Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Kamati nne (4) za Kudumu za Bunge zitaanza kukutana tarehe 10 hadi 30 Oktoba, 2022 Jijini Dodoma. Kamati hizo ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI.
Shughuli zilizopangwa na Kamati za Bunge zinajumuisha maandalizi ya shughuli za Mkutano wa Tisa wa Bunge ambazo zinahusu Miswada minne ya Sheria na Tarifa za Kamati zinazosimamia Matumizi ya Fedha za Umma na Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ambazo ni PAC, LAAC na PIC.
Pamoja na mambo mengine, zinatarajiwa kuwezesha Kamati nane kuandaa Taarifa zitakazowasilishwa Bungeni wakati wa vikao vya Mkutano wa Tisa wa Bunge ikiwemo Uchambuzi wa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Hesabu za Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2021.