Kambi maalum na mafunzo ya matibabu ya maumivu ya magoti na mabega kuelekea michuano ya AFCON 2027

Kambi maalum na mafunzo ya matibabu ya maumivu ya magoti na mabega kuelekea michuano ya AFCON 2027

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
KAMBI MAALUM NA MAFUNZO YA MATIBABU YA MAUMIVU YA MAGOTI NA MABEGA KUELEKEA MICHUANO YA AFCON 2027

Dar es Salaam: 07/09/2026

Uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) unapenda kuutaarifu umma kuwa, kwa kushirikiana na madaktari bingwa na bobezi wa magoti na mabega kutoka Uingereza, itaendesha kambi maalum pamoja na mafunzo ya matibabu ya maumivu na majeraha ya magoti na mabega kwa wanamichezo.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya utoaji wa huduma za afya na tiba kwa wanamichezo kuelekea Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, itakayoandaliwa kwa pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda. Mafunzo yatawakutanisha wataalamu wa afya kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Uingereza kwa lengo la kubadilishana uzoefu, kuongeza ujuzi na kuimarisha uwezo wa matibabu ya maumivu na majeraha ya magoti na mabega ambapo mafunzo yatafanyika MOI tarehe 14-15 Septemba 2026.

Kabla ya mafunzo hayo, MOI itaendesha kambi maalum ya uchunguzi na ushauri wa kitabibu tarehe 10-11 Septemba 2026, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 11:00 jioni, katika kitengo cha wagonjwa wa nje MOI (OPD).

Kupitia taarifa hii, MOI inawaalika Watanzania wote wenye changamoto za maumivu au majeraha ya magoti na mabega kufika katika Taasisi ya MOI katika tarehe na muda uliotajwa, ili kupatiwa uchunguzi na ushauri kutoka kwa madaktari bingwa na wabobezi wa Tanzania kwa kushirikiana na wenzao kutoka Uingereza.

Wananchi wenye changamoto hizo wanahimizwa kutumia fursa hii muhimu kupata ushauri wa kitaalamu na maelekezo kuhusu matibabu sahihi ya maumivu ya magoti na mabega hususani kwa wanamichezo. Kwa taarifa zaidi wasiliana nasi kupitia 0655982997, 0713439493

Imetolewa na
Patrick Mvungi Meneja Uhusiano- MOI


IMG-20260907-WA0015.jpg
 
Back
Top Bottom