The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Kamati ya Siasa Wilaya ya Chamwino, Dodoma, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chamwino, George Malima, imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2024.
Akikagua miradi hiyo, Malima amesema ameridhishwa na utekelezaji wake kwani miradi yote aliyoipitia imeakisi thamani ya fedha zilizotumika. Pia, ameupongeza uongozi wa serikali wa wilaya hiyo kwa kusimamia vyema miradi ambayo Serikali imeelekeza fedha nyingi ili kupeleka huduma kwa wananchi.
Pia soma Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Miradi iliyotembelewa ina thamani ya takribani shilingi bilioni 4.1, ambayo imegusa sekta ya elimu ya msingi na afya ngazi ya msingi, elimu ya sekondari, barabara, maji na umeme.
Wajumbe wa kamati hiyo nao wameonesha kuridhika na utekelezaji wa miradi hiyo kwenye majimbo yote mawili ya Chamwino na Mvumi. Wameipongeza Serikali kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi hiyo, wakisema imekwenda sambamba na namna Ilani ya CCM (2020-2025) ilivyobainisha.