Kamati ya Maadili ya CCM: Kangaroo court

Nia ya uzi mrefu hivi kwa mambo ya ndani ya chama ambacho hukipendi na sio chako Ni nini hasa? Jitahidi kuandika sera na mambo ya chama chako. Mana hao CCM wanao utaratibu wao kama nyie mlivyo na utaratibu wa kutokuwa na ukomo wa uongozi chamani kwenu kwa kisingizio cha „ Mwamba tuvushe“.

Mnaonekana mko frustrated sana na mambo yasiyowahusu. Sasa mko tayari hata kutetea ujinga Mradi ndo upinzani. Pole sana mkuu. Kama ya Mbowe mnasema yasiingiliwe na you are right then kuwa na msimamo. Usiwe kama Chura Huelewi umekaa. Umechuchuma au umepiga Msamba.
Yaani ukiichakuwa hii jforum utapa asilimia 90% za wanaccm wanaohoji ya chadema kana kwamba niwahusika jee wao yanawahusu. Wacha tujadili kakeee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa sipendi kujibu hoja za mawazo mfu lakini goja nichangie

Japo wewe sio mwanachama wa CCM ( predictions) bado una maoni yako kwa hiko chama kama ulichokifanya

Sitaki kuingia ndani sana lakini goja nikudokeze tu, kamuulize Bernard Membe namna chombo nyeti kinavyofanya kazi, kama kutakuwa na kosa kisheria kama ulivyobwabwaja humu then atakachokujibu utupe mrejesho, kwa uelewa wangu linapofikia suala la Kiusalama, kuna utaratibu wake wa kuchukua hatua! CCM ni chama kilichopo madarakani, CCM ndio usalama na kwa maana hiyo akiyetukanwa kwenye zile clips ni kiongozi na mkuu wa nchi,hii haina haja kuifafanua sana, nje ya Rais masuala yote ya Kiusalama huweza kushughulikiwa kwa muktadha na mtazamo mpana!

Kinachoangaliwa hapa ni authenticity ya mashtaka hayo, kitendo klichofanywa na watuhumiwa ni cha kiusalama ndio maana wameitwa na chombo hicho, kosa lile ni la uhaini tatizo letu ni siasa tu but hata kama umedai hawakuwa na lengo la ile habari haikuwa for the public consumption, lakini si ukweli unaweza kuthibitisha kuwa walifanya hicho kitendo? Je public consumption tunaiangalia katika dhana ipi? Kama sita wale ama the big three wangeweza ku expose au leak ile taarifa unajua ni kwa watu wangapi ingekuwa consumed?

Chama chochote cha siasa kina utaratibu wake, japo inapofikia kwa umma hata asiye mwanachama huwa mchambuzi mzuri na zaidi hutoa maelekezo kana kwamba anayajua ya ndani mwe; huwezi sema they did so not with the intention of spreading the message to the public, haijalishi na kwa namna gani umefanya kosa kama hilo ukawa defensive kwa nadharia hiyo, ndio maana kuna Cyber crimes but all in all serikali inamkono mrefu na kwa sasa CCM ndio serikali

Tuache chama kiamue kwa wanachama wake

Tusiwe na viherehere vya kuchambua ya ngoswe tumpe mwenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba kosa ni la uhaini, alitaka kuipindua nchi????
 
Treason si wapelekwe mahakamani, tangu treason inapelekwa CCM?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu wito wa kuwadhalilidha wazee haukuwa na maana yoyote, haya mambo yalishapoa haikuwa busara kuanza kuyachokonoa hasa ukizingatia wazee wameonewa sana kudukuliwa mazungumzo yao ya private
 
Nia ya uzi mrefu hivi kwa mambo ya ndani ya chama ambacho hukipendi na sio chako Ni nini hasa? Jitahidi kuandika sera na mambo ya chama chako. Mana hao CCM wanao utaratibu wao kama nyie mlivyo na utaratibu wa kutokuwa na ukomo wa uongozi chamani kwenu kwa kisingizio cha „ Mwamba tuvushe“.

Mnaonekana mko frustrated sana na mambo yasiyowahusu. Sasa mko tayari hata kutetea ujinga Mradi ndo upinzani. Pole sana mkuu. Kama ya Mbowe mnasema yasiingiliwe na you are right then kuwa na msimamo. Usiwe kama Chura Huelewi umekaa. Umechuchuma au umepiga Msamba.
Mijadala ya kisomi haiangalii uko mrengo gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama hatukubaliani na andiko lake refu lakini ukweli ni kwamba amejitahidi kujenga hoja,,kwahiyo tujibu hoja,hakuna sababu ya kumshambulia au kumtukana,kufanya hivyo ni kupungukiwa busara.Hoja inajibiwa kwa hoja,sio matusi.
 
Wito wao deadline ni lini.Toka lini majadiliano ya faragha yakaitikiwa wito
 
Kuna makosa ya msingi sana kikao kilichoamua kuwapeleka wazee akina Makamba, Kinana na Membe kwenye kamati ya maadili.

1. Wajumbe wa kikao cha maadili wameshatoa hukumu yao.

Katibu mkuu wa CCM ambaye ni mjumbe wa kamati ya maadili ameshasikika tangu zile sauti zilizodukuliwa zilipovuja akitoa hukumu yake, alisikika akibeza yaliyozungumzwa mle huku akiwaita wazungumzaji wale kuwa ni Wapumbavu wa mwaka.

Katika hali kama hii ambapo mshitaki ana maamuzi tayari haki itatendeka vipi?

2. Ushahidi wa kuwashitaki Wazee umebase katika kuingilia faragha zao na udukuzi kinyume cha sheria

Mazungumzo ya Wazee wetu hayakuwa kwa ajili ya public consumption.

Wazee wale faragha zao ziliingiliwa kinyume cha katiba ya nchi na sheria za nchi.

Sidhani kama chama kinachoongoza nchi na kinachotakiwa kulinda na kutetea katiba na sheria za nchi kinaweza kuanza kwenda rogue kudukuadukua au kutegemea udukuzi wa kinyume cha sheria ili kutoa maamuzi dhidi ya wanachama wake.

Ushahidi unaopatikana kwa kuvunja sheria siyo ushahidi at all.

3. Huwezi kumuita Membe bila kumuita pia aliyekuwa akizungumza naye

Kama Membe alitenda kosa, Je huyoaliyekuwa "akiteta" naye kwenye simu hajaitwa kwenye kikao cha maadili? Au Shida yenu ni Membe?

4. Mshitaki kwenye hiyo kamati ya maadili ni nani?

Je ni CCM inashitaki kwaniaba ya Mwenyekiti au Mwenyekiti anashitaki chamani kuvunjiwa heshima?

Kama ni Mwenyekiti mbona Mwenyekiti alitoa kauli mwezi septemba kuwa ameamua kukaa kimya hilo suala asilipeleke kwenye kamati ya maadili, Je mwenyekiti leo kawa kigeugeu? amekuwa na ndimi mbili?

Na kama siye yeye yaani Mwenyekiti kwenda kushitaki kwa kudhani katendewa kosa, ni nani kashitaki? Kwa kuathiriwa vipi huyo aliyeshitaki yeye binafsi hadi ashitaki?

Na kama ni chama ndicho kinashitaki sasa kamati ya chama ya maadili itakwendaje kinyume na chama chenyewe?

5. Hukumu imeshatoka

Kama unasema akina Nape, Makamba mdogo walikosa ila wamesamehewa baada ya Kamati ya maadili kukubaliana na msamaha wa Mwenyekiti.

Ina maana tayari hata wazee waliokuwa wakiongea kwenye simu na hao vijana kamati imeshawaona na Makosa isipokuwa tu "hawajapata msamaha wa Mwenyekiti".

Bashiru alisema, Kusamehewa na Rais Magufuli siyo hoja ya shauri kutofikishwa kwenye kamati ya maadili, lakini Bashiru huyohuyo hakutwambia kuwa Msamaha wa Mwenyekiti sio hoja ya maamuzi ya kikao cha kamati ya maadili, lakini kikao cha maadili kimechukua msamaha wa Mwenyekiti kuwa ni uamuzi wa kikao hicho kwamba sasa vijana wale wasamehewe.

Je ina maana kikao hicho cha maadili kinafanya kazi kwa huruma ya mwenyekiti na hii maana yake maadamu wazee wale hawajapewa msamaha wa mwenyekiti basi hicho kikao kinakwenda kushughulika nao.

Huu ni utaratibu wa ajabu kweli wa utendaji haki ndani ya chama.

HITIMISHO
1. Hili zoezi la kuwaita wazee kwenye kikao cha maadili ni udhalilishaji mwingine kwa hawa wazee.

Yaani kwanza walizushiwa mambo mengi na mwanachama wa CCM aitwaye Musiba walikaa kimya kwa muda mrefu.

Wakajiribu kutafuta haki kupitia baraza la wazee, sauti zao zikadukuliwa, na leo wanadhalilishwa tena kwa kuitwa kwenye kikao cha maadili.

2. Mshitaki hajulikani
Kama ni Mwenyekiti ndiye anayeshitaki kwa kudhani ametendewa mabaya na wale wazee, aseme.

Lakini hata akisema leo ni tofauti na kauli yake ya September ya kuwa aliamua kukaa kimya ili hayo mambo yasiende huko mbali. Sasa je ni nani anashadadia haya mambo, je ni katibu mkuu, au ni nani?

3. Badala ya kuponya hili suala linatibua vidonda, makovu na maumivu

Chama kinahitaji umoja, watu wameumizana kwa namna moja au nyingine, ilihitajika healing process badala ya kutunishiana misuli katika kipindi hiki.

Chama leo kipo hapa sababu kila mwanachama, awaye madarakani au nje ya madaraka amevuja jasho kwa ajili ya chama hiki.

Walioko madarakani leo, wajue miaka mitano iliyopita kuna watu walipambana ili waingie washike usukani katika spirit ya chama.

Fikiria katibu mkuu aliyetumikia chama, akawa amechoka anaomba astaafu, anabembelezwa aendelee, anawaomba jamani niacheni nipumzike, lakini bado tu wanang'ang'ania aendelee kubeba mzigo.

Huyu kweli unaweza kumburuza huko kwenye vikao vya maadili tena kwa kumdukua?

4. This is Kangaroo court
Wanaoshitaki kwa niaba ya Mwenyekiti miongoni mwao ni wajumbe wa kamati ya maadili, yaani washitaki ni haohao na watoa hukumu ni haohao. Hakuna haki hapo, hii ni Kangaroo court.

A party that can for dubious reasons crucify its own comrades who fought and bleed for it is no longer a political party, It is a monster. It can do anything to anybody without bating an eye!
Ila hii hadithi inawahusu nyinyi kwa nyinyi. Inayotuhusu sisi ni tume huru na katiba mpya!
 
Huwa sipendi kujibu hoja za mawazo mfu lakini goja nichangie

Japo wewe sio mwanachama wa CCM ( predictions) bado una maoni yako kwa hiko chama kama ulichokifanya

Sitaki kuingia ndani sana lakini goja nikudokeze tu, kamuulize Bernard Membe namna chombo nyeti kinavyofanya kazi, kama kutakuwa na kosa kisheria kama ulivyobwabwaja humu then atakachokujibu utupe mrejesho, kwa uelewa wangu linapofikia suala la Kiusalama, kuna utaratibu wake wa kuchukua hatua! CCM ni chama kilichopo madarakani, CCM ndio usalama na kwa maana hiyo akiyetukanwa kwenye zile clips ni kiongozi na mkuu wa nchi,hii haina haja kuifafanua sana, nje ya Rais masuala yote ya Kiusalama huweza kushughulikiwa kwa muktadha na mtazamo mpana!

Kinachoangaliwa hapa ni authenticity ya mashtaka hayo, kitendo klichofanywa na watuhumiwa ni cha kiusalama ndio maana wameitwa na chombo hicho, kosa lile ni la uhaini tatizo letu ni siasa tu but hata kama umedai hawakuwa na lengo la ile habari haikuwa for the public consumption, lakini si ukweli unaweza kuthibitisha kuwa walifanya hicho kitendo? Je public consumption tunaiangalia katika dhana ipi? Kama sita wale ama the big three wangeweza ku expose au leak ile taarifa unajua ni kwa watu wangapi ingekuwa consumed?

Chama chochote cha siasa kina utaratibu wake, japo inapofikia kwa umma hata asiye mwanachama huwa mchambuzi mzuri na zaidi hutoa maelekezo kana kwamba anayajua ya ndani mwe; huwezi sema they did so not with the intention of spreading the message to the public, haijalishi na kwa namna gani umefanya kosa kama hilo ukawa defensive kwa nadharia hiyo, ndio maana kuna Cyber crimes but all in all serikali inamkono mrefu na kwa sasa CCM ndio serikali

Tuache chama kiamue kwa wanachama wake

Tusiwe na viherehere vya kuchambua ya ngoswe tumpe mwenyewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh! Hata wewe mpenda ukweli huu ndio msimamo wako?
Kweli mtu ka Kinana aliyepigana 2015 kwa kiasi kile kuhakikisha watu wanaingia madarakani na kwa uchovu akaomba apumzike na Mara mbili nzima mnamkatalia Leo mnamdukua kinyume cha sheria na kuokota neno mojatuu "mshamba" basi mnalisimamia kumdhalilisha?
Jee kweli ni maamuzi ya Chama chake Kinana (CCM) au chama cha Mwenyekiti ( Chama cha Magufuli)?
Lucas philipo jaribu kuangalia ukweli mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom