Kamati ya Maadili yajifungia kupitia mafaili wataka urais Zanzibar

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ratiba za chama hicho.

Kamati hiyo ina jukumu la kupitia fomu ya kila mgombea kabla Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM upande wa Zanzibar haijakaa vikao vyake leo vitakavyohitimishwa kesho chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein.

Gazeti hili jana lilipiga kambi ofisi za CCM Kisiwandui mjini Unguja, ambako lilishuhudia baadhi ya wajumbe wakiingia katika kikao hicho na hadi ilipofika saa 10 jioni walikuwa hawajatoka.

Kikao hicho cha Maadili hukaa chini ya uenyekiti wa Makamu Mwenyekiti wa CCM kwa upande wa Zanzibar na kuwa na baadhi ya wajumbe wachache ambao wanahusika na masuala ya maadili na usalama wa chama.

MTANZANIA ilimtafuta Katibu wa Kamati Maalumu wa NEC Zanzibar anayehusika na Idara ya Itikadi na Uenezi, Catherine Peter Nao, ambaye alisema bado vikao vinaendelea na baada ya kukamilika kwa ratiba yote atatoa ufafanuzi.

“Kwa sasa kikao bado kinaendelea cha maadili, ulinzi na usalama, hivyo naomba tusubiri wakimaliza ndio nitakuwa na la kusema, lakini kwa sasa tuvute subira,” alisema Catherine.

Hadi sasa wagombea 31 kati ya 32 wamesharudisha fomu wakisubiri hatima yao kupitia vikao vya chama hicho tawala.

Wengi wa wagombea hao wamerudisha fomu hizo baada ya kukamilisha utaratibu wa chama, ikiwamo kupata wadhamini 250 katika mikoa mitatu ya Zanzibar.

Akizungumza kuhusu kukamilika kwa mchakato huo na hatua inayofuata juzi mjini Unguja, Katibu wa Idara ya Oganaizesheni ya Kamati Maalumu ya NEC CCM Zanzibar, Galos Cassian Nyimbo, alisema kuwa kazi inayofuata ni suala la vikao vya chama tayari kuanza mchujo kwa kupitia kila fomu ya mgombea aliyeomba nafasi hiyo.

Nyimbo alisema kuwa wagombea wengi walifuata utaratibu wa chama, ikiwamo kutokwenda na mbwembwe kama vile ngoma au msafara wa magari.

“Mgombea gani atateuliwa hilo ni uamuzi wa vikao na sote tunajua misingi na mfumo wa CCM katika kupata wagombea. Na tunaamini kwamba hata wangelikuwa 10 ni lazima apatikane mmoja,” alisema Nyimbo.

Kwa mujibu wa ratiba ya CCM hasa kwa upande wa Zanzibar, vikao vya uteuzi vimeanza jana ambapo Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar ilikutana kuanza kupanga ajenda za uteuzi pamoja na kupitia kila fomu ya mgombea kabla vikao vya ngazi ya juu havijafanya maamuzi.

“Julai 3 kitakutana kikao cha Kamati ya Ulinzi, Usalama na Maadili ya chama na Jumamosi Julai 4 (kesho) kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa itakutana hapahapa Kisiwandui.

“Kwa kawaida kikao hiki cha Kamati Maalumu pia hutoa mapendekezo, lakini mwisho wake huishia kwenye vikao vya chama taifa ambavyo vitaanza Julai 9 jijini Dodoma, Makao Makao Makuu ya CCM,” alisema Nyimbo.

Alisema mapendekezo ya Kamati Maalumu yatafikishwa mbele ya kikao cha NEC baada ya kutoa pendekezo la majina yasiyozidi matatu.
 
Back
Top Bottom