Kamati ya nidhamu ya TFF imempiga faini ya milion 5, Afisa habari wa Klabu ya Yanga Jerry Muro

Kamati ya nidhamu ya TFF imempiga faini ya milion 5, Afisa habari wa Klabu ya Yanga Jerry Muro

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,229
Reaction score
610
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF iliyoketi jumanne tarehe 5 Mei, 2015 imempiga faini ya sh. 5,000,00 (milioni tano), Afisa Habari wa klabu ya Yanga SC Jerry Muro kwa kutoa kauli za chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF.

Akitoa utetezi wake mbele ya Kamati ya Nidhamu, Jerry Muro alikiri na kujutia kufanya kosa hilo na kudai ilitokana na ugeni wake katika uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo kamati ilimuepusha na adhabu ya kufungiwa..

Kwa mujibu wa Ibara ya 53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi yake ya Ligi mbele ya umma, kamati imemtoza faini ya sh. 5,000,000 (millioni tano), Jerry Muro na kuwaonya viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu kutojihusisha na vitendo vya matamshi ya aina hiyo.
 
Mmmmmmh! Ngoja Nijiridhishe Na Ulichokiandika Kisha Nitarudi Baadae Kidogo.
 
Nimerudi Tena Na Ukweli Ni Kwamba Hakuna Maamuzi Kama Hayo Yaliyotolewa Ukizingatia Juzi Na Jana Viongozi Wengi Wa TFF Walikwama Na Mikoko Yao Huko Waishipo Kutokana Na Mvua Hizi Kubwa Zinazoendelea Hapa Jijini Dar es Salaam Na Hata Huyo Jenny Murro Jana Siku Nzima Kashinda Tu Anaogelea Pale Jangawani Huku Akitaka Kumuokoa Mzee Ibrahim Akilimali Ambaye Alikuwa Amezama Na Anaelekea KIBRA!
 
Nimesikia Simba wakiwapa Yanga kama wanataka wawahifadhi pamoja na kombe lao kipindi hiki cha mafuriko, basi yanga wawashangilie na kuvaa jezi za Simba kwenye mechi ya Simba ya mwisho
 
Bado manara aropoka mno na sambusa zake
 
Aliwaumbua na akawambia mkithubutu atawaumbua mengi anavideo ufisadi tff muro kiboko polisi wanampa sarut
 
Basi TFF huo mkwanja wanaoupiga kwa vilabu na viongozi wake watumie kukomboa nyasi zilizo bandarini waache kulialia hawana hela wakati wanapiga mkwanja mrefu hasa kwa simba akigoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
 
Muro anaropoka kwenye media ka yupo kijiwe cha kashata na mzee akilimali.mbaya zaidi wabongo wanafiki,Yanga walimwacha tu akashfu
 
Nimerudi Tena Na Ukweli Ni Kwamba Hakuna Maamuzi Kama Hayo Yaliyotolewa Ukizingatia Juzi Na Jana Viongozi Wengi Wa TFF Walikwama Na Mikoko Yao Huko Waishipo Kutokana Na Mvua Hizi Kubwa Zinazoendelea Hapa Jijini Dar es Salaam Na Hata Huyo Jenny Murro Jana Siku Nzima Kashinda Tu Anaogelea Pale Jangawani Huku Akitaka Kumuokoa Mzee Ibrahim Akilimali Ambaye Alikuwa Amezama Na Anaelekea KIBRA!

Mdau umekurupuka. Taarifa za mleta uzi ni sahihi kwa 100%, taarifa za vyombo vyote vya habari vimetoa kwenye vipindi vya michezi
 
Kusema kweli bila unafki napenda watu waropokaji hivyo binafsi nafurahishwa na watu aina ya Muro na Manara bila kumsahau yule msomali aliyekua rais wa simba Rage huyu jamaa ni kiboko namkubali nje ya siasa
 
Nani atalipa hiyo faini yeye mwenyewe au ni yanga
 
Nimesikia Simba wakiwapa Yanga kama wanataka wawahifadhi pamoja na kombe lao kipindi hiki cha mafuriko, basi yanga wawashangilie na kuvaa jezi za Simba kwenye mechi ya Simba ya mwisho

Akha! katu Simba wasilisogelee kombe letu wasije wakaling'ang'ania kwa nguvu wakidai kuwa ni lao, ni miaka mingi sasa wanalitolea udenda bila mafanikio.
 
walopokaji wengine wanaradha kama ukimsikiliza masau bwile au thobias kifaru full kucheka yani kwa mikwala yao..
 
Mdau umekurupuka. Taarifa za mleta uzi ni sahihi kwa 100%, taarifa za vyombo vyote vya habari vimetoa kwenye vipindi vya michezi

Wewe Mwenyewe Pia UMEKURUPUKA Kwani Habari Hii Aliitoa Tokea Mchana Na Hakuweka Source Je Tungeiamini Vipi? Na Wewe Na Ujanja Wako Huu Wa KIPOPOMA Umesubiri Hadi E FM Wametangaza Ktk Kipindi Chao Cha Michezo Cha Saa Moko Usiku Huu Ndiyo Na Wewe Sasa Unaibuka Kunijibu! Huo Ujanja Wako Ni Wa Kizamani Sana Mkuu.
 
Muro anaropoka kwenye media ka yupo kijiwe cha kashata na mzee akilimali.mbaya zaidi wabongo wanafiki,Yanga walimwacha tu akashfu

Wanayanga nliwaulza kati ya Muro na Manara nani mropokaji hawajanjibu hadi leo. Jibu limetolewa na tff basi inatosha
 
Back
Top Bottom