Kamati yafuta adhabu ya Kadi Nyekundu ya Gibril Sillah wa Azam FC, sasa kuwavaa Simba

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania imefuta adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wa Azam FC, Gibril Sillah, katika mchezo namba 034 dhidi ya Kagera Sugar uliomalizika kwa Azam kushinda mabao 2-0.

Uamuzi huo umezingatia Kanuni ya 12:8 ya Usimamizi wa Ligi, baada ya Kamati kujiridhisha kupitia picha jongeo pamoja na taarifa za wataalamu kuwa mchezaji huyo hakustahili kuonyeshwa kadi hiyo.

Wakati huo huo, Kamati imempa Onyo Kali mwamuzi wa akiba wa mchezo huo, Greyson Buchard kutoka Kagera, kutokana na kuonyesha mapungufu ya kiuchezaji yaliyosababishwa na kushindwa kutafsiri vyema sheria za mpira wa miguu. Adhabu hiyo dhidi ya mwamuzi imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 43:1(1.8) inayohusu Udhibiti kwa Waamuzi.
Screenshot 2026-09-04 143522.png
 
Hawakufanya marejeo ya FVS kabla ya kutoa RED CARD?!
 
Hiyo mechi ya Azam vs simba ni lini? Kama naiona vile simba ikienda kuangusha point 2 au 3 kwenye huo mchezo.
 
Back
Top Bottom