Kambarage Stadium kama Old Traford/Sansiro/Giusepe meaza

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Viwanja tajwa hapo juu ni kati ya viwanja vigumu sana timu ngeni kwenda na kupata matokeo mazuri kipindi Ac Milan,Inter milan na Manchester united zilipokuwa kwenye ubora wao...

Imebidi nivifananishe Viwanja hivyo na kiwanja cha KAMBARAGE STADIUM kilichoko Shinyanga kinachotumiwa na STAND UNITED aka wapiga debe kwani tangu msimu uanze pamekuwa pagumu sana kwa timu za mikoani kupata matokeo mazuri pale hata ya sare tu.

Alianza YANGA akala kimoja,Leo tena AZAM kala kimoja.

Tunasubiria Simba kama ataweza kuvunja mwiko wa Stand united kutopoteza mchezo wowote dimba la Kambarage

Pia tumbumbuke Stand United ndo timu ambayo haijapoteza mchezo wowote mpaka sasa imecheza michezo tisa ikiwa na point 19 Nyuma ya Simba.

Hongereni Stand united.
 
Simba kapoteza mchezo gan? Et stand ndo timu haijapoteza mchezo
Huyu mleta mada kanishangaza kweli.. Anadhani kwa kua timu zao zimepokea vipigo basi na Simba atafungwa.. Simba tumejipanga sana msimu huu.. Huyo stand wao tutampiga goli nyingi kama wamesimama katika uwanja wao.. mbele ya mashabiki wao, na hawataamini.
 
Nimeongelea stand united zaidi nashukuru kutujuza pia kwamba simba hawajapoteza mchezo wwte hongereni watani
 
Huyu mleta mada kanishangaza kweli.. Anadhani kwa kua timu zao zimepokea vipigo basi na Simba atafungwa.. Simba tumejipanga sana msimu huu.. Huyo stand wao tutampiga goli nyingi kama wamesimama katika uwanja wao.. mbele ya mashabiki wao, na hawataamini.
Sio mbaya ndugu naona msimu huu mmeanza na moto mjitahd na nyie mpande ndege mwakani
 
Sisi lengo letu kuu ni kuchukua ubingwa tukiwa hatujapoteza mechi hata moja.. Hayo ya kupanda ndege yatafuata baadae.
 
Tusubiri tuone Ndugu ndo kama game za tisa ivi safar bado ndefu mkiweza itakua vizuri pia...ukibeba ubingwa automatic kifuatacho ni kupanda Ndege
 
Sisi tutapanda meli.. [emoji2] [emoji2]
 
Simba hatoki kambarage. Yan ushindi wa simba kambarage ni droo
 
Kwa kumbukumbu zangu simba alishawai kula kisago pale kambarage...tena Liewig atakua na hasira nao sana
 
Yeah alkula moja bila msimu uliopita hapo kambarage. Simba hana historia nzur kwa stand ktk mechi zote walizokutana.
 
Hiyo historia ilikuwepo hata Mbeya.. Ila huu mwiko tumeuvunja rasmi Jana.
 
Back
Top Bottom