Pre GE2025 Kamati ya Siasa CCM Dodoma mjini waigomea taarifa ya mradi wa ujenzi wa Soko la Zayoni lililopo Nkuhungu

Pre GE2025 Kamati ya Siasa CCM Dodoma mjini waigomea taarifa ya mradi wa ujenzi wa Soko la Zayoni lililopo Nkuhungu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
WAJUMBE wa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Dodoma mjini wameigomea taarifa ya mradi wa ujenzi wa Soko la Zayoni lililopo Kata ya Nkuhungu mkoani Dodoma kwa kudai ina mapungufu kutokana na hali ya kusuasua kwa mradi huo na hivyo kuagiza kuandaliwa kwa taarifa mpya yenye majibu sahihi.

Wajumbe hao wametoa kauli hiyo wakati wakikagua mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 45 wakati wa ziara yao ya ukaguzi wa miradi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025 wilayani wakiongozwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Dodoma, Sophia Kibaba.

Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi amewataka wataalamu wanaosimamia mradi huo kuwa makini na fedha zinazotolewa na Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya wananchi ili kuepuka kuigombanisha serikali na wananchi na kuwaahidi wajumbe hao kwenda kukaa na wataalamu hao kuona namna ya kupatia ufumbuzi suala hilo.

 
Back
Top Bottom