Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujilipa posho mil. 438 kwa mwaka

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujilipa posho mil. 438 kwa mwaka

Trump2

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
1,553
Reaction score
2,609
Tarehe 28/10/2017 Kamati ya Utendaji ya TFF, ilifanya Kikao katika Hoteli ya SEA SCAPE Kunduchi Beach jijiji Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine ilipitisha azimio la Wajumbe wa Kamati hiyo kuanza kulipwa posho ya kila mwezi kwa mchanganuo ufuatao:
1. Rais wa TFF Tsh.Mil.6 kwa mwezi sawa na Mil.72 kwa Mwaka.
2. Makamu wa Rais wa TFF, Tsh. mil. 5 kwa mwezi sawa na Mil.60 kwa mwaka.
3. Wajumbe 20 wa Kamati ya Utendaji kila mmoja Tsh. Mil. 1 kwa mwezi sawa na mil.12 kwa mwaka , kwa wajumbe 20 ni Tsh. Mil. 240 kwa mwaka.

NB: Posho hizi ni mpya na hazijawahi kuwepo katika shirikisho hilo katika uongozi uliopita.

Aidha Posho za kila kikao zimepanda kutoka Tsh. 300, 000/= uongozi uliopita hadi laki tano (500,000/) uongozi wa sasa kwa kila mjumbe, kwa mwaka kuna vikao vya kawaida visivyopungua sita, kwa Wajumbe wote 22 kwa mwaka itakuwa mil.66.

Kwa mchanganuo huo, Gharama za Posho tu kwa mwaka kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji tu ni milioni mia nne thelathini na nane (mil.438). Bado posho za vikao vya dharura, posho za watumishi wengine n.k

Moja ya changamoto za maendeleo ya Mpira wa Miguu Tanzania ni Ukosefu wa fedha. Timu zetu za taifa zinashindwa kukaa kambini, Waamuzi wanakosa Mafunzo, viwanja vya michezo vinashindwa kuboreshwa, vilabu vya michezo havisaidiwi na mambo mengine chungu nzima hayafanyiki sababu ya ukosefu wa fedha, leo hii EXCOM inakwenda kujifungia Sea ESCAPE na kuidhinisha mil. 438 kwa ajili kujilipa posho! Kwa mwendo huu tusitegemee maendeleo katika soka Tanzania. Rais wa TFF, WALES KARIA na Makamu wake, MICHAEL WAMBURA wanapaswa kujitathmini upya.
 
Sababu zao za kugombea sasa ni wazi. Kwanza wakatwe kodi. Hayo ni mapato tena makubwa
 
Kwa mpango huu tusitarajie maendeleo ya soka la Tanzania. Bongo kila kitu hovyo hovyo.
Siasa hovyo.
Utawala hovyo.
Afya hovyo.
Elimu hovyo.
Muziki hovyo.
Michezo hovyo.
Katiba na sheria hovyo.
Demokrasia hovyo.
Miundombinu hovyo.
Kila kitu ni hovyo hovyo tu!!!!!!!!!!
 
Nyie mnataka watu wawafanyie kazi km wamisionari?? Milioni 6 kwa Rais unaona hela kubwa hiyo?? Unajua Katibu na secretariati wanalipwa bei gani? Hao wanalipwa na Fifa
 
Mil 6 kwa mwezi kama posho ya Rais unaiona ni nyingi?? wewe utakuwa masikini mkubwa sana
 
Watanzania mna roho mbaya sana na wivu ndo maana mtazidi kuwa masikini.

Mjinga gani atakubali afanye kazi iliyojaa presha km kuongoza mpira wa Bongo bila mshahara na marupurupu ya kueleweka.

Nini thamani ya mateso anayopata Malinzi huko jela na matusi pamoja na dhihaka alizopata akiwa Rais. Kazi zinazoweza kusababisha matokeo km hayo, hulipwa vizuri, ipo hivyo kote duniani.
 
Back
Top Bottom