Kamati ya masaa 72 yaifuta kadi nyekundu ya Derick Mukombozi

Kamati ya masaa 72 yaifuta kadi nyekundu ya Derick Mukombozi

Wakipekee

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2019
Posts
6,194
Reaction score
10,711
Ligi inazidi kunoga, Kila mtu ashinde anavojua...

Kamati ya Masaa 72 imefuta kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa Namungo, Derick Mukombozi, katika mchezo dhidi ya Simba SC. Uamuzi huu umefikiwa baada ya kamati kupitia kwa kina ripoti ya mwamuzi na kulinganisha na picha za video za tukio husika.

Baada ya uchunguzi, kamati imebaini kuwa maelezo ya mwamuzi hayalingani na kile kilichoonekana kwenye video, hivyo kadi hiyo imeonekana kuwa batili. Kutokana na uamuzi huu, Mukombozi hana hatia yoyote na atakuwa huru kuendelea kuitumikia Namungo kwenye michezo inayofuata.
Screenshot_20250223-102340_1.jpg
 
Mwanzo Mwamuzi huyo Japheth Smarti alidai kua "Alihisi" kua Mkombozi alitoa lugha chafu... Pia alidai "huenda" alimpiga kibao Ateba hivo hakua na namna zaidi ya kumtwanga Kadi nyekundu "umeme" Ili iwe fundisho [emoji23]

Kumbuka pia Mwamuzi huyo Japheth Smarti aliwahi kumalizia mechi kati ya Simba na Coastal Union huku mchezaji wa coastal akiwa kwenye move ya kwenda kufunga goli hali iliyozua taharuki na kupelekea baadhi ya wachezaji kuangua vicheko uwanjani...

Soma hapa... Refa amepiga filimbi ya kumaliza mpira baada ya kuona Simba SC wanataka kufungwa goli nyingine
 
Huyo refa ni kichaa
 
Hali hii imekuwa mazoea, Kamati ya saa 72 inachukua hatua ila wakati huo hatua hizo zinakuwa hazina faida kwani mchezo unakuwa umeshakwisha, Na timu kama Namungo tayari imeshaathirika kwa maamuzi mabovu kabisa ya mwamuzi

Je, Bodi ya Ligi inawanufaisha vipi Namungo fc ambao tayari wameshaathirika kwa kucheza pungufu kwa masaa yote ya mchezo yalitobakia?

Je, Mwamuzi amechùkuliwa hatua gani?

MAONI.
5imba sc wanyang'anywe alama 3 na aidha zigawanywe au zote apewe Namungo fc.

Mwamuzi apewe adhabu kali ikiwemo kufungiwa moja kwa moja, viboko 12 pamoja na kushrakiwa kwa tuhuma za rushwa
 
Back
Top Bottom