Ina maana wakina aveva wameshindwa kabisa kuiendesha Simba!!! Na nyie wanachama hawa watu si mmewachagua wenyewe ina maana mlikiwa Hampimi walichokuwa wanaahidi? Kama mmefikia huo uamuzi basi sawa ila mnatakiwa mfanye evaluations na tafiti ya kila kuhusiana na simba na Mali zake ili thamani halisi iwekwe na sio mtu ndo apange kiasi ambacho atawekeza maana hata ukienda sokoni kariakoo muuzaji ndo anapanga bei kwa hiyo ww mnunuzi ndo unaweza kubargain na sio we ndo unapanga bei.
Na hilo swala la tathmini linakuja baada ya kukubaliana ni mabadiliko ya aina gani simba ina kwenda kufanya?
Je ni private company ambayo itanunuliwa na mtu mmoja pekee na wanasimba kubaki kama washabiki tuu kama ilivyo Azam japo haikununuliwa?
Je ni public company kama lengo la Dewiji lilivyo la kununua baadhi ya hisa na wanachama na wewekezaji wengi kuruhusiwa kununua? Japo Dewiji anahitaji kuwanunulia hisa wanachama.
Cha muhimu kwa sasa kama wana hitaji mabadiliko ni kuanza na mabadiliko ya katiba ambayo yataibadili simba kuwa public company au kuwa private company halafu watapeleka mapendekezo hayo TFF.
Pili ni lazima ifanyike tathimini au evaluation ya thamani ya mali za Simba na thamani ya kila mwanachama ndani ya simba ina gharama kiasi gani hapa lazima pande zote zishirikishwe kuanzia TFF, uongozi wa simba , wanachama na wawekezaji.
Pia ni lazima iangaliwe na ipimwe kwa uhalisia wa sasa kulingana na thamani ya simba na hisa na thamani ya hisa watakazo ona hiyo billion 20 ina thamani gani kwa hisa na thamani za hisa?
Bila shaka huu mchakato una hitaji wataalam na wanasheria sio mchakato wa kukurupuka tuu.. Ni wazi lazima watu wakae chini na wapime hayo mambo.
Pia ni lazima watu wajue kuwa Mo ametoa offer ya 20bn lakini simba wanaweza wakapima baada ya utathimini wakamwambia kwa hiyo 51% hatuwezi kukubali labda uongeze kiasi fulani au kwa hiyo 20bn utapewa 48% halafu zilizo baki zitakuwa nafasi kwa wanachama na wawekezaji wengine kununua.
Na katika huu mchakato ni lazima Simba wajisajili kwenye soko la hisa la Dares.-salaam(DSE) ili watu na wengine wanunue hizo hisa..!
Hivyo ni vyema wana simba wakawa na upole maana swala hili linaweza kuchukua mwaka mzima au zaidi kufikia makubaliano mazuri na yamanufaa.
Kwa kipindi hiki Mo anaweza wasaidia kununua wachezaji kama mpenzi wa simba wakati mchakato wa mabadiliko na mazungumzo ukiendelea..
Hapa ugumu unaweza kuwa ni thamani ya hisa na kiasi mtu anacho taka apewe na fedha aliyo nayo pia thamani ya mali za simba kwa sasa.
Ni vyema wana simba wakawa wapole kwa sasa wasitake kuharakisha mambo bila taratibu kufatwa.