OCC Doctors
Senior Member
- Jul 20, 2018
- 113
- 172
Kamba ya kitovu kumzunguka mtoto shingoni kabla ya kuzaliwa (nuchal cord), matatizo yanaweza kujumuisha shida ya kupumua, na kuzaa mtoto aliyekufa.
Kamba ya kitovu inaweza kumzunguka mtoto kwa ulegevu (loose), na inaweza kumzunguka mtoto kisha ikamkaza (tight), na inaweza kumzunguka mtoto mara mbili (double nuchal cord) ambapo huwa ni ngumu kwa mtoto kujinasua.
Mara nyingi kunahusishwa na hatari kubwa zaidi ikiwemo uharibifu wa ubongo wa muda mrefu au kupooza kwa ubongo kunaweza kutokea.

Kikawiada Kamba ya kitovu hulindwa na mafuta laini yaitwayo 'Wharton's jelly'. Husaidia kamba isijifunge fundo ili mtoto awe salama bila kujali ni kiasi gani anajikunyata na kujipindua ndani ya tumbo la mama yake.
Inapotokea kamba ya kitovu ina upungufu wa mafuta hayo laini (insufficient Wharton’s jelly), hiyo inafanya uwezekano wa kamba kujifunga fundo au kumzunguka mtoto shingoni (Nuchal Cord ).
Hivyo basi, kamba itamzunguka mtoto ikiwa ni watoto mapacha, kuwepo kwa maji mengi ya uzazi, kamba kuwa ndefu na yenye muundo duni.
View attachment 2726398