFF aliyekuwa mkuu wa protokali siku hiyo kiwanjani pale Arusha.

Kiti au Mamlaka ndiyo yemekosewa maadili na sio mtu. Kwahiyo kimsingi hata kamati ya maadili sidhani kama ina kazi kubwa kutafuta ushahidi kwakuwa mwenyewe kashakubali na kuomba msamaha hadharani akikili kukosea.

Kwa ufahamu wangu kamati ya maadili ni kamati huru ambayo haiingiliwi na mtu yoyote hata Rais wa TFF ambaye anaiteua.

Kwahiyo msamaha wa Karia kwa mhamasishaji kama ameutoa hauna la kufanya na kesi yake kwenye kamati.

Kazi ya kamati ni kuhakikisha maadili yanafatwa kwa kuhukumu ipasavyo wale wanaokiuka kanuni.

Kuna wengi wamehukumiwa na kamati hii na sasa wanatumikia hukumu zao. Wengi wao hawakuwa na nafasi ya kuongea na wakubwa na kunywa nao juice wakiomba msamaha.

Kwa namna yoyote ile watakuwa wanaifatilia hii kuona nini kitaendelea baada ya msamaha. Mvuto umekuwa mkubwa zaidi baada ya mtuhumiwa kuomba radhi na kukiri hadharani makosa yake.

Kuna mtego mkubwa kwa kamati na uongozi wa TFF kwenye jambo hili. Kuna dhana ya baadhi ya watu kuwa hawagusiki kwenye mpira wetu na kuwafanya wajione wakubwa wenye haki kuliko wengine.

Hili linaweza kuleta tafsiri mbaya kwenye uongozi unaofuata taratibu kama wa TFF hii ya Rais Wallace Karia.

NB: Sikuja mjini kujuana na watu, mtu mwenyewe wa kujuana nae nani?

BIN KAZUMARI (The voice of the voiceless)

My Take
Kama msahama utaharibu maamuzi basi nyinyi na Manara wote ni watu wa hovyo na mnalea upuuzi kwenye soka
 
Hoja ya mwanzo ya Bin Kazumari ni kuwa Manara alitoa matusi. Sasa ni wapi Manara kakiri kumtukana Karia?

Manara amekiri kujibizana na Karia. Tena kasema yeye ndiye aliyeanzwa. Daaaah sijui mnataka nini kwa Manara
 
Huyo hana tofauti na Mzee wa kongwa.
Yani anaomba msamaha huku akijitetea, nadhani mda utatuambia lakini awamu hii hachomoki
 
Manara atleast apewe miaka minne ya kutojihusisha na mpira ili akajifunze kufanya kazi bila mihemko.
 
All in all, Karia ndiye aliyeanza kumprovoke Manara, kwa kujua or kutokujua Manara angereact vipi, yawezekana ilikuwa ni kiutani, ila mwenzake akachukulia serious, majibizano yakafanyika.

Manara katumia busara kwenda kuomba msamaha hewa, maana hakukosea chochote (as long as he was provoked first).

Huyo Karia kama ana busara usingemuona anabishana na mtu vile.

Kwakujua kabisa nia ya TFF ni nini, Manala kaamua jishusha chini yaishe, na Karia nae kwa kujua kabisa kwamba alimkosea mwenzake, nae amekubali msamaha hewa, akijua akihitajika toa utetezi wake kwenye kamati ya maadili ataonekana wa ovyo.
 
Hoja ya mwanzo ya Bin Kazumari ni kuwa Manara alitoa matusi. Sasa ni wapi Manara kakiri kumtukana Karia?

Manara amekiri kujibizana na Karia. Tena kasema yeye ndiye aliyeanzwa. Daaaah sijui mnataka nini kwa Manara
Wanadhani Manara akifungiwa Yanga haitakusanya makombe tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…