Kamati ya Zitto kumweka kitimoto gavana wa BoT

Kamati ya Zitto kumweka kitimoto gavana wa BoT

System ya Tanzania ipo kwa ajili ya kuzalisha viongozi na wafanyakazi wezi, majambazi na wabadhilifu wa mali zetu. Zamani tulikuwa tunatafuta wezi na wabadhilifu kati ya raia wema na wazalendo lakini sasa tunatafuta raia waaminifu na wazalendo kati ya mijizi na mibadhilifu inayozalishwa na system hii.
 
Ndullu kisha sema kuwa ana nyumba kama hiyo marekani kama Ballali nae alivyokuwa na nyumba huko huko na kaishia kuzikwa huko!! Sasa inaelekea hawa jamaa hatima ya maisha yao ni huko huko majuu hapa wanakuja kutuibia tu!!

Tatizo la wenzetu ‘waliobahatika’ kuishi/kufanya kazi nje wakirejea nyumbani wanasahau kwamba Tanzania bado ni nchi ya dunia ya tatu. Wanakuja wakiwa na ile kasumba ya maisha ya kifahari/ya juu waliyoishi nje. Matokeo yake ndio hayo tunayoyaona ya akina Ndulu na wengine wa aina yake kudhani kwamba nchi inaweza ku-afford kujenga nyumba za mabilioni kwa ajili ya Mtanzania mmoja ama wawili bila kutilia maanani na bila dhamira zao kuguswa kwamba fedha hizo zingeliweza kuwasaidia Watanzania wengi zaidi kwa kuwapatia huduma za jamii.

Si hivyo tu hata viongozi wa kisiasa, viongozi wa Wizara, Idara, Makampuni Binafsi n.k. hujiona wao wako katika category nyingine kabisa kwa hiyo wako tayari kupanga na kupitisha bajeti kubwa kwa manufaa ya wachache bila kujali na kuangalia wanawezaje kuwasaidia wengine iwapo watapunguza matumizi yasiyo ya lazima ama hata kukubali kupunguziwa mishahara mikubwa wanayojipangia.

Nchi inaweza kuanza kuona mabadiliko pale tu Watanzania walio juu watakapokuwa tayari kuwafikiria na kuchukua maamuzi ya kuwasaidia Watanzania wenzao walio chini.
 
Na Sadick Mtulya
Mwananchi
Januari 19, 2010



KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imepanga keshokutwa kuwa siku ya kumwita gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu ajieleze kuhusu matumizi ya Sh 2.5bilioni kujenga nyumba mbili za kuishi.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na Makamu Mwenyekiti wa POAC, Ester Kilasi zimeeleza kuwa Profesa Ndulu ataitwa katika kamati hiyo baada ya wajumbe wake kufanya ziara eneo la mradi kulikojengwa nyumba hizo.

Kilasi aliliambia gazeti hili jana kuwa ziara hiyo itafanyika kwa siku mbili; leo na kesho.

"POAC imemwita Profesa Ndulu Alhamisi hii (kesho kutwa) ili atupe maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa nyumba anayoishi na za manaibu gavana wake," alisema Kilasi na kuongeza: "Lakini kabla ya kupata maelezo hayo kamati imeamua kufanya ziara ya kuzungukia na kuangalia hali halisi ya mradi wa ujenzi wa nyumba hizo tujiridhishe." alisema.

Habari ambazo Mwananchi imezipata zinasema kwamba Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe ambaye yuko masomoni Ujerumani amelazimika kurudi nchini kusimamia sakata hilo.

Kamati hiyo itakutana na Profesa Ndulu siku chache baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo kuunda kamati ya kuchunguza suala hilo.

Mkulo aliliambia gazeti hili Ijumaa iliyopita kuwa ripoti ya kamati hiyo imekwishawasilishwa kwake na yeye ameanza kuipitia kabla ya kuitoa hadharani.

"Nikitoka hapa ninakwenda kuisoma ripoti niliyoiagiza kuhusu matumizi ya fedha yaliyotumika katika mradi wa ujenzi wa nyumba ya gavana na manaibu gavana," alisema Mkulo na kuongeza:

"Hizi tuhuma ni nzito na zinamhusu mtu nyeti wa serikali, hivyo itachukua muda kidogo kutoa majibu ya ripoti niliyonayo."

Mkulo alifafanua kuwa amechelewa kuitoa ripoti hiyo kutokana na kuhusika kwa vyombo vingine nyeti vya serikali katika uchunguzi wake.

"Nikimaliza kuisoma ripoti hii, nitalazimika nishauriane na washauri wangu na kisha nivishirikishe vyombo vingine nyeti vya serikali," alisema

Kwa mara ya kwanza taarifa ya matumizi ya fedha katika ujenzi wa nyumba hizo ziliripotiwa na gazeti hili, lakini baadaye BoT ilitoa ufafanuzi ikieleza kuwa nyumba hizo zilijengwa baada ya kufuatwa taratibu zote za zabuni.

Kabla BoT kujibu tuhuma hizo, Profesa Ndulu alikiri kutumika kwa kiasi hicho cha fedha, lakini akafafanua kuwa fedha ilitumika kujenga upya nyumba hizo na siyo kuzikarabati.

Nyumba haijakarabatiwa, imejengwa from the ground (kutoka chini)... ni tofauti kukarabati na kujenga nyumba mpya huu, ni upotoshaji wa wazi na kujaribu kuchafua mema, alilalamika gavana huyo.

Ok.ngoja tusubiri tuone!
 
Huu uwajibikaji mbele ya kamati ni mzuri na gavana atajibu maswali. tatizo kwa kamati kama hii ni kutokuwa na meno. Watajadili alafiu wanaishauri serikali. Hatahivyo 2.5 bilion kwa nyumba mbili ni sawa. Tatizo jiingine ni umaskini. Watu wamekuwa maskini kiasi kwamba wanataka gavana aishi kwenye nyuma kama zamanzese
 
"Hizi tuhuma ni nzito na zinamhusu mtu nyeti wa serikali, hivyo itachukua muda kidogo kutoa majibu ya ripoti niliyonayo."

Mkulo alifafanua kuwa amechelewa kuitoa ripoti hiyo kutokana na kuhusika kwa vyombo vingine nyeti vya serikali katika uchunguzi wake.

"Nikimaliza kuisoma ripoti hii, nitalazimika nishauriane na washauri wangu na kisha nivishirikishe vyombo vingine nyeti vya serikali," alisema

kidumu chama cha mapinduzi. sera za kulindana oyee!
 
Gharama ya Kiwanja maeneo mengi inafika 600 Million


Ninakubaliana na wewe kuwa kiwanja kinaweza kuwa na bei ya juu kiasi hicho, japo kwa Dar kwa kweli inatia kichefuchefu.

Lakini wao walikuwa na viwanja tayari kwa hiyo gharama zao ni za vifaa vya ujenzi kama cement, nondo, na vitu vingine ambavyo bei zake sokoni ziko sawa haitegemei unajenga wapi.

1.2 Bilion bado iko juu sana!
 
Amen-na iwe hivyo ili vizazi vijavyo vipate watu wa kuwalaumu kwa kuchelewesha maendeleo!Mmeona huu usultani wanaojenga wa wazazi kuwaachia wana ufalme na himaya za nchi hii?Gavana hawezi kuwa msafi kuliko genge lililompa kazi!Tena Gavana alifanya kazi na Ballali-aliyeneemeka na kudaiwa kurehemika kwa siri!Wote wana nyumba zao nje ya kijiji cha Tz na kwa hiyo hawana njaa kama ninyi meti!TATIZO MTAWAPA TENA SERIKALI KUELEKEA 2015!AIBU KWENU NA MIMI NA DAMU ZETU NI JUU YA VICHWA VYETU.SEMA AIIIIIIIIIIIIIIIIIIMMMMMMMMEEEEEEEEEEEEEEEEEEEENNNNNNNNN!
 
Kama ilivyotarajiwa, hatimaye kamati ya bunge (PAC) imeafiki matumizi ya mabilioni ya fedha ktk ujenzi wa hekalu la Gavana wa BoT, Prof. Nduli...ooops Ndulu na manaibu wake. Binafsi nilitegemea kamati hiyo ingejaribu kufuatilia kwa kina ili kuona uhalisia wa gharama za ujenzi huo lakini kilichotokea ni kukubaliana na maelezo ya Prof. Kwenu wanaJF mnasemaje juu ya hilo.....?
 
kwani hiyo kamati inaongozwa na nani, ? ila nijuacho ni kua taratibu za mkandarasi zilifuatwa, sasa tusubiri tuone CAG atatueleza nini juu ya VALUE FOR MONEY AUDITING . maana hata kama kamati itasema haijajiridhisha hawana ushahidi wakisomi kua kwanini majengo hayo ni aghali, hivyo ni vyema CAG akatoa ripoti yake kisha tuhoji.
 
Kama ilivyotarajiwa, hatimaye kamati ya bunge (PAC) imeafiki matumizi ya mabilioni ya fedha ktk ujenzi wa hekalu la Gavana wa BoT, Prof. Nduli...ooops Ndulu na manaibu wake. Binafsi nilitegemea kamati hiyo ingejaribu kufuatilia kwa kina ili kuona uhalisia wa gharama za ujenzi huo lakini kilichotokea ni kukubaliana na maelezo ya Prof. Kwenu wanaJF mnasemaje juu ya hilo.....?

Laiti kama mnejua madudu yanayofanywa na hizo mnazoziita kamati za Bunge mngepata kichefuchefu.

Kwa kifupi hizi kamati za Bunge huwa ''zina-negotiate'' kabisa kiwango cha pesa ya kupewa na taasisi husika kabla hawajaipitisha ripoti ya taasisi husika! Ni maigizo tu hakuna lolote!
 
why u dont care Mwakijiji ?

because it doesn't matter!

Tulilalamika kuhusu rada wasinunue.. do you remember what they said halafu ikaishi wapi? 50,000,000 USD!
Tulilalamika kuhusu Gulfstream 500 wasinunue unajuwa walisema nini halafu tumeishia wapi? 50,000,000 USD!
Tulilalamika kuhusu Airbus 320 wasinunue mnakumbuka walisema nini? 60,000,000USD!
Tulipigia kelele ujenzi wa Twin Towers za boT, Abt 330,000,000 USD!
Tumepigia kelele wizi wa Kagoda Agriculture 40,000,000USD
..
..
..
..

Sasa tunapigia kelele nyumba mbili, 2,600,000!!!??


Kama hawakusiliza kwenye mambo yanayohusu, 530, 000, 000!! what are the chances that they will be moved by 2.6? NO CHANCE, NYET, NONE, ZERO, TUPU, SIFURI (YENYE MASIKIO)!
 
Mara nyingi tumezoea kusiki viongoz wetu wakitumia fedha zetu vibaya nakushindwa kujielezea hata hvyo Gavana wetu Prof Ndulu ameleta mabadiliko kama sio mapinduzi. Ktk taarifa ya habari iliokuwa ikionyeshwa pitia vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini. Prof Ndulu alionyesha umahiri wake wakujibu hoja nakuwa mkweli maana hata mh Zitto alijikuta akikosa lakusema nakumwachia mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kufanya uchunguz ikiwa kama nikweli kiasi hiko kilitumia kialali ktk ujenzi huo. Kwa maoni yangu Prof amekuwa chachu yawataka maendeleo nakuwa muwazi ktk matumizi ya fedha. God bless Tanzania and God bless Tanzanian people. Amen.
 
Kwa mtazamo wangu ni kuwa wanakamati walishindwa kutafuta the right question. Nina hakika hata huyo mkaguzi mkuu akienda kukagua vitabu hatakuta kosa lolote. Kwa nini? Kwa sababu kwenye bajeti ya BOT, kuna line item inayohusu hizo nyumba kwa cost ya 1.2b, na matumizi yake nayo yamepitia hatua sahihi za PPPR. Swali la msingi, je ni sawa kuweka bajeti ya kiwango hicho kwa ujenzi wa nyumba za/ya mtu mmoja?
 
Mara nyingi tumezoea kusiki viongoz wetu wakitumia fedha zetu vibaya nakushindwa kujielezea hata hvyo Gavana wetu Prof Ndulu ameleta mabadiliko kama sio mapinduzi. Ktk taarifa ya habari iliokuwa ikionyeshwa pitia vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini. Prof Ndulu alionyesha umahiri wake wakujibu hoja nakuwa mkweli maana hata mh Zitto alijikuta akikosa lakusema nakumwachia mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kufanya uchunguz ikiwa kama nikweli kiasi hiko kilitumia kialali ktk ujenzi huo. Kwa maoni yangu Prof amekuwa chachu yawataka maendeleo nakuwa muwazi ktk matumizi ya fedha. God bless Tanzania and God bless Tanzanian people. Amen.
Kamati za wawakilishii wetuuu wengi wao upeo wa mambo ni mdogo na zaidii hupendaa kushabikiaa zaidii kuliko upembuzii yakinifuuuuuuu...UVIVU WA KUFIKIRIIII..

Prof alibase kwenye utaratibuu tuu uliotumika katika kufikia maaamuzii ya ujenzii huooo..hapoo walikosaa maswali ya msingii kwani wajumbe wengi walikuwa wakiongozwaa na hisiaa na media..

Wajumbe wa kamati za bunge wajifunze kusoma sheria na kanuni mbali mbali na wawe na upembuzii yakinifuuuuuuuuu...USHABIKI HAUWAJENGIIII WAO WALA TAIFAA
 
Bwana ametoa bwana ametwaa
jina la bwana libarikiwe
 
Back
Top Bottom